Napinga Dkt. Harrison Mwakyembe kuwa Mwenyekiti wa Tume ya kuchunguza kufeli kwa wanafunzi wengi wa Law School

Tume imejaa watumishi wa taasisi za serikali ambao wanawajibika kwa serikali ambayo inaimiliki pia taasisi ya LST chini ya Wizara ya Sheria. Kwa kweli, tunampongeza waziri Ndumbaro kwa kuchukua hatua lakini tunaomba aongeze wajumbe kwenye hiyo tume, aweke wanasheria wa kujitegemea, wajumbe wa bodi nyingine za kitaaluma, waandishi wa habari, wanafunzi waliofeli, na hata mwanafunzi aliyepo darasani sasa.

Mkuu umeandika vyema. Tatizo ni kuwa hawa ndugu huwa hawasikii kwa kuwa rai tu. Haipo nia njema bado.

Composition ya tume haikubaliki:

Tume Kuchunguza kadhia ya Law School inapaswa kuwa huru
 
Mwenyekiti wa Tume ya Kuchunguza masuala ya Law school, ikiwemo wanafunzi wengi kufeli mitihani, anapaswa kuwa mtu Muungwana, Mtulivu, Msikivu na asiye na makuu, anapaswa kuwa mkweli, Mwakyembe hana sifa hizi.

Napinga uteuzi wa Harisson Mwakyembe kuwa Mwenyekiti wa Tume hii kwa vile Haaminiki, si mkweli na ni mpenda sifa.

Kwa mfano, alipokuwa Mwenyekiti wa Tume ya bunge kuchunguza Richmond, katika Taarifa yake aliyoisoma bungeni ALIFICHA BAADHI YA TAARIFA ILI KUOKOA SERIKALI, maana yake ni kwamba alificha taarifa za Mhusika Mkuu wa Jambo lile na kuangushia jumba bovu wasiohusika, leo huyu awezaje kuaminika na kukabidhiwa tume nyingine? JE, SAFARI HII HATOFICHA TAARIFA ILI KUIOKOA SERIKALI?

Mwakyembe akiwa mgombea Ubunge wa Jimbo la Kyela kupitia CCM, aliwaahidi watu wa Jimbo lake kwamba AMEPATA SOKO LA UHAKIKA LA MCHELE WAO NCHINI MAREKANI (ikumbukwe kwamba mchele wa Kyela ndio unaoongoza kwa utamu duniani)

Lakini hadi anang'olewa kwenye ubunge hakuwahi kusaidia hata kilo 10 za mchele wa Kyela kuuzwa Marekani, Mtu kama huyu hastahili kuaminiwa kuongoza tume yoyote ile.

UNAPODANGANYA NYUMBANI KWENU HUWEZI KUAMINIKA UGENINI.

Harrison Mwakyembe ni mtu aliyejaa dharau kubwa sana , huyu hawezi kuwatendea haki watu wenye digrii moja wanaopigania haki yao ya matokeo.

ALIWAHI KUKATAA MASWALI KWAO KYELA kwa kisingizio kwamba wanaomhoji ni Darasa la 7, wakati yeye anamiliki digrii 4 na kwamba watu wasio na elimu wanachopaswa kumhoji ni kuhusu kama hawana hela mifukoni mwao na labda awasaidie. Huyu hafai kuongoza Tume ya kufuatilia haki popote duniani.

Tunamuomba Waziri wa Sheria ATENGUE HARAKA UTEUZI WAKE.

NITASEMA KWELI DAIMA FITNA KWANGU MWIKO.
Hakuna mwana CCM msafi, muadilifu na mkweli.
 
Matokeo ya Law School yako sawa mengine ni mihemuko tu!
Wanafunzi wengi ni weupe mno vichwani na wanakariri vitu vya kujibia mitihani tu basi!
Kwanza hata huku mitaani kuna mawakili huwezi hata amini kama wamepita Law School,ni " weupe" mno vichwani na hawasomi !
Kazi zao ni copy, paste na edit basi!
Kiingereza ndo wengi hawajui kabisa!
Msimchoshe Dr.Mwakyembe na kamati zisizo na misingi!
Chukueni Wanafunzi 30 ( randomly) then wapigwe oral interview ( Live on TV) mtaona Tanzania ilivyo na majanga mengi na sote tutaishia kuwapongeza hao Lecturers wa Law School wasiotaka ujinga ujinga katika fani ya Sheria.
hiyo first degree waliipataje?kama ndo hivyo basi tuchunguze na hivyo ndaki za vyuo vikuu vinavyotoa hizo degree.kingereza kwangu si ajenda kwani kuna nchi nyingi duniani haziongei hiyo lugha hasa ukizingatia karne hii yenye utandawazi mkubwa.mtu yeyote anayetaka kujifunza hiyo lugha ataijua tu kama akina diamond,harmonize na wasanii wengine wanaongea lugha hiyo walisoma wapi?ndo maana kuna mjadala wa vyuo vikuu kufundisha kwa lugha ya kiswahili.hii itawasaidia wengi kumudu masomo yao.hata nyie mnaotetea hiyo lugha ni sababu tu wazazi wenu walipata fursa serikalini wakakwapua mali za walalahoi na kuwapeleka shule za kiingereza vinginevyo na nyie hamngekuwa fluent ktk lugha hiyo.
 
