Napendekeza mfumo wa ‘Randomizer’ kwenye usajili wa ‘plate number’ za magari nchini

Malori ikifungwa vizuri tandamu namba A wa namba D akasome wajanja kwa sasa hawaagizi magari nje sana.
Ni kweli, pale Jangwani Fusi namba ‘A’ ndio zinaongoza kwa kupiga mzigo, gari inasukwa kama imetoka kiwandani, ila kwakuwa ni gari ya kazi, hakuna anaejali kuhusu namba. Shida ipo kwenye hizi za kutembelea, namba ‘A’ ni kama tusi hivi
 
 
Kwa hio unalalamikia serikali kushindwa kuuza cresta no A ..ulinunua uuze? Serikali haijakataza choma Moto nunua jingne
 
Kwa hio unalalamikia serikali kushindwa kuuza cresta no A ..ulinunua uuze? Serikali haijakataza choma Moto nunua jingne
Soma hoja uielewe ndugu. Japan anatajirika kwa kutuuzia mikangafu, kwanini unajua? Kwa sababu wao magari yao wakiyafanyia restoration (rangi, engine nk.) na kuwa kama moya, hapa nchini zikija zinapewa namba mpya kabisa, zile za zamani za Japan zinabaki hukohuko. Ila ukifanya restoration hapa bongo na kuifanya iwe kama mpya, unalazimika kutumia namba zile zile za zamani, sasa hapo ndipo mtihani ulipo, maana mtu atashindwa kurudishanpesa aliyotumia kwenye restoration kwa sababu namba ya zamani inasababisha kupata bei ndogo kwenye soko, hata kama gari ni mpya na ipo katika hali nzuri sawa na ya kiwandani.

Siku nyingine jadili kwa hoja na sio kama unamekali kitu kigumu, taahira wewe.
 
Nipo na namba A yangu iliingia 0km miaka hiyo maisha yanaendelea. Sijui nitaiuza lini? Ila nimependa idea ya car restoration. Nadhani mtumba wa Japan uliotumika TZ ukibadilishwa kwa kuwekewa engine mpya, gearbox mpya na ukawa pimped utatengeneza ajira iwapo utakuwa na soko. Na kama unavyosema, soko lipo affected na namba sababu wateja wengi wananunua magari si kwa usafiri tu bali na pride au showoff.
 
Wewe sasa umenielewa, yaani tuna export ajira kwenda Japan kwa sababu ya kijinga kabisa, hiyo gari yako namba A unaweza ukashindwa kuiza kwa bei nzuri, lakini hiko gari lingekuwa Japan halafu likapigwa rangi na kuservive engine nk, likija hapa bongo likapewa na ‘E’ ya sasa, unauza bei hata mara 10, sasa niambie, sisi ni mataahira au ni wendawazimu, just tell me!
 
Reactions: Tsh
Nimekuelewa boss ila tatizo ukifungua madirisha wanapita hadi nyoka, huu mfumo una loophole nyingi sana za wezi na matapeli but still upo sahihi sababu hatutakiwi kubaki nyuma sababu ya kuwaogopa wezi, bora kubadili fikra.
 
 
 
kwahiyo kila mkoa upewe mamlaka ya kufanya hivyo... tuunde vyombo kama mamlaka zamaji?

Usajili unafanywa na TRA, na Kila wilaya kwenye nchi hii ina ofisi ya TRA so nafkiri itakuwa rahisi tu kwa jambo hili wala hakuna haja ya kuunda vyombo Kama mamlaka za maji.
Gari zikisajiliwa kwa namna ya ushauri anaoutoa mdau kwanza plate number zitakuwa na mvuto. Ukiangalia kwa Africa number plate sinazo vutia niza South Africa, na wao wamesajili magari yao kimkoa.
 

Akunaga kitu kipya wala kizee ata iyo namba E ipo sku itakua nzee sa km ni unyonge ni kununua gar jipya kla namba mpya ikitoka iyo itakusaidia kuondoa unyonge,
Ila suala la kuuza gar nazan nyie wauza magar ndo muanze kutoa ushauri na elimu ya kutosha kwa wateja wenu wajue usajir sio ubora wala upya wa gar bali upya na ubora wa gar ni Engine,gear box nk
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…