Napendekeza kazi za kuhesabu idadi ya watu (Sensa 2022) ifanywe na wajumbe wa nyumba 10 , pesa zitakazookolewa zikajenge flyover TAZARA

Inaonesha unajua unachokiandika. Mweleze pia kuwa kuna makundi maalum ambayo mjumbe hawezi kuyaona mfano wamachinga ambao huwa wanahama hama. Tunaposema usiku wa sensa tunaanza kuhesabu saa 6 usiku. Tunazingira hata majumba ambayo huwa yanalaza watu mfano Kariakoo.

Sijaona sensa ambayo hili suala halijawahi kutokea ati wajumbe ndiyo wawe wahesabuji.

Mfahamishe kuwa kuna tofauti kati ya utafiti (survey) na sensa (census ). Tofauti moja ni sample based - idadi ndogo ya watu inawakilisha wengi, wakati sensa ni total coverage ya entire population.

Mwisho mfahamishe kuwa sensa pamoja na kutoa denominator ya kikokotoo kuhusu masuala ya watu, hutumika katika kutoa takwimu za kupanga mipango ya maendeleo. Tusisahau, nchi isiyotumia takwimu kupanga Maendeleo yake huwa ni mufilisi.

Kwa faida yake shirika la umoja wa mataifa UNFPA lilianzishwa kusidia nchi zote duniani kufanya sensa. Maana ni mazoezi mawili yanatimia fedha nyingi katika Nchi yeyote:
1. Vita na 2. Ni sensa
 

Umeeleza vizuri, ningeomba pia nawe unisaidie kumuelimisha eidha kwa maelezo au kwa kujibu maswali atakayouliza au aliyouliza kwenye posti zilizopita kwa lengo la kujenga uelewa wa pamoja. Ahsante na tupo pamoja rafiki
 
Umeeleza vizuri, ningeomba pia nawe unisaidie kumuelimisha eidha kwa maelezo au kwa kujibu maswali atakayouliza au aliyouliza kwenye posti zilizopita kwa lengo la kujenga uelewa wa pamoja. Ahsante na tupo pamoja rafiki
Mbona Umejibu sawia, wengine ni wapuuzi kama FRANCIS DA DON na huwezi kuwasaidia kwa hali yoyote!
 
Mawazo ya Mtu Mjinga haya unaaangalia interest zako tu hujui kuwa wajumbe hawajui hata maana ya Sensa maana 99% Ni brain washed waliokuwa waramba viatu vya Jpm
 
Mawazo ya Mtu Mjinga haya unaaangalia interest zako tu hujui kuwa wajumbe hawajui hata maana ya Sensa maana 99% Ni brain washed waliokuwa waramba viatu vya Jpm
Mjinga ni wewe unaeita wajumbe walamba viatu bila hoja yeyote ya msingi.
 
Kijana sensa hii ni sensa ya kidijitali na tayari sensa ya majaribio ilishafanyika na ikaja na utaratibu mzima wa jinsi sensa kuu itakavyofanyika.

Na hao watu wako watakuwa ni sehemu ya kufanikisha sensa hii kama watakuwa na sifa lakini wengine watakuwa kwenye kamati za sensa za ngazi mbalimbali ( so relax)

Lakini kama unataka ndio totally watumike kufanikisha hili kwa njia ya de jure hakiwezekani hicho kitu.

Mawazo yako hayana tija na yanalenga kudhoofisha taaluma za wasomi wetu waliotoa ushauri wa kuifanya sensa hii iwe ya kidijitali.

Vile vile maoni yako yanavyoonekana kama yanalenga kuhujumu taifa letu. Kama mtalaam mmoja alivyosema hapo juu kwamba sensa ni sawa na vita. So unataka kutuangamizia taifa letu kwa kuwa na takwimu za hovyo.

