Watanzania hao wenye shuku na uchunguzi juu ya kifo cha mpendwa wetu JPM huwezi kuwakuta JAMII FORUM au TWITTER tuko wachache
Wengi sana hawana ACCESS ya hii mitandao miwili.
Kuna wakati niliandika uzi kuhusu serikali kuweka wazi kuhusu kifo cha Magufuli na si kutupaka mafuta kwa mgongo wa chupa. Uzi haukumaliza dakika hata moja ulifutwa. Sielewi kwanini. Nitasema hata tufiche ukweli ipo siku ukweli utajulikana.
Tumejenga utamaduni kwa kuwa kimya watu hawataki kuhoji. Ukihoji ni matusi. Lakini serikali ikiruhusu uchunguzi itasaidia kuondoa hayo yanayosemwa.
Mhe. Rais, alikataza kusiwe na uvumi bali watu wenye ushahidi wapeleke la sivyo hatua kali za kisheria zitachukuliwa.
Ni majuzi tu yule mwanaharakati Msiba alitamka wazi kuwa Magufuli aliuliwa. Mbona serikali ipo kimya haija mhoji msiba atoe ushahidi kuhusu tuhuma za Magufuli kuuwawa. Rais Samia anasema madaktari walitoa taarifa kafa kwa ugonjwa wa moyo, hivyo tusihoji kwa kua madaktari wamesema.
Rais anatufunga mdomo. Kwani mara ngapi madaktari udai mtu kafa kwa hiki, lakini uchunguzi ukifanyika unakuta ni tofauti. Mfano Yasin Arafat taarifa ya madaktari ilikuja kutofautiana na uchunguzi ulofanyika. Ikaonekana aliuwawa kwa sumu.
Nachojiuliza ni kwanin serikali ilificha kuumwa kwa Magufuli, na hata siku alokufa inadaiwa si hiyo. Haya yalisemwa wazi na Tundu Lissu pamoja na Lema.
Wakishirikiana na vyombo vya habari vya Kenya. Lissu katika twiter aliongea magufuli tayari kafa. Lakini vyombo vya ndani vilibaki kimya na serikali pia, ilificha.
Na viongozi walikanusha hasa Waziri Mkuu alidai Rais Magufuli alikuwa mzima na anachapa kazi. Baadae aliye kuwa mkuu wa mkoa Mbeya alisema kaongea na Rasi Magufuli yupo mzima anachapa kazi.
Makamu wa Rais akiwa ziarani Tanga, nae alisema Rais Magufuli hajambo na anawasalimia wananchi. Baadae akatoa kauli mtu ni kawaida kusumbuliwa na mafua ya hapa na pale.
Hii kauli ilileta utata!
Kesho yake Makamu wa Rais akatangaza msiba wa kitaifa. Kuwa Rais Magufuli kafariki.
Huu mtililiko unaleta mashaka na inaonesha serikali ilikuwa inaficha jambo. Kuanzia Rais Samia, Waziri Mkuu na alie kuwa RC Mbeya waombe masamaha kwa kupotosha jamii.
Pia serikali itueleze kwa nini Magufuli alikuwa anaumwa lakini ilifichwa. Wananchi walikosa haki ya kumuombea.
Haya yote yanafanya uhalali kuwa iundwe tume huru kuchunguza kifo cha Magufuli. Haya mambo ya kunyamazishana si haki. Kwanini serikali haitaki uchunguzi? Wakiguswa wanakuwa wakali?
Kunasiku watu watakwenda mahakamani kudai haki ya kuundwa tume huru kuchunguza kifo cha Magufuli.
Hatuwezi kuwa tunanyamaza wakati viongozi wa Taifa wanakufa, pasipo hata kujiridhisha?
Ifikie wakati kuwe na uchunguzi.
Rais Samia, leo watakupamba usifanye uchunguzi, lakini kikulacho siku zote ki nguoni mwako. Kuwa makini, usidhani kushabikiwa na kupigiwa makofi ndo kupendwa.