Napendekeza mfumo wa ‘Randomizer’ kwenye usajili wa ‘plate number’ za magari nchini

Napendekeza mfumo wa ‘Randomizer’ kwenye usajili wa ‘plate number’ za magari nchini

wewe unaona kuuza gari lake tu ndicho kitu muhimu sana mpaka kuvuruga system nzima.

Mbona miaka yote toka tunapata uhuru namba zinaenda kwa mtiririko huo huo wa TZA ikiisha ndiyo inafata TZB, na bado watu waliuziana magari tu
Achana nae huyo mtoa post. Anataka kutupiga kwenye biashara yake ya magari.
 
Good idea, ila pia namba ziwe ‘randomized’ , zisionyeshe mtiririko wa kujua ipi imesajiliwa zamani na ipi imesajiliwa recently.
Mtakapotaka kuuziana gari lazima uoneshe kadi ya gari na pale kwenye gari ya gari juu kabisa wameandika "First Registration" huoni hapo mtu tayari ameshajua gari ilisajiliwa lini.
Ushauri wangu mtu anunue gari kutokana na hali yake na sio namba ya gari.
 
Shida si mtu anaenunua kuona mwaka wa kusajiliwa, shida ni pale unapoendesha gari mang’anyu barabarani halafu imeandikwa namba ‘A’, hicho ndiocho kinaketa shida hata watu kununua hizo namba ‘A’
 
Kwa hiyo " registration number" inaweza isitamkwe iwekwe "plate number"?
Namba ya usajili wa magari ndio inaweza ikatamkwa ‘plate number’ , ila namba ya usajili wa mwanafunzi chuoni huwezi tumia ‘plate number’, legeza ubongo
 
Shida si mtu anaenunua kuona mwaka wa kusajiliwa, shida ni pale unapoendesha gari mang’anyu barabarani halafu imeandikwa namba ‘A’, hicho ndiocho kinaketa shida hata watu kununua hizo namba ‘A’
Mawazo yako brother wewe unaendasha gari yako unayoipenda na kuiamini unapata wapi shida ya kuwaza kwa watu wengine ambao gari sio yao?
 
Namba ya usajili wa magari ndio inaweza ikatamkwa ‘plate number’ , ila namba ya usajili wa mwanafunzi chuoni huwezi tumia ‘plate number’, legeza ubongo
Sawa. Kwa hiyo nikisema "a car with a number Plate T 123 XYZ" nitakuwa Niko Sawa!?
 
wewe unaona kuuza gari lake tu ndicho kitu muhimu sana mpaka kuvuruga system nzima.

Mbona miaka yote toka tunapata uhuru namba zinaenda kwa mtiririko huo huo wa TZA ikiisha ndiyo inafata TZB, na bado watu waliuziana magari tu
Nazani hujamuelewa vizuri. Rudia Tena kusoma.

Lambda nikusaidie kidogo. Kutana na gari zote za mwaka 2004 ila kwa vile moja ni namba A haiwezi uzika haraka na kwa Bei ya Juu kama ilivyo namba D. Hizi zote ni used na unakuta matunzo ni yaleyale.
Kitu kingine ni uagizaji wa magari holela ambao unatumia pesa nyingi sana na kufanya pesa ikosekane mtaani. Wakati tungekuwa na mfumo mzuri tungekuwa tunanunua humuhumu kulingana na ubora wa gari wakati wa kununua. Hii ingeongeza mzunguko wa pesa kwa Raia.
 
Binafsi nadhani tungerudi kwenye utaratibu wa kusajili magari kutokana na mikoa yanapotoka na mwishoni herufi mbili zozote.Mfano wale wa Iringa,gari inaweza kuwa IR 2345 GN,kwa Dar Es Salaam ingekuwa kwa manispaa yatokapo mfano,Kinondoni ingekuwa KN 3124 TU.Pia hata uhalifu wa kutumia magari ungepungua.
Msumbji wanafanya hivyo katika kusajili magari wanazingatia mkoa
 
Back
Top Bottom