Konseli Mkuu Andrew
JF-Expert Member
- May 10, 2013
- 749
- 875
Serikali kupitia wizara husika inapasa kufanya mabadiliko kidogo katika sheria ya uhalifu wa kimtandao ya mwaka 2015 yaani Cyber Crimes Act , 2015 kwani tangu ilipoanzishwa na kupitishwa na Bunge tarehe 22 .05.2015 polisi ndio wamepewa mamlaka ya kufuatilia uhalifu na uchunguzi juu ya masuala ya kimtandao, hali inayopelekea kuwepo na ulasimu sana hasa linapokuja suala la upelelezi.
Napendekeza pawepo na usajili wa taasisi binafsi zitakazo saidia kufanya uchunguzi kwa baadhi ya mambo ambayo yanaigusa jamaa kila siku, mfano sualla la uwizi wa simu jeshi la polisi limekuwa likichukua muda sana hadi kunamwezesha mwizi wa simu ku-bypass simu husika au kuchange imei box na kupelekea kutoonekana tena hiyo simu.
Unaweza hata peleka taarifa ya simu yako unayotumia ukawaambia imepotea na bila kuchezesha unaweza ambiwa bado mwizi hajaiwasha hivyo uwe na subira itapatikana ili hali unayo mkononi.
Mwisho japo sio kwa umuhimu, kuruhusu taasisi binafsi kufanya uchunguzi au upelelezi kutasaidia kuwaishwa kwa kufanyika maamuzi juu ya kesi zinahusiana na uhalifu wa kimtandao.