Napendekeza iundwe Tume Huru ya kuchunguza kifo cha Hayati Magufuli

Napendekeza iundwe Tume Huru ya kuchunguza kifo cha Hayati Magufuli

Kuna mdada mmoja alipendekeza kaburi lizilibwe kwa nondo kabisa asijetoka
Hahahaha. Yaani angejua mtaani kulivyo na furaha angekaa kimya. Waweke jiwe kubwa mno juu aisee.
 
Kwani mlikua hamjui anategemea Mashine ya mzungu kusukuma damu? Yye anawachochea muwachukie wazungu huku yye anapumua kwa msaada wa beberu. Sasa mashine ikifeli unatafuta mchawi? Kejeli zote zile hta kutengeneza mashine ya kusukuma damu humi nchi alishindwa?

Mnafurahisha
😀😀😀😀😀😀
 
WAPO watakao amin mimi binafs ningependa kupata hata kidogo dokezo la chanzo cha ule mosh
Wazee wa Korosho walimkataa. Ile hasara ya Korosho waliopata angerudi kipindi cha kampeni angetandikwa moto kabisa. Bora Machale yalimcheza haikwenda na badala yake walimzuia Lissu asiende kutema Cheche kule. Kweli kama udikteta tuliuona na hakika iwe jua au mvua hakuna mtu kutoka Ile kanda atateuliwa kuongoza hii nchi. Marehemu baba wa Taifa alionya baadhi ya makabila kupewa Urais wa nchi ikiwemo Sukuma. Huyu mzee alikuwa ni genius kabisa. Tulichokipata kwa Mwendazake tunaomba kisitokeee tena katika historia ya marais wa hii nchi.
 
Kwa hiyo tupoteze muda na fedha kuhangaika na mzoga wa shetani
 
KUMBUKA JAMBO HILI;

Hakuna maisha hata ya mtu mmoja yasiyo na thamani...

Uhai wa mtu yeyote ni Wa thamani kubwa sana...

Yeye hakulijua hili. Alichukulia maisha ya wananchi wengine hayamuhusu kama kiongozi mkuu wa nchi...

Alisahau kuwa na yeye ipo siku angekufa kifo cha kawaida na cha aibu kabisa...

Alichukulia kuwa maisha ya wengine ni takataka tu, na kwamba yake yeye, ya familia yake, ndugu zake, na ya rafiki zake tu ndiyo yana thamani zaidi kuliko ya wengine hususani waliokuwa wanampinga au kutokukubaliana naye ktk baadhi ya mambo/maswala....

Hili lilikuwa kosa. Hiki ndicho chanzo cha kifo na mauti yake. Hakuna mchawi nje ya hili...!!

HIVYO KAMA MNATAKA HIVYO NA ILI KILA MTU ATENDEWE HAKI; basi haya yafanyike kwanza;

1. Iundwe kwanza tume ya kijaji kuchunguza chanzo cha kushambuliwa Tundu A. M Lissu kwa risasi kwa lengo la kumuua mchana kweupe katikati ya mji wa Dodoma kwenye makazi ya viongozi wa ngazi za juu wa serikali mwaka 2017 wakati wa utawala wake unayetaka aundiwe tume eti ili kuchunguza...

2. Iundwe tume huru ya kijaji kwanza ili kuchunguza vifo vya utata vya wananchi wengi wakati wa utawala wake; watu waliotekwa na na kupotezwa pasipo serikali yake kutilia maanani huku majibu yakiwa rahisi tu kuwa;
"....ameuwawa au kupigwa risasi au kupotezwa na watu 'wasiojulikana'..."

Sasa ni wakati wa kuwajua hawa "wasiojulikana" walikuwa kina nani...

Ni wazi kuwa "WASIOJULIKANA" ndiyo waliomuua..!! Si aliwalea na kuwalisha, akawalipa na mshahara mnono na kuwa na silaha mwenyewe bwana...? Au uongo?

