Napendekeza iundwe Tume Huru ya kuchunguza kifo cha Hayati Magufuli

MIMI NASHAURI IUNDWE TUME KWANZA YA KUCHUNGUZA KIFO CHA MKAPA,MPAKA LEO SINA AMANI KWA JINSI ALIVYOKUFA GHAFLA MWEZI ULE JULY KABLA YA UCHAGUZI,NA MAZISHI YAKE KUFANYIKA HARAKA HARAKA GHAFLA.....!
Mkuu,

Kifo cha BWM na JPM vinafanana kazi hiyo iende sambasamba hapo ndipo tabia ya watu fulani kuwa na hati ya kudhulumu uhai kupitia matatizo ya kiafya au ajali mtawaweza vinginevyo wataendelea kudunda sio kwa sababu ni wema hapana.

Kuna kiongozi mwandamizi kipindi cha kifo cha BWM alidai mbele ya vyombo vya habari kwamba hawakuwa na taarifa kwamba alikuwa anaumwa!!! Ni maajabu sana

Kiongozi yeyote wa nchi akistaafu anapangia mlinzi kutoka usalama wa taifa ambaye hutoa taarifa kwa DG kisha naye hupeleka kwa Rais

Tanzania kuna tatizo lipo mahala, siku mkibaini mtatamani hata kama unauwezo kuogombea Urais utaghairi maana ukishaingia Ilkulu kisha ukakuta mambo yanayohitaji marekebisha ka faida ya wananchi watakupangia mkakti zingiti ila sio bayana. Jiongoeze
 
Hii covid baada ya kumuondoa Magu ikapotea?
 
Then Tume itamfufua?
Muachage upopompo basi....
 
Hii covid baada ya kumuondoa Magu ikapotea?
nyungu zote zimetupwa majalalani - hiki ndicho kiwango cha unafiki cha baadhi ya watu hasa wanasiasa!! wapiga nyungu wote sasa hivi wapo na mama kuipokea report ya chanjo.

 
Rais kasema kifo kilitokana na 'Atrial Fiblilator' wewe unasema korona huoni kwamba tayari unakubailiana kwamba kuna haja ya kuwepo uchunguzi kuondoa nadharia yako hiyo au iliyotolewa na serikali?

Wengine mnadai kifaa cha 'Pacemaker' kiliisha muda wake maana aliwekewa mwaka 2011 na kilikuwa na uwezo wa kuishi kwa miaka 10!!

Je, kulikuwa hakuna uwezekano wa kuweka kingine kipya cha teklojia ya kisasa kama sio kumchoka kwa sababu binafsi?
 
Umetaja wale vichwa Nazi wote ndio wawepo huko

Sent from my vivo 1915 using JamiiForums mobile app
 
Watanzania hao wenye shuku na uchunguzi juu ya kifo cha mpendwa wetu JPM huwezi kuwakuta JAMII FORUM au TWITTER tuko wachache

Wengi sana hawana ACCESS ya hii mitandao miwili.
Kuna wakati niliandika uzi kuhusu serikali kuweka wazi kuhusu kifo cha Magufuli na si kutupaka mafuta kwa mgongo wa chupa. Uzi haukumaliza dakika hata moja ulifutwa. Sielewi kwanini. Nitasema hata tufiche ukweli ipo siku ukweli utajulikana.

Tumejenga utamaduni kwa kuwa kimya watu hawataki kuhoji. Ukihoji ni matusi. Lakini serikali ikiruhusu uchunguzi itasaidia kuondoa hayo yanayosemwa.
Mhe. Rais, alikataza kusiwe na uvumi bali watu wenye ushahidi wapeleke la sivyo hatua kali za kisheria zitachukuliwa.

Ni majuzi tu yule mwanaharakati Msiba alitamka wazi kuwa Magufuli aliuliwa. Mbona serikali ipo kimya haija mhoji msiba atoe ushahidi kuhusu tuhuma za Magufuli kuuwawa. Rais Samia anasema madaktari walitoa taarifa kafa kwa ugonjwa wa moyo, hivyo tusihoji kwa kua madaktari wamesema.

Rais anatufunga mdomo. Kwani mara ngapi madaktari udai mtu kafa kwa hiki, lakini uchunguzi ukifanyika unakuta ni tofauti. Mfano Yasin Arafat taarifa ya madaktari ilikuja kutofautiana na uchunguzi ulofanyika. Ikaonekana aliuwawa kwa sumu.

Nachojiuliza ni kwanin serikali ilificha kuumwa kwa Magufuli, na hata siku alokufa inadaiwa si hiyo. Haya yalisemwa wazi na Tundu Lissu pamoja na Lema.
Wakishirikiana na vyombo vya habari vya Kenya. Lissu katika twiter aliongea magufuli tayari kafa. Lakini vyombo vya ndani vilibaki kimya na serikali pia, ilificha.
Na viongozi walikanusha hasa Waziri Mkuu alidai Rais Magufuli alikuwa mzima na anachapa kazi. Baadae aliye kuwa mkuu wa mkoa Mbeya alisema kaongea na Rasi Magufuli yupo mzima anachapa kazi.

