Napendekeza taa za mwanga barabarani na nyaya za simu zifungwe kwenye nguzo za umeme

Yaani badala ya kununua milingoti ya chuma na wire kwa ajili ya kufunga zile taa za mwanga barabarani, napendekeza taa ziwe zinafungwa kwenye mistimu ya umeme iliyopo kando kando ya barabara na ziungwe kwenye umeme moja kwa moja, hii itakoa fedha nyingi mno.

Pia badala ya kusimika mistimu ya nyaya za simu napendekeza hizo nyaya za simu zifunge tu kwenye mistimu ya umeme ambayo ipo tayari hivyo kuokoa gharama kubwa sana katika usambazaji wa mawasiliano.

Mamlaka husika ziwasiliani na Tanesco ambao ndio wamiliki wa nguzo hizo ili kuona utekelezaji wake.
View attachment 1280265
Wazo zuri lakini halitekelezeki
 
Unadhani nguo za umeme zimeongozana kama siafu? Unajua umbali wa kutoka nguzo moja hadi nyingine?

Unataka ili mradi ionekane kuna taa za barabarani au unataka kuona nini wewe?
Umbali wa taa za barabarani na umbali wa nguzo za Tanesco ni sawa.
 
Wakati wengine wakifikiria kusafirisha umeme bila nguzo bali kwa induction tu au kuzika nyaya chini, sisi tunafikiria kuunganisha nyaya zote kwenye nguzo moja, sasa daraja litakua na nguzo ngapi?
 
Vipi kwa kipindi hiki ambapo bado hatujapata uwezo wa kusimika waya chini ya ardhi, je tukitumia nguzo zilizopo kubeba taa za barabarani ili kuokoa fedha, kuna shida gani?
 
Umbali wa taa za barabarani na umbali wa nguzo za Tanesco ni sawa.
Sijui kama unafahamu unachouliza. Taa za barabarani zimeweka mpangilio na zinakuwa karibu tofauti na nguzo za umeme ambazo nazo husimikwa kwa umbali ambao si sawa na ule wa taa za barabarani.

Tuseme nguzo ya umeme hufuatana kwa umbali wa mita 60. Ina maana tutakuwa tuna taa ambazo lazima zifuate uwepo wa nguzo na hii itafanya ukosefu wa mwanga wa kutosha.

Walioamua kuweka nguzo za umeme na nguzo za taa za barabarani sio wajinga. Na kwa uhakika nikwambie tu kuwa HAITAKUJA KUWEZEKANA NGUZO ZA UMEME ZIFUNGWE TAA ZA BARABARANI.

KAMA ILISHINDIKANA ENZI HIZO HAIWEZEKANI ENZI HIZI NA HAITAKUJA KUWEZEKANA. (SAHAU NA ONDOKA KICHWANI)
 
Vipi kwa kipindi hiki ambapo bado hatujapata uwezo wa kusimika waya chini ya ardhi, je tukitumia nguzo zilizopo kubeba taa za barabarani ili kuokoa fedha, kuna shida gani?
Unakoa fedha ili iweje wakati gharama za barabara huwa zinajumuisha hadi uwepo wa taa za barabarani. Tanesco wakitaka kufanya marekebisho kwenye nguzo zao tukose taa za barabarani kisa kubana matumizi na kuokoa pesa.

Nani kakwambia pesa inaokolewa kwenye miundombinu ya lazima hii.
 
Sijui kama unafahamu unachouliza. Taa za barabarani zimeweka mpangilio na zinakuwa karibu tofauti na nguzo za umeme ambazo nazo husimikwa kwa umbali ambao si sawa na ule wa taa za barabarani.

Tuseme nguzo ya umeme hufuatana kwa umbali wa mita 60. Ina maana tutakuwa tuna taa ambazo lazima zifuate uwepo wa nguzo na hii itafanya ukosefu wa mwanga wa kutosha.

Walioamua kuweka nguzo za umeme na nguzo za taa za barabarani sio wajinga. Na kwa uhakika nikwambie tu kuwa HAITAKUJA KUWEZEKANA NGUZO ZA UMEME ZIFUNGWE TAA ZA BARABARANI.

KAMA ILISHINDIKANA ENZI HIZO HAIWEZEKANI ENZI HIZI NA HAITAKUJA KUWEZEKANA. (SAHAU NA ONDOKA KICHWANI)
Sikuuliza bali nimekujulisha tu kwamba, umbali wa taa za barabarani na umbali wa nguzo za umeme ni sawa, na endapo kunatofauti kidogo, basi inafidiwa kwa kuadjust ukubwa na power ya taa husika (Size and watts).
 
Unakoa fedha ili iweje wakati gharama za barabara huwa zinajumuisha hadi uwepo wa taa za barabarani. Tanesco wakitaka kufanya marekebisho kwenye nguzo zao tukose taa za barabarani kisa kubana matumizi na kuokoa pesa.

Nani kakwambia pesa inaokolewa kwenye miundombinu ya lazima hii.
Kama huwa inajumuishwa kwenye bajeti ya barabara, mbona kuna barabara nyingi mitaani hazina taa? Na kwa zile ambazo zinataa, huoni gharama za mradi zingepungua kwa kutumia nguzo za umeme na hivyo pesa zilizookolewa zingeenda kutumika kununua madawa hospitalini?, marekebisho ya Tanesco hata yangefanywa bila hizo taa kuwa juu ya nguzo za Tanesco si bado zisingewaka kwa kukosa umeme? Unless kama ni solar, but in any case marekebisho hayatokei muda wote, na taa si hewa kwamba wakikata kwa nusu saa tukakosa mwanga barabarani tutakufa, you are being ridiculous.
 
