Napinga Dkt. Harrison Mwakyembe kuwa Mwenyekiti wa Tume ya kuchunguza kufeli kwa wanafunzi wengi wa Law School

Napinga Dkt. Harrison Mwakyembe kuwa Mwenyekiti wa Tume ya kuchunguza kufeli kwa wanafunzi wengi wa Law School

Hoja za kisheria ndio kama hizo, mitihani ya LST inatoka bila mwanafunzi kufundishwa?? Kama jibu ni ndiyo iweje ashindwe kukariri ilhali aliweza kwenye LLB?
Kwani wale wanaofeli Form VI hawakufaulu Kidato cha IV?!

Wale wanao-disco vyuoni, hawakufaulu Kidato cha VI?

I bet utazungumzia suala la mass failure lakini hata huko kwingine inatokea miaka kunakuwa na mass failure!

Man, kwenye mada hii najitahidi sana kuto-undermine baadhi ya vyuo vyetu... please, don't make me go there but deep inside your heart, I know you know what I mean.
Hoja nyingine, je, booklet zinaruhusiwa kuhakikiwa au la? Kama jibu ni Ndiyo, je LST wanatekeleza takwa hilo? Wanawapa wanafunzi booklet wazihakiki?
Sasa kwanini una-conclude kwamba kuna uonevu wakati wala huna uhakika kama zinahakikiwa au hapana, na kwa maana hiyo kumbe wala hujaona ikiwa hao wanaosema wameonewa ni kweli wameonewa au hapana?

Yaani tungekuwa mahakamani, hapo tayari umeshaunguza kesi ya mteja wako!!
Hoja ya tatu, unaweza kukata rufaa kwa kusema maksi zako hazijajumlishwa au kusema mtihani wako umesahishwa vibaya ilhali hujaona booklet? Hauoni ni kama utakuwa unaagua kiganga?
Ulitakiwa kuwa na hayo majibu kabla ya ku-conclude kwamba wameonewa; na ndo maana mara zote nimejizuia kusema ikiwa haki imetendeka au hapana kwa sababu sina majibu ya hayo maswali!!
Hizi zinapaswa kuwa HADIDU ZA REJEA kwa hiyo Kamati HURU ya uchunguzi
Nakubaliana na wewe, na kama hawatafanya hivyo, basi sioni sababu ya kuwepo kwa hiyo kamati!!
 
Sasa kwanini una-conclude kwamba kuna uonevu wakati wala huna uhakika kama zinahakikiwa au hapana, na kwa maana hiyo kumbe wala hujaona ikiwa hao wanaosema wameonewa ni kweli wameonewa au hapana?

Yaani tungekuwa mahakamani, hapo tayari umeshaunguza kesi ya mteja wako!!
Mkuu, mimi ni mmoja wa wanafunzi wa LST waliofeli na kuona tunaonewa. Mahakamani unapomtuhumu Jaji kuwa na upendeleo, wanasema hata kama hakuna upendeleo, ni vyema jaji kujitoa katika kesi hiyo ili haki itendeke maana cha muhimu sio kile anachokiona Jaji bali ni zile fikra alizonazo mlalamikaji/mlalamikiwa kuwa jaji ana upendeleo, hizo ndio zinazopaswa kufutwa kichwani mwake kwa Jaji mtuhumiwa kujitoa. Sasa ukija LST, wanafunzi hawakuanza kulalamika kuwa wanaonewa, walianza kwanza kutaka kuhakikisha maksi zao, waone usahishaji na namna walivyojibu, LST wakakataa kutoa booklet, hapo ikaja imani kuwa wanafunzi wanaonewa, dhana yao ikawa imejibiwa kwa matendo ya LST. Dhana yao kufutwa, ni kwa LST kutoa booklet na sio kusema kuwa wana maandalizi duni. Kwa hiyo conclusion yangu inakuja kupitia matendo ya LST, na hapo hakuna kesi inayoungua kuwa nimesema kwa hisia tu, hapana, matendo ya LST yanajionesha, wanazuia kwa kila hali, watu wasione booklet ilhali sheria yao wenyewe inaruhusu jambo hilo. Hapa ndipo Barunguza alipoenda mahakamani, kuomba iwaamuru watoe booklet (sio kuwa wamfaulishe) ili aone mtihani wake ulivyosahishwa na kutolewa maksi