3. Mwisho iko hivi;

"...AUAE KWA UPANGA, NAYE VIVYO HIVYO KATIKA SAA NA WAKATI ASIODHANI, ATAUWAWA AU KUFA KIFO CHA NAMNA ILEILE CHA UPANGA...!!"

Karma is always a bitch...
Big up
 
MIMI NASHAURI IUNDWE TUME KWANZA YA KUCHUNGUZA KIFO CHA MKAPA,MPAKA LEO SINA AMANI KWA JINSI ALIVYOKUFA GHAFLA MWEZI ULE JULY KABLA YA UCHAGUZI,NA MAZISHI YAKE KUFANYIKA HARAKA HARAKA GHAFLA.....!
Bila hata wananchi kutangaziwa rasmi na serikali kuhusu chanzo cha kifo chake. Ukweli ilileta walakini mno. Na baadaye kampeni kuendelea kama vile hakuna msiba na kupeana majogoo njiani.

Malipo ni hapa hapa duniani.
 
nyungu zote zimetupwa majalalani - hiki ndicho kiwango cha unafiki cha baadhi ya watu hasa wanasiasa!! wapiga nyungu wote sasa hivi wapo na mama kuipokea report ya chanjo.

Na walivaa barakoa kiroho safi
 
Wewe ni mpumbavu na mzandiki!

Kwanini walipokuwa wakitekwa watu na kuuawa ulikuwa hutaki tume huru ya kuchunguza matukio hayo?
Iundwe kwanza tume ya kuchunguza aliyemteka Ben saanane, Azor gwanda, waliomshambulia Mh Lisu, uchunguzi juu ya zile maiti zilizokuwa zinaonekana fukweni zikiwa kwenye viroba pamoja na mateso waliyokuwa wakipewa wafungwa wa kisiasa kipindi cha magufuli.
Hakuna mtanzania mwenye haki zaidi ya mwingine! Kama ni uchunguzi tutaanza kwa namba...

Nyie watu acheni ubaguzi na kujiona wa muhimu kuliko mliokuwa mkiwapoteza
Huu uzi ulitakiwa kufungiwa hapa.

Nashangaa kuna comments 400+ mbele.

Sizisomi, for me, uzi umefungwa na hii reply mujarab kabisa.
 
Inaonekana una taarifa sahihi na kwa kuzipeleka hupajui! Hapa sio mahali pake. Zipeleke kwa igp au rpc aliye jirani na ulipo atazipokea na kuzifanyia kazi na majibu utayapata!
Nikutahadharishe tu kuwa; hili kosa la kutishia amani na usalama wa nchi adhabu yake unaijua? Sijakutisha Bali nimekusaidia kukupa elimu na kukuambia kuwa, " umejificha katikati ya uwanja wa Mpira yaani katikati ya dimba"! Wanakuona ujue!
Mwambie KABISA kuwa IP ya simu na latitude na longitude ziko captured kimawasiliano. Unakamatwa kama kuku
 
Well
Si wewe pekee uliefutiwa uzi wa aina hio humu nakumbuka kuna mshiriki mmoja alikuja na mada " Utata juu ya kifo cha Magufuli " pia waliufuta ule uzi, alielezea vyema sana na utata wenyewe uligusia kwenye ;

1. Hujuma katik kifaa cha pacemaker
2. Ujio wa wageni kutoka china
3. psu ndani ya psu

Au tutegemee kuna utata zaidi ambao haukuzungumwa hapo

Matukio yanayozalisha maswali ( ? ) ni mengi ikiwemo hilo taarifa za mgonjwa kuvuja hata kabla ya kifo na mbaya zaidi circle yake ( PM, Makamu, Wakuu wa mikoa nk ) haikua na taarifa na kama walipewa basi ni za uongo.

Hivi unadhani ni kweli Chalamila, Majariwa na Makamu walikua wanajua kuwa mzee amefariki ? ALAFU wao wakaamua tuu kusema yuko anapiga kazi ama yupo nimewasiliana nae. Inawezekana ?