Nchi yetu nzuri sana. Kama ukiwa upinzani hata kama sifa zako za kitaaluma ni za kubabaisha lazima utasifiwa sana

BAVICHA OYEEEE.
 
Ingekuwa mimi ndio waziri ngumbaru, ningechukua mitihani ya wanafunzi waliofeli ikasahihishwe upya kwenye mamlaka yenye uwezo kama chuo cha sheria katika nchi nyingine za jumuiya ya madola.
Wakina Mwakyembe hawatakuja na kitu cha maana zaidi ya porojo tu!
 
Mwenyekiti wa Tume ya Kuchunguza masuala ya Law school, ikiwemo wanafunzi wengi kufeli mitihani, anapaswa kuwa mtu Muungwana, Mtulivu, Msikivu na asiye na makuu, anapaswa kuwa mkweli, Mwakyembe hana sifa hizi.

Napinga uteuzi wa Harisson Mwakyembe kuwa Mwenyekiti wa Tume hii kwa vile Haaminiki, si mkweli na ni mpenda sifa.

Kwa mfano, alipokuwa Mwenyekiti wa Tume ya bunge kuchunguza Richmond, katika Taarifa yake aliyoisoma bungeni ALIFICHA BAADHI YA TAARIFA ILI KUOKOA SERIKALI, maana yake ni kwamba alificha taarifa za Mhusika Mkuu wa Jambo lile na kuangushia jumba bovu wasiohusika, leo huyu awezaje kuaminika na kukabidhiwa tume nyingine? JE, SAFARI HII HATOFICHA TAARIFA ILI KUIOKOA SERIKALI?

Mwakyembe akiwa mgombea Ubunge wa Jimbo la Kyela kupitia CCM, aliwaahidi watu wa Jimbo lake kwamba AMEPATA SOKO LA UHAKIKA LA MCHELE WAO NCHINI MAREKANI (ikumbukwe kwamba mchele wa Kyela ndio unaoongoza kwa utamu duniani)

Lakini hadi anang'olewa kwenye ubunge hakuwahi kusaidia hata kilo 10 za mchele wa Kyela kuuzwa Marekani, Mtu kama huyu hastahili kuaminiwa kuongoza tume yoyote ile.

UNAPODANGANYA NYUMBANI KWENU HUWEZI KUAMINIKA UGENINI.

Harrison Mwakyembe ni mtu aliyejaa dharau kubwa sana , huyu hawezi kuwatendea haki watu wenye digrii moja wanaopigania haki yao ya matokeo.

ALIWAHI KUKATAA MASWALI KWAO KYELA kwa kisingizio kwamba wanaomhoji ni Darasa la 7, wakati yeye anamiliki digrii 4 na kwamba watu wasio na elimu wanachopaswa kumhoji ni kuhusu kama hawana hela mifukoni mwao na labda awasaidie. Huyu hafai kuongoza Tume ya kufuatilia haki popote duniani.

Tunamuomba Waziri wa Sheria ATENGUE HARAKA UTEUZI WAKE.

NITASEMA KWELI DAIMA FITNA KWANGU MWIKO.
sema baba sema usiogope
 
Ingekuwa mimi ndio waziri ngumbaru, ningechukua mitihani ya wanafunzi waliofeli ikasahihishwe upya kwenye mamlaka yenye uwezo kama chuo cha sheria katika nchi nyingine za jumuiya ya madola.
Wakina Mwakyembe hawatakuja na kitu cha maana zaidi ya porojo tu!
mwakyembe na ndumbaro wanatokea UDSM. huyu Ndumbaro mpaka anaondoka pale PSPA alikuwa ameshawafelisha wengi? fikiria DR anafundisha organization Behavior darasa la watu 100 anayefaulu sana anapata B +
 
Duuuuh !! halafu aliwahi pia kupigwa marufuku kujihusisha na soka ndani na nje kutokana na makandokando
 
mtu kasoma KIU katoka na first class anataka na Law school atoke na first class
Kwenye diploma hamna kitu kinaitwa 'first class'

First class inatumika kwenye degree tu.

Law School hawatoi degree bali ni Post Graduate Diploma in Legal Practice, PGDL, na Certificate.

Naona mjadala umejaa kenge!
 
Back
Top Bottom