Napendekeza iundwe Tume Huru ya kuchunguza kifo cha Hayati Magufuli

Sisi tunataka tume ya kuwatafuta wakina Azori na Ben Saanane.

Raia tuna shuku mengi mtaani, mtu mzima hapotei ni anasahau njia tu ila hawa jamaa eti wamepotea tena wamepotea Tanzania hatuwaoni.

Hivi inakuingia akilini kuwa raia wote karibu milioni 55 hawajawaona hawa ndugu zetu?
 
Huyo magufuli ndio nani mpaka afanyiwe uchunguzi yeye tu?

Hebu tuondoleeni uharo hapa.

Watanzania milioni 60 wanafurahia mtesi wao kufa wewe unaleta habari za uchunguzi
Watu wengine, hivi kwanini usijibu hoja mpaka utumie lugha zisizo faa. Limtokaro mtu ndo lijazalo moyo wake. Hata mawazo ulotoa ni uharo tu.
 
😀
 
Hata km kauwawa they won’t tell you...sio kwania mbaya bali ni kwa kukulinda wewe..

Jiulize tu wangetangaza kauwawa pangekalika?!
Jitahidi uwe raisi wewe halafu uone km shughuli hio ya tume ungeifanya
 
Jambo usilolijua ni sawa na usiku wa giza. Unachoandika hata sikuelewi.
Samia pia hukumuelewa sasa waliomuelewa huwezi waelewa yaani.
Unaandika maelezo mengi sana ila sentensi mbili tu za mwanzo zinatafsiri yanayofata kuwa ni majibu mradi umejibu.

NIMALIZE KWA KUSEMA SAMIA AMESHAELEZA SABABU YA KIFO NA JESHI LIMEMUELEWA.
 
Hivi wakiunda time ya kuchunguza kifo cha mkapa kabla kuna makosa?....Ni vyema wakaunda tume huru ya kuchunguza kifa cha mkapa then waliompiga lissu risasi then ifuate ya Jpm
Hapana hapana, kama ni kuchunguzwa nani kamuua nani basi na waanze ni nani hasa alikuwa behind kumuua rais wa kwanza wa zanzibar Abeid Amani Karume kisha wafuatilie ni nani hasa alikuwa behind kumuua Sokoine.
 
Isaidie nini hiyo tume?

TUunde tume ya kuchunguza namna ya kuchunguza vifo , kuzuia vifo .
 
Hadi leo sijauelewa ule "moshi" ulitokea wapi?!! ni kweli?! hakika ule moshi ulimuumiza mpendwa wetu, ila sijaelewa nini haswa kilitokea huko Ntwara!
 
kuandika mengi
si hoja, shida ni uvivu wako wa kusoma. Ndo maana unajibu havieleweki. Hujui kujenga hoja kwa misingi ya kisheria. Bali umejazwa na ushabiki ukidhani huyo samia atakuona weye wa maana.
Hoja ya kuundwa Tume huru itaendelea na haitakufa na ipo siku yatafanyika. Samia si Mungu na muamuzi wa yote, ni binadamu wa kawaida, alie pewa dhamana ya Urais kuwaongoza watanzania. Si mbaguzi ni mama alie na akili na mwelewa pia msikivu. Na ukubali kukosolewa.
ya kesho huyajui.
Nasisitiza kamati huru iundwe kuchunguza kifo cha Magufuli, kama unaumia umia.
 
Mwache mwendazake ameisha endazake! Raisi Samia Hassn Suluhu katuambia amekufa kwa tatizo la moyo. Una maana alitudanganya waTanzania? Una maana Raisi muongo? Acha hizo!!!!
 
Watanzania hao wenye shuku na uchunguzi juu ya kifo cha mpendwa wetu JPM huwezi kuwakuta JAMII FORUM au TWITTER tuko wachache

Wengi sana hawana ACCESS ya hii mitandao miwili.
Ben ,Azory , Kanguye na wengine hawakuwa binadamu ..Nyie watoto wa Marehemu kaeni kwa kutulia tu
 
Napendekeza Tume ya kuchunguza jinsi ya Kumfufua Raisi Magufuli iongozwe na na Nabii Tito
Msikilize hapa anavyotoa ufafanuzi👇

 
Nasisitiza kamati huru iundwe kuchunguza kifo cha Magufuli, kama unaumia umia.
Msisitizo wako hauna maana kama Samia na jeshi lake hawaelewi hizo propaganda.

Hoja ya kuumia ni hoja ya kimuhemko kwa mtu binafsi haionyeshi umuhimu wowote wa kuanzishwa tume huru kwa anayetakiwa kuiunda.
 


Mkuu Tuane na tume za kuchunguza 1.Kupotea kwa Ben Saa 2. Kupotea kwa yule mwandishi wa habari, 3. Kifo cha mwanafunzi Aquilina, 4. Kushambuliwa kwa risasi Tundu Lisu, 5. Miili iliyo opolewa mto Ruvu, Kura feki zilizokamatwa wakati wa uchaguzi 2020, Sakata la wabunge 19 waliofukuzwa uanachama chadema. 6. Wasiojulikana waliokuwa wanateka watu ni nani na wakitumwa na nani.
Baada ya hapo mkuu kutakuwa na uhalali wa tume huru kuchunguza kifo cha mwendazake.
 
Kwani kuna uchunguzi ulishafanyika?? mbona mleta mada anasema "iundwe tume kuchunguza upya"!!!!!!
 
Yawezekana una hoja ya msingi na bila shaka kama kweli tume itaundwa utasaidia sana. Lakini kwa ulinzi aliokuwa nao JPM wa vikosi vya usalama na wale wataalam wa Gamboshi waliotangaza kuwa kama angeokea mtu kugombea kiti cha urais kum-challenge JMP wangeshughulikia sidhani kama wangemuacha mwanadamu achezee uhai wa JPM. Unasemaje juu ya swala la ulinzi na usalama? Ina maana huna imani na timu ile? Tuanzie hapo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…