Mbaya zaidi mtu tuu wa nje kabisa ya mfumo yuko full detailed na anatoa dhihaka juu ( Lema, Lissu na wengineo )

Mpaka taarifa za hayati kusafirshwa kwenda kenya walilijua and sishangai Kigogo kuwa na kibendera cha kenya kwenye account yake, hakipo kwa bahat mbaya

Kuna mambo mengi kweli yana leta utata.

Kuna umuhimu wa kuundwa Tume ituletee majibu, Lakin question comes what if they will lie ?
Mpaka kumuua kama ni kweli wanadhani hivyo ujue siyo jambo la mchezo. Tutafakari kwa kina ili Rais mwingine asijerudia kosa.
 
Endelea kusubiri kama unategemea mama kuja kupiga kampeni chumbani kwako!!! Sisi wananchi wapiga kura tunamuelewa sana na tunasema mama mitano, mitano na mitano tena, ikiwezekana maisha kabisa.
With all my love. Cute reply
 
Mwambie KABISA kuwa IP ya simu na latitude na longitude ziko captured kimawasiliano. Unakamatwa kama kuku
Zogwale
Hawa vijana watafuta matatizo na shida za kujitakia kwa ujira mdogo waliolipwa na wajinga wachache. Siku jumba bovu liwaangukie watajua kuwa hawajui. Hivi walishajiuliza maudhui ya uwepo wa tcra? Tuwape muda tu kwani wanapeleka msiba na kilio kwao kwa ujira usiokidhi bando la wiki!
Mwambie KABISA kuwa IP ya simu na latitude na longitude ziko captured kimawasiliano. Unakamatwa kama kuku
Zogwale
Hawa vijana wanaitumikia na wanasiasa uchwara wasiojitambua na wenye malengo ya kutawala ili wakwapue watawaachia msala pindi kikiwasanukia.
 
Marehemu meko katika uhai wake alikuwa anaamini juu ya tume huru?? Kama walimuua walifanya vizuri Sana wanastahili nishani kabsa
 
Habar watanzania lengo langu la kuanzisha huu uzi si kwa Nia Mbaya ila nikutaka tu Kumaliza Maswali ya Watanzania wengi wanao shuku kua Hayat kafanyiwa hujuma.

Baada ya kuona mambo mengi Yanayo endelea kwenye mitandao ya kijamii na mitaani. ni wazi kabisa Baadh ya watanzania walio wengi Wana shuku kifo cha Hayat Magufuli na kudhan kua kifo chake kina Hujuma.

Serikal iheshimu mawazo ya watanzania tunao tilia shaka kifo cha Rais wetu na izingatie kwa kuunda Tume huru ya uchunguzi.

Mimi Binafsi nikikumbuka Tukio la ule Moshi uliomfata Hayat Magufuli Mtwara alipokua kwenye Gari bila kujulikana wapi umetokea na kuzua Taharuki nazid kua na mashaka kua Huenda zile zilikua baadhi ya mbinu za kutaka kujaribu na zilishindwa Lakini waliojaribu hawakuacha.

Pia wasiwas wetu unakua mwingi baada ya Habari kua nyingi za magufuli kafarik kabla hata ya serikal kutangaza huku picha za Gar la mait ambalo lilibeba mwili kusambazwa kwenye mitandao ya kijamii

Kwanini Kina Tundulisu na kigogo walikua wanapata taarifa na walikua na uhakika kabisa kua mzee lazima afe na asipo na wengine kusema kabisa mzee kafa

Kwanini kifo chake walikitangaza Adui zake uku wakisherekea ushind

Kwanini kabla Magufuli yupo Hai viongoz walianguka kama kuku Tena wa karibu yake ila baada ya yeye kufa Hamna kiongoz hata mmoja alie kufa?

Huwezi kusema ule ulikua uchawi sababu hakuna uchawi na wala siamini uchawi kama upo.

