Kwa kadri mambo yanavyoenda nashauri uwepo uchunguzi huru. Inawezekana tukawa tunamchukia Magufuli lakini tukiacha wawepo watu ambao wanaweza muondoa Rais madarakani kwa njia hiyo.
Basi tufahamu hatupo salama na hatutakuwa salama. Leo hii tunaweza furahi au kasirika lakini tuangalie siku zijazo. Nadhani ili watu wawe na amani inapaswa kuwepo Tume Huru ya mchanganyiko, watu ithibitishe kilichomuua Dr. Magufuli ni nini, kisha maisha yaendelee.
Lakini tuangalie sana ikiwa kunaweza kukawa na jamii fulani inataka watu wake tu ndiyo watawale, basi tusijedhani tutakuja kuwa salama au kuendelea nchini. Haijalishi dini na kabila zetu, haijalishi vyama vyetu.