Mkuu, mimi ni mmoja wa wanafunzi wa LST waliofeli na kuona tunaonewa. Mahakamani unapomtuhumu Jaji kuwa na upendeleo, wanasema hata kama hakuna upendeleo, ni vyema jaji kujitoa katika kesi hiyo ili haki itendeke maana cha muhimu sio kile anachokiona Jaji bali ni zile fikra alizonazo mlalamikaji/mlalamikiwa kuwa jaji ana upendeleo, hizo ndio zinazopaswa kufutwa kichwani mwake kwa Jaji mtuhumiwa kujitoa. Sasa ukija LST, wanafunzi hawakuanza kulalamika kuwa wanaonewa, walianza kwanza kutaka kuhakikisha maksi zao, waone usahishaji na namna walivyojibu, LST wakakataa kutoa booklet, hapo ikaja imani kuwa wanafunzi wanaonewa, dhana yao ikawa imejibiwa kwa matendo ya LST. Dhana yao kufutwa, ni kwa LST kutoa booklet na sio kusema kuwa wana maandalizi duni. Kwa hiyo conclusion yangu inakuja kupitia matendo ya LST, na hapo hakuna kesi inayoungua kuwa nimesema kwa hisia tu, hapana, matendo ya LST yanajionesha, wanazuia kwa kila hali, watu wasione booklet ilhali sheria yao wenyewe inaruhusu jambo hilo. Hapa ndipo Barunguza alipoenda mahakamani, kuomba iwaamuru watoe booklet (sio kuwa wamfaulishe) ili aone mtihani wake ulivyosahishwa na kutolewa maksi
Sasa Chifu lengo la kuanzisha hiyo tume si ndo hicho unachosema?!
Wewe kama Mwanasheria unatakiwa kujikita kwenye hoja zilizotolewa na
Erythrocyte.
Look at him... pamoja na u-CHADEMA wake ulio wazi, bado thread yake imeegemea kwenye kutokuwa na imani na Mwenyekiti wa Tume husika, and I agree with him.
Na kama nilivyosema hapo kabla, Mwakyembe sio tu hana sifa za kuongoza hiyo tume, hana sifa hata za kuwa mjumbe!!
Sauti yenu itakuwa na nguvu zaidi mkisimama kwenye hoja ya kuwa na tume huru kuliko kujikita kwenye kuonewa coz', none of you, can prove kwamba mmeonewa!
Law sio exact mathematical science kwahiyo hata ukipewa paper yako bado huwezi ku-prove beyond reasonable doubt kwamba umeonewa!
Lakini mkipigania Tume Huru, kwa maana ya HURU kweli kweli... ikibidi ihusishe hata Students Leadership, hapo ndipo inaweza kupatikana suluhu!!
LST wameconclude kuwa wanafunzi wanakuja LST wakiwa na elimu duni toka vyuo walivyojifunzia LLB, vigezo walivyotumia LST kupata hiyo conclusion vipo vichwani mwao wenyewe.
Hii ndo ile mada ambayo nilikuambia hapo kabla kwamba, please, don't let me go upande huo!
Anyway, let's assume waliofeli ni wanafunzi 100, na kati ya hao 75 wanatoka kwenye aina fulani ya vyuo, huku waliotoka kwenye aina nyingine ya vyuo, majority wamefaulu!!
Hapo utasema conclusion ya LST ni ya kichwani?!
Kui-counter attack hoja hiyo ya LST ulitakiwa kutupatia percentage ya waliofeli kutoka kila chuo au at least percentage ya waliofeli na kufaulu kupitia makundi mbalimbali ya vyuo...
Kama average is almost the same kwa kila chuo au makundi ya vyuo basi hoja hiyo ya LST itakuwa ni ujinga mtupu!!
Hata hivyo, kama ni aina fulani tu ya vyuo ndio imetowa waliofeli wengi, hapo HUWEZI kuipinga hoja ya LST unless ama uthibitishwe kwamba nyote mmeonewa au wale wa vyuo vingine wamependelewa!!