Sasa ili kujiridhisha Basi serikal ifanye uchunguzi na uchunguzi uwe wa wazi ili kufuta hii shauku ya Baadhi ya watu kwani ikiendelea ivi na serikal kukaa kimia huwezi jua Baadaye itakua na madhara gani pia huto jua maadui baadae wanaweza kuutumia huu uvumi kama silaha so nibora serikal ilimalize kwanza ili swala kwani kila siku mambo yanazid kupamba moto.

Video ya tukio la moshi hio apo chini.

Kalale tena
 
Hoja inaungwa mkono na ishirikishe watalaamu wafuatao bila kuchomeka mwanasiasa au mwanaharakati wa aina yoyote
1. Cybercrime/Cyber-security & IT/Ethical Hacking (Forensics)
2. Madaktari bingwa wa mifumo ya umeme wa moyo (pacemaker operative & troubleshooting experts) na human anatomy
3. Wanasheria
4. Wanausalama
5. Majaji wabobezi
6. Wapelelezi wasio na mfungamano na upande wowote

NB: Bunge, Mahakama na Serikali wasubiri matokeo yake kwa uchambuzi na utekelezaji.

Wanaotoa madai haya wasipuuzwe kwa kuwa ni kutengeneza bomu kubwa sana ambalo kulipika kwake unaweza kupelekea utawala ulipo kuja kushitakiwa baadae kwa kukwamisha sauti za wananchi kusikilizwa kwa kuwa hawajavunja sheria yoyote.
Hoja namba mbili bila shaka wahusishwe mabeberu sivyo😂
 
Habar watanzania lengo langu la kuanzisha huu uzi si kwa Nia Mbaya ila nikutaka tu Kumaliza Maswali ya Watanzania wengi wanao shuku kua Hayat kafanyiwa hujuma.

Baada ya kuona mambo mengi Yanayo endelea kwenye mitandao ya kijamii na mitaani. ni wazi kabisa Baadh ya watanzania walio wengi Wana shuku kifo cha Hayat Magufuli na kudhan kua kifo chake kina Hujuma.

Serikal iheshimu mawazo ya watanzania tunao tilia shaka kifo cha Rais wetu na izingatie kwa kuunda Tume huru ya uchunguzi.

Mimi Binafsi nikikumbuka Tukio la ule Moshi uliomfata Hayat Magufuli Mtwara alipokua kwenye Gari bila kujulikana wapi umetokea na kuzua Taharuki nazid kua na mashaka kua Huenda zile zilikua baadhi ya mbinu za kutaka kujaribu na zilishindwa Lakini waliojaribu hawakuacha.

Pia wasiwas wetu unakua mwingi baada ya Habari kua nyingi za magufuli kafarik kabla hata ya serikal kutangaza huku picha za Gar la mait ambalo lilibeba mwili kusambazwa kwenye mitandao ya kijamii

Kwanini Kina Tundulisu na kigogo walikua wanapata taarifa na walikua na uhakika kabisa kua mzee lazima afe na asipo na wengine kusema kabisa mzee kafa

Kwanini kifo chake walikitangaza Adui zake uku wakisherekea ushind

Kwanini kabla Magufuli yupo Hai viongoz walianguka kama kuku Tena wa karibu yake ila baada ya yeye kufa Hamna kiongoz hata mmoja alie kufa?

Huwezi kusema ule ulikua uchawi sababu hakuna uchawi na wala siamini uchawi kama upo.

Sasa ili kujiridhisha Basi serikal ifanye uchunguzi na uchunguzi uwe wa wazi ili kufuta hii shauku ya Baadhi ya watu kwani ikiendelea ivi na serikal kukaa kimia huwezi jua Baadaye itakua na madhara gani pia huto jua maadui baadae wanaweza kuutumia huu uvumi kama silaha so nibora serikal ilimalize kwanza ili swala kwani kila siku mambo yanazid kupamba moto.

Video ya tukio la moshi hio apo chini.

ule moshi haikuwa mtwara bali lindi. Hivyo hoja hii haina mashiko sababu za kutokuwa mkweli
 
Back
Top Bottom