Aidha, ikumbukwe kuwa tukiharibu /tukikusanya takwimu za uongo kwenye sensa , Mipango yetu itaathirika kwa kipindi cha miaka 10 kwa kuwa sensa ndio hutoa baseline data za kila mwaka ambazo hutumika kupanga mipango yetu ikiwa ni pamoja na kugawa rasilimali, kupanga bajeti za serikali n.k

So nadhani umeelewa sasa umuhimu wa takwimu za sensa na kwanini hatuwatumii hao watu wako moja kwa moja japo yawezekana watatumika kwa njia tofauti ktk kufanikisha.

Vile vile, ikumbukwe kuwa kwenye sensa ya majaribio walitumika sana kusaidia kuwatembeza makarani kwenye kaya za watu. Na sensa hiyo ilitoa majawabu mazuri ya kuwatumia watu hao kama vile kuwa sehemu ya wajumbe wa kamati za sensa ngazi za mitaa/ vitongoji ( kama watu mashuhuri).

Salaam maleko
 
Na hao watu wako watakuwa ni sehemu ya kufanikisha sensa hii kama watakuwa na sifa lakini wengine watakuwa kwenye kamati za sensa za ngazi mbalimbali ( so relax)

Lakini kama unataka ndio totally watumike kufanikisha hili kwa

Nilisahau kugusia hili, zoezi lilitoa miongozo ya kuunda kamati za sensa katika ngazi ya Kata na Mitaa/Vijiji. Kwa nilivyofahamishwa watakaounda kamati hizo ni Watendaji, Wenyeviti, Walimu Wakuu, Maafisa Maendeleo Jamii, Watu maarufu katika eneo husika, Wajumbe nakadhalika. Wajumbe watakaokidhi vigezo vinavyohitajika ndo watajumuishwa, hivyo si wajumbe wote watakaoshiriki, ukizingatia idadi ya wanakamati katika ngazi ya Mtaa inaaminiwa haitazidi watu watano

Wankuru Nyankuru [emoji120]
 
Kwani kigezo cha kuweza kuhesabu watu ni kujua kutumia smartphone? Wao watakusanya data kwa analog, then itakuwa ni jukumu la afisa mtendaji ku-digitize na kutuma taarifa kwa mamlaka husika...
Sasa huoni hapo kazi itakuwa mara mbili mkuu? Wajumbe wakusanye data kwa analog, alaf watendaji wazibadili into digital.

Acha vijana wapige hiyo kazi. Hata serikali ikibana bajet , Hela zitaishia mikononi mwa wachache na sio kwa nchi
 
Sasa huoni hapo kazi itakuwa mara mbili mkuu? Wajumbe wakusanye data kwa analog, alaf watendaji wazibadili into digital.

Acha vijana wapige hiyo kazi. Hata serikali ikibana bajet , Hela zitaishia mikononi mwa wachache na sio kwa nchi
Kwani hizo tablet zinaokotwa chini ya muembe jamani, si pesa hiyo au? Mfano una maafisa laki 6 wa kuhesabu watu, uwanunulie kila mmoja tablet, jamani..
 
Afu wengine wabaki bila Ajira acheni vijana wapewe Ajira na wao waenjoy national cake
Sensa sio mbadala wa ajira. Tafuteni ajira. Ajira ya siku au wiki itakuwa suluhisho...? Kwa baadhi inaweza ikawa jiwe la msingi. Hata hivyo kwa kina "ngoswe" taabu na mashaka yataongezeka!

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
 
Labda ungesema mtendaji wa kitongoji, maana yule ni afisa wa serikali, lakini hawa mabalozi wanaochaguliwa kwa sifa ya uchawi au mwenye majini mengi no!

Lakini shida hio ni pesa, kila mtu anaitaka
 
Ivi huko daslam barabara haziwatoshi au mnataka kila mtu awe na yake?

Tanzania ni kubwa,nguvu kubwa kuelekezwa kwa hao panyaroad wasioridhika ni kuharibu resources.
 
 
Watanzania hampendi kuona pesa zikiingia mtaani umma wa watanzania wafaidi.

Ooooh Mara pesa hakuna mtaani[emoji28][emoji28][emoji28]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…