Inaonesha unajua unachokiandika. Mweleze pia kuwa kuna makundi maalum ambayo mjumbe hawezi kuyaona mfano wamachinga ambao huwa wanahama hama. Tunaposema usiku wa sensa tunaanza kuhesabu saa 6 usiku. Tunazingira hata majumba ambayo huwa yanalaza watu mfano Kariakoo.Sawa Mjumbe, nasubiri hiyo imla, ZINGATIA: Ni vema hoja zako zitajikita kwenye fani husika na siyo siasa na maoni hewa yasiyo na msingi egemezi
Kwenye fani ya takwimu kuna kauli mbiu mashuhuri isemayo pasina takwimu/data huna haki ya kuzungumza, kunielewa nilichomaanisha hapo kunalazimu ujue maana ya Statistics "singular/plural"
Fani: Population, Demography, Statistics, Economics, Planning
Sijaona sensa ambayo hili suala halijawahi kutokea ati wajumbe ndiyo wawe wahesabuji.
Mfahamishe kuwa kuna tofauti kati ya utafiti (survey) na sensa (census ). Tofauti moja ni sample based - idadi ndogo ya watu inawakilisha wengi, wakati sensa ni total coverage ya entire population.
Mwisho mfahamishe kuwa sensa pamoja na kutoa denominator ya kikokotoo kuhusu masuala ya watu, hutumika katika kutoa takwimu za kupanga mipango ya maendeleo. Tusisahau, nchi isiyotumia takwimu kupanga Maendeleo yake huwa ni mufilisi.
Kwa faida yake shirika la umoja wa mataifa UNFPA lilianzishwa kusidia nchi zote duniani kufanya sensa. Maana ni mazoezi mawili yanatimia fedha nyingi katika Nchi yeyote:
1. Vita na 2. Ni sensa