Napendekeza iundwe Tume Huru ya kuchunguza kifo cha Hayati Magufuli

Napendekeza iundwe Tume Huru ya kuchunguza kifo cha Hayati Magufuli

Sasa mbona tunaona anatajwa sana huyo Ben saa8 au Lissu tu? Kama Magufuli alidhuru na kuuwa watu wengi mbona kila siku tunasikia hao hao tu ndio maana nauliza kwani wao ni nani hapa Tz?
Kasome Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977 ibara ya 12 na 13 ndipo utaelewa kuwa Ben Saanane ni katika nchi hii.
 
Pasi na shaka itafahamika. Na kwa taarifa tu hii itakua siku mbaya mbaya sana kwa wahusika. Wapo watakaokufa kwa presha hapohapo. Yule alikua Rais wa nchi, hawezi kufa tu kama kuku. Cha msingi ni kuomba uzima na kusubiri. Waangalieni wanaosemekana kuhusika kwa sasa ni kama wamechanganyikiwa, usoni wanachekacheka kama kawaida yao ila mioyo yao inalia. Sidhani hata kama wanapata usingizi
Dua la kuku halimpati mwewe endelea tu kuota.
 
Habari Watanzania, lengo langu la kuanzisha huu uzi si kwa nia mbaya ila nikutaka tu kumaliza Maswali ya Watanzania wengi wanaoshuku kuwa Hayati Magufuli kafanyiwa hujuma.

Baada ya kuona mambo mengi yanayoendelea kwenye mitandao ya kijamii na mitaani, ni wazi kabisa baadhi ya watanzania walio wengi wanashuku kifo cha Hayati Magufuli na kudhani kuwa kifo chake kina hujuma.

Serikali iheshimu mawazo ya watanzania tunaotilia shaka kifo cha Rais wetu na izingatie kwa kuunda Tume huru ya uchunguzi.

Mimi Binafsi nikikumbuka tukio la ule Moshi uliomfuata Hayati Magufuli mkoani Mtwara alipokuwa kwenye Gari bila kujulikana wapi umetokea na kuzua Taharuki nazidi kuwa na mashaka kuwa huenda zile zilikuwa baadhi ya mbinu za kutaka kujaribu na zilishindwa Lakini waliojaribu hawakuacha.

Pia wasiwasi wetu unakuwa mwingi baada ya Habari kuwa nyingi za Hayati Magufuli kafariki kabla hata ya Serikali kutangaza huku picha za Gari la maiti ambalo lilibeba mwili kusambazwa kwenye mitandao ya kijamii

Kwanini kina Tundu Lissu na Kigogo walikuwa wanapata taarifa na walikuwa na uhakika kabisa kuwa mzee lazima afe na asipo na wengine kusema kabisa mzee kafa

Kwanini kabla Magufuli yupo hai viongozi walianguka kama kuku tena wa karibu yake ila baada ya yeye kufa hamna kiongozi hata mmoja aliyekufa?

Huwezi kusema ule ulikuwa uchawi sababu hakuna uchawi na wala siamini uchawi kama upo.

Sasa ili kujiridhisha basi serikal ifanye uchunguzi na uchunguzi uwe wa wazi ili kufuta hii shauku ya Baadhi ya watu kwani ikiendelea hivi na Serikal kukaa kimya huwezi jua Baadaye itakuwa na madhara gani pia hutojua maadui baadae wanaweza kuutumia huu uvumi kama silaha so ni bora Serikali ilimalize kwanza ili suala kwani kila siku mambo yanazidi kupamba moto.

Video ya tukio la moshi hiyo hapo chini.


Tena ayatolla Zitto anapaswa kuuawa kwa kuhumiwa kifo kwa kunyongwa mpaka kufa ikithibitika alishiriki kumuua Dkt Magufuli maana ndiye alikuwa mwanasiasa wa kwanza kuposti kumpongeza Rais Samia baada ya jaribio la Mtwara kushindikana.
 
Unaposema binaadamu wote ni sawa ni sawa katika nini? Wote ni kundi moja la binaadamu ila hatupo sawa na ndio maana hata humu anatajwa sana Bensaa8 na Lissu kuliko wengine tungekuwa sawa tu basi tungekuwa tunataja wengine sio hao tu?
Katika kula,kuvaa na makazi.Pia pumzi aliyo nayo kiongozi yoyote ndiyo ile ile aliyonayo hata mwehu.
 
Natarajia kugombea kiti cha urais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania hapo baadae mungu akipenda,

Pamoja na majukumu mazito nitakayo kuwa nayo kubwa zaidi ni uchunguzi wa vifo vya harakaharaka vya hawa ma legends wawili, yaani Magufuli na Mkapa

Nitatumia vyombo vya ndani na vya kimataifa kubaini ukweli,mengi yamesemwa,nami kama binadamu ninalo langu moyoni nitapenda kujiridhisha.

Ni hayo tu, jioni njema kwa wote jukwaani
 
Back
Top Bottom