Makamu wa Rais akiwa ziarani Tanga, nae alisema Rais Magufuli hajambo na anawasalimia wananchi. Baadae akatoa kauli mtu ni kawaida kusumbuliwa na mafua ya hapa na pale.
Hii kauli ilileta utata!

Kesho yake Makamu wa Rais akatangaza msiba wa kitaifa. Kuwa Rais Magufuli kafariki.
Huu mtililiko unaleta mashaka na inaonesha serikali ilikuwa inaficha jambo. Kuanzia Rais Samia, Waziri Mkuu na alie kuwa RC Mbeya waombe masamaha kwa kupotosha jamii.

Pia serikali itueleze kwa nini Magufuli alikuwa anaumwa lakini ilifichwa. Wananchi walikosa haki ya kumuombea.
Haya yote yanafanya uhalali kuwa iundwe tume huru kuchunguza kifo cha Magufuli. Haya mambo ya kunyamazishana si haki. Kwanini serikali haitaki uchunguzi? Wakiguswa wanakuwa wakali?
Kunasiku watu watakwenda mahakamani kudai haki ya kuundwa tume huru kuchunguza kifo cha Magufuli.

Hatuwezi kuwa tunanyamaza wakati viongozi wa Taifa wanakufa, pasipo hata kujiridhisha?
Ifikie wakati kuwe na uchunguzi.
Rais Samia, leo watakupamba usifanye uchunguzi, lakini kikulacho siku zote ki nguoni mwako. Kuwa makini, usidhani kushabikiwa na kupigiwa makofi ndo kupendwa.
 
Imetoka hiyo ndugu yangu hairudi ngó! Mbona hukuomba iundwe tume ya kuchunguzi risasi zilizomiminwa kwa Lissu? Mwendazake mwache aende zake. Nyodo zilizidi. Alizingua wakamzingua mazima
 
Huo moshi ambao wewe una wasiwasi nao mwenyewe wala hakuwahi kuutilia shaka na ndio maana katika kipindi chake hakuunda tume sasa amekufa ndio iundwe tume?
Huo utakuwa upotevu/ matumizi mabaya ya pesa za wananchi pasipo sababu yoyote ya msingi
 

Maisha yetu yako mikononi mwa Mwenyezi Mungu. Hayo mengine pia anayajua na atayapatia majawabu yeye mwenyewe. Tumuache JPM apumzike kwa amani
 
Serikali ilishatoa sababu ya kifo cha marehemu! Uchunguzi wa nini tena? Lakini hilo halitoshi, Rais Mpya naye alisema kama watu wana ushahidi, basi waupeleke kwenye vyombo usika kwa ajili ya uchunguzi!

Hivyo kama una wasiwasi, anzisha uchunguzi wako wa chini kwa chini ili huo ukweli ubainike. Ila sisi wengine, tumeshakubali matokeo.
 
Nakuunga mkono mwazo yako na serikali inashauri isipuuze mkangaiko huu vinginvyo ijiandae kuadhibiwa. Hii sauti hatonyamazishwa kwa vitisho kamwe.

Wasikilizeni wanaolalamika wana hoja yenye mashiko ili mbaki salama jisafisheni hakuna namna ya ujanja wa matamko ya kisiasa.

Waziri mkuu, mkuu wa mkoa wa Mbeya, Balozi wa Tanzania Namibia na weza kuwatetea sio kosa lao.

Kuna kikundi kilishika hatamu ya ghafla baada ya hayati kufariki kisha huenda wakawa wanatoa mwongozo nini cha kusema kuzuia taharuki maana JPM alikuwa anatisha wakati akiwa na pumzi na walikuwa na hofu huenda pumzi ikamrudia ndio walitumia muda mrefu kujiridhisha kweli uhai umeondoka vinginevyo ingekuwa balaa, watu wangetamani ardhi iwameze kukwepa rungu lisilo na huruma.
 
Imetoka hiyo ndugu yangu hairudi ngó! Mbona hukuomba iundwe tume ya kuchunguzi risasi zilizomiminwa kwa Lissu? Mwendazake mwache aende zake. Nyodo zilizidi. Alizingua wakamzingua mazima
Kwahiyo baada ya tume hiyo kushindikana kuundwa mkaamua kulipilza kisasi kwa mlango wa nyuma baada ya kesi ya The Hague nayo kukwama?

Endeleeni kujibu tu sauti ya wanaohoji huku wakikusanya taarifa ni akina waliohusika
 
Kwahiyo baada ya tume hiyo kushindikana kuundwa mkaamua kulipilza kisasi kwa mlango wa nyuma baada ya kesi ya The Hague nayo kukwama?

Endeleeni kujibu tu sauti ya wanaohoji huku wakikusanya taarifa ni akina waliohusika
Kama The Hague imeshindikana, tume ya kuchunguza risasi zilipigwa na nani na walitumwa na nani imeshindikana, na mateso yanaendelea wewe unafikiri njia nyingine ingekuwa ipi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…