Napendekeza iundwe Tume Huru ya kuchunguza kifo cha Hayati Magufuli

Napendekeza iundwe Tume Huru ya kuchunguza kifo cha Hayati Magufuli

Yeye mbona alikataa kuchunguza tukio la Tundu Lisu kupigwa risasi. Pelekeni ujinga huko gengeni kwenu.
 
Kitu kizuri nilichokipenda kutoka kwa Magufuli ni Kushift upepo wa siasa ndani ya CCM ambazo ziliegemea zaidi majina ya Wanasiasa wa zamani na watoto wao.

By the way,Magufuli alizidiwa kete na mbaya zaidi alikiwa hana exposure kubwa ya mambo-wahuni wakamchezea keusi kekundu.

Maana sote tunatambua Nchi ni Rais na Katibu Mkuu Kiongozi-so,kwa akili za kawaida sio rahisi hao watu wawili wote wafariki kwa kupishana mwezi 1.Alianza kijazi 17 February,2021 kisha Magufuli 17 March,2021-hivi sio vifo vya kawaida lazima kuna watu katika hilo.

Ila ndio mchezo wa siasa duniani kote,ni either uwawahi maadui zako au wakuwahi.
Aliiletea dharau Corona nayo ikapita naye
 
Magufuli hakuwa muumini wa uchaguzi wa vifo au madhila ya wapinzani wake, sasa unataka watu wachunguze kifo chake ili iweje? Ukiua kwa upanga utakufa kwa upanga fullstop.
Point yake ni kwamba leo tutaona ni sawa tu kwa sababu ni Magufuli ila kesho mfano rais ni mwengine halafu watu kwa sababu zao binafsi wakaamua kurudia kumuondoa madarakani rais wa wakati huo kwa njia ile ile ya kwa Magufuli.
 
Kwa kadri mambo yanavyoenda nashauri uwepo uchunguzi huru. Inawezekana tukawa tunamchukia Magufuli lakini tukiacha wawepo watu ambao wanaweza muondoa Rais madarakani kwa njia hiyo.

Basi tufahamu hatupo salama na hatutakuwa salama. Leo hii tunaweza furahi au kasirika lakini tuangalie siku zijazo. Nadhani ili watu wawe na amani inapaswa kuwepo Tume Huru ya mchanganyiko, watu ithibitishe kilichomuua Dr. Magufuli ni nini, kisha maisha yaendelee.

Lakini tuangalie sana ikiwa kunaweza kukawa na jamii fulani inataka watu wake tu ndiyo watawale, basi tusijedhani tutakuja kuwa salama au kuendelea nchini. Haijalishi dini na kabila zetu, haijalishi vyama vyetu.
Tuanze kwanza na tume huru dhidi ya mashambulizi ya Tundu Lisu kwanza
 
Isifanyike sasa.

Maana wata toa ripoti ya mchongo ili kupoza watu.

Ngoja awamu flani ipite kwanza ndio tuhangaike na mambo kama hayo.
 
Wenyewe walishukuru ibilisi kurudi kuzimu
Utawala wa awamu hipi au rais yupi hakuwa ibilisi nchi hii au umezaliwa utawala wa Rais Magufuli ndo maana unaropoka tu.??Hivi unakumbuka watu waliofunikwa kwanye mashimo ya mgodi wa Bunyahuru kisa tu awataki kutoka,unakumbu watu walivyokula kichapo mtwara kisa tu wanadai gesi yao,unakumbuka kichapo zanzibar mpaka watu wakawa wakimbizi Mombasa kidongo chekundu,unakumbuku Dr Olimboka kilichokuta kisa tu mgomo wa madaktari,Unakumbuka mabomu Arusha kwenye mkutano wa Chadema.Sasa wewe endelea kuongelea Magufuri kwa maneno ya kinafiki kama hauna kichwa.
 
Back
Top Bottom