Siyo kila barabara ina bajeti ya taa za barabarani.

Na ndiyo maana kuna utofauti wa gharama za matengenezo.
 
Naam, kwa hizo ambazo hazikujengwa na taa kutokana ufinyu wa bajeti, ndio napendekezwa zifanyiwe maboresho ya gharama nafuu kwa kuwekewa taa kwa kutumia miundo mbinu ya nguzo za umeme ambayo ipo tayari
 
Bagamoyo Rd. (Morocco-Mwenge) Usiku ni machinjioni.
 
Kwanza Tanzania inatia aibu sana katika swala la taa za barabarani,, miji mingi usiku ni giza, achilia mbali barabara za mitaani hata kubwa za mjini kati hazina taa,
 
Kuhusu taa kufungwa kwenye nyaya za umeme sina pingamizi lakini nyaya za simu kidogo kuna shida kidogo.
Hujasema nguzo za umeme za msongo mkubwa(high tension) au msongo mdogo.
Kuna kanuni inaitwa kanuni ya kiganja cha kulia cha mkono ya Jean Ampere'.(Ampere's hand right rule).Kanuni inasema ukikamata waya wa umeme(grip) welekeo wa dole gumba ni welekeo wa umeme na welekeo wa vidole vingine vilivyobaki ni welekeo wa mawimbi sumaku(electromagnetic fields) kwa welekeo wa kinyume saa(anticlockwise).
Waya wowote unaopitisha umeme kando kando yake kuna mawimbi sumaku.Yanakuwa na nguvu kubwa kama umeme ni wa msongo mkubwa.
Ndio maana chunguza panapokuwa na umeme wa msongo mkubwa sana kunakuwa na eneo kubwa chini yake hairuhusiwi kujenga.
Kumbuka waya wa umeme ulio wazi hasa msongo mkubwa unapokuwa na nia ya kuugusa kiukweli kuna umbali kabla hujaugusa unakuvuta wenyewe shauri ya haya mawimbi sumaku.
Tuje kwenye mada nyaya za simu kumbuka sio tu zinapitisha mawimbi umeme ya maongezi zinapitisha mawimbi mengine mfano channel za TV,Fax,computer,wakati mwingine maongezi ya radio,fiber optics n.k.
Hivyo kuchanganya hizi nyaya na za umeme kuna uwezekano mkubwa wa muingiliano(interference) wa mawimbi sumaku na kuleta sintofahamu kubwa kimawasiliano.
 
kanuni ya Andre Ampere kama picha chini hiyo miviringo miyekundu ni mawimbi sumaku.Uelekeo wa dole gumba ni umeme unakokwenda
Screenshot_2019-12-03-14-42-24-1.jpeg
 
Kuhusu taa kufungwa kwenye nyaya za umeme sina pingamizi lakini nyaya za simu kidogo kuna shida kidogo.
Hujasema nguzo za umeme za msongo mkubwa(high tension) au msongo mdogo.
Kuna kanuni inaitwa kanuni ya kiganja cha kulia cha mkono ya Jean Ampere'.(Ampere's hand right rule).Kanuni inasema ukikamata waya wa umeme(grip) welekeo wa dole gumba ni welekeo wa umeme na welekeo wa vidole vingine vilivyobaki ni welekeo wa mawimbi sumaku(electromagnetic fields) kwa welekeo wa kinyume saa(anticlockwise).
Waya wowote unaopitisha umeme kando kando yake kuna mawimbi sumaku.Yanakuwa na nguvu kubwa kama umeme ni wa msongo mkubwa.
Ndio maana chunguza panapokuwa na umeme wa msongo mkubwa sana kunakuwa na eneo kubwa chini yake hairuhusiwi kujenga.
Kumbuka waya wa umeme ulio wazi hasa msongo mkubwa unapokuwa na nia ya kuugusa kiukweli kuna umbali kabla hujaugusa unakuvuta wenyewe shauri ya haya mawimbi sumaku.
Tuje kwenye mada nyaya za simu kumbuka sio tu zinapitisha mawimbi umeme ya maongezi zinapitisha mawimbi mengine mfano channel za TV,Fax,computer,wakati mwingine maongezi ya radio,fiber optics n.k.
Hivyo kuchanganya hizi nyaya na za umeme kuna uwezekano mkubwa wa muingiliano(interference) wa mawimbi sumaku na kuleta sintofahamu kubwa kimawasiliano.
Yeah, ila nyaya nyingi za simu ziko within a less than a meter kutoka nyaya za umeme, hasa kariakoo, na hakuna notable effect, labda kwa msongo mkubwa
 
Don nimependa uzi wako una chachu ya kujifunza.Less than a metre no problem sababu kwa msongo mdogo huu wa 240v hizo electromagnetic waves ni so weak ila kwa 10,000-200,000V au zaidi ni habari ingine.
Na ndio maana nguzo ndefu zile za machuma kutoka mkoa hadi mkoa huwezi kuta zinafungwa na vitu vingine kwanza hata ukipita chini unasikia umeme ukitiririka
 
Back
Top Bottom