Napendekeza Serikali ya Tanzania ichapishe Noti za Shilingi Elfu (50,000) na Laki moja (100,000)

Napenda kutoa mapendekezo muhimu kwa Serikali ya Tanzania (GOT) na Benki Kuu ya Tanzania (BOT) kuhusu umuhimu wa kuchapisha noti mpya za Shilingi 50,000 na 100,000. Pendekezo hili lina lengo la kuongeza hadhi ya fedha nchini na kuleta faida za kiuchumi na kifedha kwa taifa letu.

1. Pendekezo langu la kwanza ni kwamba noti mpya za Shilingi 50,000 na 100,000 zitaongeza hadhi ya fedha nchini Tanzania. Kuwa na noti za thamani kubwa katika mzunguko wa fedha kunaweza kuimarisha sifa ya taifa letu katika jumuiya ya kimataifa na kuonyesha ustawi wa uchumi wetu. Nchi nyingi duniani zimechukua hatua kama hii ili kuboresha hadhi ya fedha zao na kuonyesha nguvu ya uchumi wao. Kwa kuongeza noti za Shilingi 50,000 na 100,000, Tanzania itajiweka katika kundi la nchi zinazofanya biashara kubwa na kuonesha kuwa ni taifa lenye nguvu na lenye uwezo mkubwa kiuchumi.

2. Kuwa na noti za thamani kubwa pia kunaweza kuchangia kuimarisha imani kwa wawekezaji na wadau wa kimataifa. Uwezo wa kuwa na noti za Shilingi 50,000 na 100,000 utaashiria kwamba Tanzania ni nchi yenye uchumi imara na inayoweza kushughulikia shughuli kubwa za kifedha. Hii itavutia uwekezaji na kuchochea maendeleo ya kiuchumi katika nchi yetu. Wawekezaji watakuwa na imani zaidi katika mfumo wetu wa fedha na watakuwa tayari kuwekeza katika miradi ya maendeleo na biashara mbalimbali. Hii itasaidia kuongeza fursa za ajira na kuchochea ukuaji wa uchumi wetu.

3. Noti mpya za Shilingi 50,000 na 100,000 pia zitawezesha shughuli za kifedha kuwa rahisi zaidi. Kuwa na noti za thamani kubwa kutawezesha mchakato wa malipo makubwa kwa urahisi na haraka zaidi. Biashara zinazohusisha miamala mikubwa zitaweza kufanya malipo kwa urahisi.

Ni matumaini yangu pendekezo hili litazingatiwa na Serikali ya Tanzania na Benki Kuu ya Tanzania kwa umakini na kufanyiwa tathmini ya kina.
Elimu yako imeishia kiwango gani.
 
Uchumi uimarike, hata hio elfu 10 & 5 hazitakiwi, note ya juu iwe ya Tsh 1000 ila iwe na nguvu.

Ukiwa na note za 100,000/ au 50,000/ ujue uchumi wako upo hoe have.

Kuna kitu walifanya Ghana na Zambia kutoa masifuri kwenye note zao na sio kuongeza.

Siku naagiza mzigo lusaka almost Tsh 1.8 M ,kuibadiri zikaja kwacha kama elfu kumi na nane hivi.
 
Enzi za Nyerere 1 usd ilifika sawa na 10 Tshs.

Kuongeza 000 kwenye noti, ni Ishara ya Uchumi kuingia shimoni.
 
Napenda kutoa mapendekezo muhimu kwa Serikali ya Tanzania (GOT) na Benki Kuu ya Tanzania (BOT) kuhusu umuhimu wa kuchapisha noti mpya za Shilingi 50,000 na 100,000. Pendekezo hili lina lengo la kuongeza hadhi ya fedha nchini na kuleta faida za kiuchumi na kifedha kwa taifa letu.

1. Pendekezo langu la kwanza ni kwamba noti mpya za Shilingi 50,000 na 100,000 zitaongeza hadhi ya fedha nchini Tanzania. Kuwa na noti za thamani kubwa katika mzunguko wa fedha kunaweza kuimarisha sifa ya taifa letu katika jumuiya ya kimataifa na kuonyesha ustawi wa uchumi wetu. Nchi nyingi duniani zimechukua hatua kama hii ili kuboresha hadhi ya fedha zao na kuonyesha nguvu ya uchumi wao. Kwa kuongeza noti za Shilingi 50,000 na 100,000, Tanzania itajiweka katika kundi la nchi zinazofanya biashara kubwa na kuonesha kuwa ni taifa lenye nguvu na lenye uwezo mkubwa kiuchumi.

2. Kuwa na noti za thamani kubwa pia kunaweza kuchangia kuimarisha imani kwa wawekezaji na wadau wa kimataifa. Uwezo wa kuwa na noti za Shilingi 50,000 na 100,000 utaashiria kwamba Tanzania ni nchi yenye uchumi imara na inayoweza kushughulikia shughuli kubwa za kifedha. Hii itavutia uwekezaji na kuchochea maendeleo ya kiuchumi katika nchi yetu. Wawekezaji watakuwa na imani zaidi katika mfumo wetu wa fedha na watakuwa tayari kuwekeza katika miradi ya maendeleo na biashara mbalimbali. Hii itasaidia kuongeza fursa za ajira na kuchochea ukuaji wa uchumi wetu.

3. Noti mpya za Shilingi 50,000 na 100,000 pia zitawezesha shughuli za kifedha kuwa rahisi zaidi. Kuwa na noti za thamani kubwa kutawezesha mchakato wa malipo makubwa kwa urahisi na haraka zaidi. Biashara zinazohusisha miamala mikubwa zitaweza kufanya malipo kwa urahisi.

Ni matumaini yangu pendekezo hili litazingatiwa na Serikali ya Tanzania na Benki Kuu ya Tanzania kwa umakini na kufanyiwa tathmini ya kina.
Kwa hio njia ya kuvutia wawekezaji ni kuwa na noti kubwa na wala sio kuweka mazingira bora?

Nchi zote uzalishaji ndio huongeza thamani ya pesa zao, hasa mauzo ya nje sasa nchi tumejaa vilaza lazima tusapoti ujinga.

Tuna import kila kitu then tunatarajia pesa iwe na thamani?
 
Masuala ya uchumi sio kama katiba eti unapendekeza au mswada hapana, inajibia na forces of economy, kama inflation rate, Export and Import balance, intensity of domestic trade, micro and macro economy, level of foreign investment etc........mapendekezo yako hayana mashiko in economic terms.
Mkuu nchi imejaaa wajinga, yaani ni hadi aibu, hii ni hatari sana mkuu,
 
Back
Top Bottom