Napendekeza simu zenye thamani ya zaidi ya milioni 1 zisajiliwe TRA na zipewe kadi kama za gari, hii itapunguza wizi wa simu

Napendekeza simu zenye thamani ya zaidi ya milioni 1 zisajiliwe TRA na zipewe kadi kama za gari, hii itapunguza wizi wa simu

FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2013
Posts
38,920
Reaction score
44,970
Kadi iwe na jina la mmiliki na taarifa zake zingine zote, na sehemu ya details ijazwe taarifa muhimu za simu kama IMEI, model, make, color na specification zingine zote. Pia pajazwe number of previous owners nk. nk.

Endapo simu itapotea au kuibiwa, by default, systems za TRA ziwe na built in permission kwenye system zao za kuitrack na kufuatilia exactly iko wapi (location), line ipi imewekwa, na hiyo laini inamilikiwa na nani kwa kutumia data base ya NIDA, TCRA na mitandao ya simu, na pawe na total synchronisation na database za polisi kitengo cha mtandaoni, endapo ni wizi, ili polisi waweze kuaccess na kumkamata mhalifu immediately, maana taarifazake zote za NIDA wanakuwa wametumiwa.

Mtu akinunua simu ya aina hiyo atakazimika kudai kadi original (kama ya gari) ili aende TRA kuibadilisha na alipe kodi stahiki, hata kama kidogo, angalau alipe.

Nimebaini kuna simu za mabilioni zinauzwa kwa njia za panya bila kulipiwa kodi hata senti tano, wanapitishia vichochoroni na kuziingiza nchini kirahisi, maana ni ndogo na zinafichika kirahisi, mtu anajidai anaenda China kununua nguo, kumbe ndani ya mabegi ya nguo kajaza Iphone 13 Plus na Pro Max za kutosha. Kwa mfumo huu, hakuna laini itasoma kama TRA hawaitambui hiyo IMEI, kodi italipwa tu safari hii.

Nawasilisha.
 
Napendekeza serikali itafute mbinu mbadala watu wapate ajira za kujiari na kuajiriwa ili tukidhi sote kununua simu za million moja tufanye na Mambo mengine ya maendeleo tuchangie uchumi wetu kukua.
 
kwani elimu ya TRA inasemaji kuhusu kodi ya vitu.

ingekuwa indeelevu kama unasema kufananisha labda magari,ndege,biashara,maduka na n.k hapo sawa.

lakini ukinunua ndio basi.sawa na kulazimisha kodi ya kichwa kwa mtindo wa kidigitali
 
Iphone huwa zinafika hadi milioni 4+, same case kwa Samsung Galaxy. Mtu anaeingiza TV ni ngumu kukwepa kodi, ila kakifaa chenye thamani ya millions kanachofichika kwenye begi la nguo ni rahisi kupitishwa kwa wingi mipakani, hivyo ukusanyaji kodi wake lazima uwe creative.
Tambua, ukiingiza iphone13 piece 3 tu, huna tofauti na aliyeagiza Toyota Crown (kabla ya kodi). Pia ifike mahala tudhibiti wizi wa kiholela holela.
 
Jiulize moja. Gari ikiibiwa, TRA wanahusikaje? Sio kazi ya TRA kusimamia simu kutoibiwa. Cha.msingi weka bima simu yako ili ikiibiwa au kupotea ulipwe.
 
mpaka kufikia bei hiyo kodi ni teyari imekatwa.

na makubaliano yapo dunia nzima mifumo ya kodi.

maana simu sio kitu kinachoendelea kama gari litapita barabarani na barabara itatikiwa kupata pesa kwa ajili ya matengenezo
 
Jiulize moja. Gari ikiibiwa, TRA wanahusikaje? Sio kazi ya TRA kusimamia simu kutoibiwa. Cha.msingi weka bima simu yako ili ikiibiwa au kupotea ulipwe.
Leo nikija kuchukua gari yako, una ushahidi gani kama ni yako? Wewe unasema yako na mimi nasema ni yangu, una kidhibitisho gani?
 
mpaka kufikia bei hiyo kodi ni teyari imekatwa.

na makubaliano yapo dunia nzima mifumo ya kodi.

maana simu sio kitu kinachoendelea kama gari litapita barabarani na barabara itatikiwa kupata pesa kwa ajili ya matengenezo
Mimi nikikuuzia simu kwa milioni 4+ wakati nimeiingiza nchini kwa njia za panya, hiyo kodi anachukua nani, mimi au serikali?
 
Mimi nikikuuzia simu kwa milioni 4+ wakati nimeiingiza nchini kwa njia za panya, hiyo kodi anachukua nani, mimi au serikali?

kuna vitu vingi vinaingia na kushindwa kulipiwa kodi.

kwa mfano hiyo simu ukichambua mfano 12 pro max.

ukisambaratisha kila kitu alafu vyote vije uvi assemble vikifika hapa.

mfano mzuri wachina wanafanya hii tabia kuanzia simu na pikipik
 
Yaani TCRA wahangaike na simu ya milioni moja, kweli vyuma vimekaza....
 
Lakini mwisho wa siku hiyo pikipiki lazima iwe na kadi, hata ukiitengneza kwa udongo au kwa miti, bado TRA hawakupi kadi bila kulipia kodi, simple as that.

Na hata hiyo simu ukichambua, lazima patakuwa na mashine yenye specific IMEI, na hakuna laini itafanya kazi kama hiyo IMEI haitambuliki TRA, as simple as that.
 
Yaani TCRA wahangaike na simu ya milioni moja, kweli vyuma vimekaza....
Milioni moja mara milioni ngapi? Kwani Tz kuna simu ngapi za Calliber hiyo, na kila baada ya miaka kadhaa watu wana-upgrade matoleo yao. Wameweza shs. 1,000/= kodi ya jengo, washindwe hili?
 
Lakini mwisho wa siku hiyo pikipiki lazima iwe na kadi, hata ukiitengneza kwa udongo au kwa miti, bado TRA hawakupi kadi bila kulipia kodi, simple as that.

uki assamble hapakuna unafuu unapingua kuliko kuleta nzima
 
Milioni mara milioni ngapi? Kwani Tz kuna simu ngapi za Calliber hiyo, na kila baada ya miaka kadhaa watu wana-upgrade matoleo yao. Wameweza shs. 1,000/= kodi ya jengo, washindwe hili?
Kwa hiyo wakulindie simu yako ya milioni moja isiibiwe, kwa nini usiikatie bima kama unaona ina thamani kubwa.....
 
uki assamble hapakuna unafuu unapingua kuliko kuleta nzima
Hata ukiassemble, lazima utafunga na mashine yake ambayo ndio ina IMEI, na haitafanya kazi unless iwe imetambulika na TRA ndio TCRA wairuhusu kufanya kazi, sasa una-assemble simu halafu haifanyi kazi, labda kama ni urembo.
 
Back
Top Bottom