1.) Ukusanyaji wa data unaweza ukafanyika kwa siku mbili, kitachochukua muda ni digitization toka kwenye karatasi kwenda kwenye tarakilishi, hivyo hapatakuwa na tatizo. Hata hivyo, hiyo Misingi unayodai itakiukwa (kama kweli ndio hiyo) , itasababisha vipi data zinazochukuliwa zisiwe za kweli? Kufanya kwa zaidi ya siku 2, kunafanya vipi data zisiwe za kweli?
2.) kama form4 leaver anaweza kutumia tehama, afisa mtendaji ambae nae ni mwajiriwa wa serikali anashindwaje kutumia tehema?
3.) Huo uelekezi ni upi sasa? Kama tunaamua kuwatumia wajumbe wa nyumba 10 si tutaunda maelekezo mapya amabayo yatafuatwa?
4.) Kwani Kufanya kwa muundo tofauti na ambao nauoendekeza kunakutofautisheje na ‘pipulation registers’, labda ungedadavua hilo
5.) Hizo qualities ulizotaja kwamba awe amehitimu chuo cha statustics, hao form 4 leavers mnaowaajiri kuhesabu watu, wamehitimu lini hiko chuo?
6.) Wewe unasema anatakiwa karani mdio aingize, na mimi nakuambia naoendekeza afisa mtendaji ndio aingize, hawawezi kushindwa kutumia kishkwambi.
7.) Hata tukitumia wajumbe wa nyumba 10, tutaweka muda elekezi na tutaufuta.
8.) Sawa
1. Sensa ya 2022 itafanyika kwa njia za kieletroniki 'digital' na siyo kwenye makaratasi rafiki yangu mbona hunielewi aisee? Zoezi la sensa kufanyika kwa siku nyingi kunapelekeaje data ziwe na dosari? Nimedokeza kwenye posti iliyopita pointi namba 1 nilipotaja aina ya makosa ya data ikiwemo duplicate. Hebu tufahamishe kwa
muda wa siku 10 utawezaje kudhibiti "dosari/makosa/mabadiliko" ya data yatakayotokana na hali zifuatazo:
- Idadi ya watoto watakaozaliwa
- Idadi ya watu watakaopoteza maisha "Watakaofariki"
- Idadi ya watu watakaohama nje ya EA
- Idadi ya watu watakaohamia ndani ya EA
- Matukio yasiyotarajiwa kama majanga "mafuriko nakadhalika" yatakayopelekea watu kuhama/kuhamia
- Idadi ya watu watakaokuwa safarini
Watakwimu waliangazia hayo na mengineyo ndo maana walithubutu kudhibiti muda maalumu wa kuhesabu watu, kwa muda wa siku moja au mbili hizo hali kitakwimu zinavumilika "error tolerance", lakini masiku yakizidi ni kipengele "mkanganyiko". Kitakwimu haswa huwa sensa inatakiwa ifanyike siku moja tu tena majira ya "asubuhi/alfajiri" au "jioni/usiku" kwa kuwa ni nyakati ambazo watu wengi hupatikana kwenye makazi yao, ama kama zoezi halitakamilika "incomplete coverage" ndani ya siku hiyo moja huongezwa siku nyingine "siku pili" ili kufukia mashino
2. Inalazimu tu kufanya hivyo kwa sababu uhitaji wa nguvu kazi ni mkubwa na zoezi linafanyika ndani ya muda mfupi mno Tanzania nzima, isingekuwa hivyo wangefanya kama walivyofanya kwenye dermacation, wangeajiri wataalamu wachache maalumu
Kwani hamna watu ambao ni illiteracy na wanajua kutumia hivyo vifaa vya tehama? Mbona hukujenga hoja kama hiyo? Elimu ya kidato cha 4 ni kigezo cha chini tu cha kitaaluma ambacho wameangazia na wakaona huenda mtu akiwa nacho anaweza akafit kuvaa jukumu husika, lakini pia wameweka hicho kigezo kwa lengo la kupata muitikio mkubwa wa maombi "kumbuka wanahitaji watu wengi sana", pia naamini wameweka hivyo kwa sababu wahitimu wengi wa madaraja ya juu ya elimu hawaishi vijijini, pia naamini watakuwa wameamua kutoa tu fursa kwa watu wa daraja hilo la kielimu "ni kundi kubwa la watu na wengi hawana kazi rasmi"
