Napendekeza serikali iweke kipengele cha cheti cha JKT kwenye matangazo yote ya kazi katika Taasisi za kiserikali na utumishi

Upuuzi mtupu,kwanza hakuna uwezekano wa kila kijana kwenda jkt,nchi Haina uwezo wa kugharamia.
Pili,kama taasisi inataka engineer au doctor,mafunzo ya kulima,na kupiga kwata yanasaidia nini kwenye kazi yake?
Sasa hv tupo kwenye karne ya sayansi,na virtual technology,robotics,wewe unawapereka vijana jeshini kujifunza kulima,kufuga,kupiga kwata,na upuuzi mwingine wa mwaka 47,hayo madudu yatawasaidia nini kwenye maisha,tuliamibishwa wakitoka huko wataweza kujjisjiri kwenye kilimo Na ufugaji,hakuna kitu wanaishia kulanda landa mjini kama kuku wasio na vichwa na kupiga raia.
Program ya jkt ni nzuri,ila iboreshwe iwe ya kisasa.
Ni bora kuweka mafunzo ya lugha za kigeni kama kifaransa,kigerman,na mafunzo ya IT shuleni kuliko kupoteza muda na rasilimali huko polini
 
Bavicha wengi watakosa ajira sababu ni wavivu hawawezi kupitia JKT wao ni kukesha mitandaoni na kuilaumu serekali
 
Hao wez wte wa nchi hii pia walipita huko
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…