Ulitakiwa kuwa na hayo majibu kabla ya ku-conclude kwamba wameonewa; na ndo maana mara zote nimejizuia kusema ikiwa haki imetendeka au hapana kwa sababu sina majibu ya hayo maswali!
LST wameconclude kuwa wanafunzi wanakuja LST wakiwa na elimu duni toka vyuo walivyojifunzia LLB, vigezo walivyotumia LST kupata hiyo conclusion vipo vichwani mwao wenyewe. TCU hawajalala kuwa washindwe kuvifungia vyuo vinavyotoa elimu duni, walimu wa vyuo hivyo wamekataa pia kubebeshwa zigo maana hata wao wanafeli, sasa nani wa kusikilizwa kwa hoja, mwanafunzi ambaye anataka sheria itekelezwe na kuwa ukataaji wa kutekeleza sheria ndio unahitimisha kuwa kuna uonezi AU LST wanaosema wanafunzi wanakuja na elimu duni pasipo kuonesha msingi waliotumia kufika hoja hiyo?
 
Kwani wale wanaofeli Form VI hawakufaulu Kidato cha IV?!

Wale wanao-disco vyuoni, hawakufaulu Kidato cha VI?

I bet utazungumzia suala la mass failure lakini hata huko kwingine inatokea miaka kunakuwa na mass failure!
Hapo ndipo tunapokuja kwenye ile hoja yako ya mahakamani, kuwa ni legal battle. Upande mmoja akiwa Tundu Lissu na upande mwingine Kibatala, bado lazima mshindi atakuwa mmoja tu. Kushindwa kwake haitamaanisha kuwa aliyeshindwa hana akili. Kumbuka hao wote wawili ni mawakili wabobevu.

Sasa hii ni hoja ya LST kuwa wanafunzi ni duni kisheria, nawe ukaongeza kuwa law sio ya kila mtu. Ndipo nikakujibu kuwa kama LLB wamekariri, ni vipi washindwe kukariri na kutumia hizo reference LST?
 
Hayo mambo ya kwamba wameonewa au hapana, narudia... siwezi kuyaongelea, lakini kwavile wewe unaamini wameonewa; je unaweza kutuambia unatumia vigezo gani ku-conclude kwamba wameonewa?
Matendo ya LST.

Rufaa ya mitihani ya LST inaongozwa na sheria ndogo ziitwazo The Law School of Tanzania (Students' Performance, Assesment and Awards) By-Laws 2011 GN. No. 172 of 2011, cha kushangaza ni kuwa sheria hii haipatikani katika tovuti yoyote ya serikali na hata kwenye tovuti ya LST wenyewe haipo. Mawazo yetu ni kuwa hawataki wanafunzi wengi waijue kwa kuwa 'itawalazimu' LST kufanya usahishaji wa haki maana kinyume cha hapo, watu wataomba kuona booklet zao na kukagua usahishaji.

Matendo ya LST kuonesha nia mbaya yao,

Kwenye aya ya 8 ya kiapo kinzani alichofanya Belinda Molel ambae ni Principal Legal Officer wa LST aliyepewa maelekezo na uongozi wa LST, anasema kuwa Sheria ndogo hiyo inapatikana katika tovuti ya chuo. Wewe hapo una intaneti, hebu ingia THE LAW SCHOOL OF TANZANIA utafute hiyo sheria uone kama inapatikana, maana utafutaji wa sheria haujitaji utaalamu wa IT.
Sehemu ya kiapo kinzani cha LST wakizungumza uongo mahakamani ni hii hapa, soma aya ya 8.
 