Kujua kutumia vifaa vya tehama hakuhusishi elimu peke yake tu, wala hakuhusishi kuajiriwa na serikali wala cheo cha mlengwa, achana na watendaji, mimi nawafahamu hadi wakuu wa Idara na Vitengo wa Taasisi mbalimbali za Serikali "hususani jinsia KE" wasiojua kutumia hivyo vifaa na baadhi yao wanaratibu mazoezi nyeti, au wanajua kutumia kidogo "beginner - basic" kiasi cha kuwafanya washindwe hata kuyaendea majukumu yao kwa weledi, mara nyingi majukumu yao yanayohusisha matumizi ya hivyo vifaa hufanywa na subordinate. Si wao tu, wapo watumishi wengi tu wasiojua kutumia hivyo vitu kwa uzuri "intermediate user", kumbuka tumeanza kutumia hivi vifaa miaka ya hivi karibuni tu maofisini. Kigezo hicho cha kielimu kimewekwa tu kama get pass "kiingilio" lakini haswa kinachokusudiwa ni kule kuweza kumudu yale majukumu. Elon Mask ana msemo wake "Siamini katika vyeti "makaratasi", ninaajiri kwa kuzingatia ujuzi hata kama mhusika hajasoma"
Fani ya Udhibiti wa Rasilimali Watu inazingatia na kuthamini sana madaraja ya kielimu, katika tasnia hii wanaamini katika kuleta ufanisi wa kazi ni vema au lazima kuajiri mtu aliyefuzu kwa daraja la kielimu nafasi husika "mbobezi/mtaalamu". Na ndo maana kwenye post iliyopita nilikutajia vigezo vya kielimu vya kitakwimu (fani husika) kwenye hizi fursa. Naamini kungekuwa na idadi kubwa ya hao wahitimu hapa nchini basi wangetumika kwenye hili zoezi na huenda hata kusingekuwa na mafunzo/semina ya masiku mengi (wale ni wabobezi na wengi wao wana uzoefu wa mazoezi ya aina hii/yanayohusisha matumizi ya vifaa hivyo). Na hata hivyo hicho siyo kigezo pekee kilichowekwa na kitakachozingatiwa kwenye kuchagua watu, vigezo ni vingi tu ikiwemo uzoefu nakadhalika. Na ukizingatia hata njia za kieletroniki za kukusanya taarifa/mapato/kodi ni changa hapa kwetu, hazijazoeleka
Fahamu: nafasi ya Maafisa Tehama iliyowekwa kwenye Tangazo hawatachukua yeyote isipokuwa wahitimu wenye vyeti husika vya Tehama tu. Na inaaminiwa watachukua watumishi wa Kitengo cha Tehama & Habari ngazi ya Halmashauri na kujazia wengine. Nafasi nyingine zilizosalia za ukarani na usimamizi ndo wenzangu na mimi tunaweza ambulia kwani majukumu haya mawili hatuhitaji tuwe tunajua sana kutumia vifaa vya tehama bali basic user tu
Jambo jingine, hizo kazi haziishii kwenye kujua kutumia vifaa vya tehama tu, kuna kujua kusoma ramani za kitakwimu na vikorombwezi vingine kidogo
Katika miko ya takwimu pia nafasi ya "ukusanyaji taarifa" huwa hazitakiwi zifanywe na watu wenye madaraja makubwa ya elimu (Shahada, Shahada ya Uzamili, Shahada ya Uzamivu nakadhalika) isipokuwa tu kama utafiti unaofanyika utakuwa complex sana na unaohitajia maarifa makubwa
3. Sijakuelewa. Ila kama ulikusudia miongozi ipo
4. Hmmm, siwezi kuelezea aisee, nimejitahidi kuandika maelezo mengi sana. Si rahisi ukanielewa kama hujachimba fani husika
5. Rejea pointi namba 2 juu nimejibu
6. Rejea pointi namba 2 juu nimejibu
Wewe ndo unasema hawawezi kushindwa, uhalisia tunaujua sisi tunaofanya nao kazi 24/7
7. Ushauri: Tafuta Mtakwimu akupitishepitishe kwenye vipengele muhimu, fani yao hii
8. Amani