Attachments

  • Screenshot_2022-10-16-10-05-39-673_com.google.android.apps.docs.jpg
    Screenshot_2022-10-16-10-05-39-673_com.google.android.apps.docs.jpg
    132.1 KB · Views: 7
Mkuu, mimi ni mmoja wa wanafunzi wa LST waliofeli na kuona tunaonewa. Mahakamani unapomtuhumu Jaji kuwa na upendeleo, wanasema hata kama hakuna upendeleo, ni vyema jaji kujitoa katika kesi hiyo ili haki itendeke maana cha muhimu sio kile anachokiona Jaji bali ni zile fikra alizonazo mlalamikaji/mlalamikiwa kuwa jaji ana upendeleo, hizo ndio zinazopaswa kufutwa kichwani mwake kwa Jaji mtuhumiwa kujitoa. Sasa ukija LST, wanafunzi hawakuanza kulalamika kuwa wanaonewa, walianza kwanza kutaka kuhakikisha maksi zao, waone usahishaji na namna walivyojibu, LST wakakataa kutoa booklet, hapo ikaja imani kuwa wanafunzi wanaonewa, dhana yao ikawa imejibiwa kwa matendo ya LST. Dhana yao kufutwa, ni kwa LST kutoa booklet na sio kusema kuwa wana maandalizi duni. Kwa hiyo conclusion yangu inakuja kupitia matendo ya LST, na hapo hakuna kesi inayoungua kuwa nimesema kwa hisia tu, hapana, matendo ya LST yanajionesha, wanazuia kwa kila hali, watu wasione booklet ilhali sheria yao wenyewe inaruhusu jambo hilo. Hapa ndipo Barunguza alipoenda mahakamani, kuomba iwaamuru watoe booklet (sio kuwa wamfaulishe) ili aone mtihani wake ulivyosahishwa na kutolewa maksi
Sasa Chifu lengo la kuanzisha hiyo tume si ndo hicho unachosema?!

Wewe kama Mwanasheria unatakiwa kujikita kwenye hoja zilizotolewa na Erythrocyte.

Look at him... pamoja na u-CHADEMA wake ulio wazi, bado thread yake imeegemea kwenye kutokuwa na imani na Mwenyekiti wa Tume husika, and I agree with him.

Na kama nilivyosema hapo kabla, Mwakyembe sio tu hana sifa za kuongoza hiyo tume, hana sifa hata za kuwa mjumbe!!

Sauti yenu itakuwa na nguvu zaidi mkisimama kwenye hoja ya kuwa na tume huru kuliko kujikita kwenye kuonewa coz', none of you, can prove kwamba mmeonewa!

Law sio exact mathematical science kwahiyo hata ukipewa paper yako bado huwezi ku-prove beyond reasonable doubt kwamba umeonewa!

Lakini mkipigania Tume Huru, kwa maana ya HURU kweli kweli... ikibidi ihusishe hata Students Leadership, hapo ndipo inaweza kupatikana suluhu!!
LST wameconclude kuwa wanafunzi wanakuja LST wakiwa na elimu duni toka vyuo walivyojifunzia LLB, vigezo walivyotumia LST kupata hiyo conclusion vipo vichwani mwao wenyewe.
Hii ndo ile mada ambayo nilikuambia hapo kabla kwamba, please, don't let me go upande huo!

Anyway, let's assume waliofeli ni wanafunzi 100, na kati ya hao 75 wanatoka kwenye aina fulani ya vyuo, huku waliotoka kwenye aina nyingine ya vyuo, majority wamefaulu!!

Hapo utasema conclusion ya LST ni ya kichwani?!

Kui-counter attack hoja hiyo ya LST ulitakiwa kutupatia percentage ya waliofeli kutoka kila chuo au at least percentage ya waliofeli na kufaulu kupitia makundi mbalimbali ya vyuo...

Kama average is almost the same kwa kila chuo au makundi ya vyuo basi hoja hiyo ya LST itakuwa ni ujinga mtupu!!

Hata hivyo, kama ni aina fulani tu ya vyuo ndio imetowa waliofeli wengi, hapo HUWEZI kuipinga hoja ya LST unless ama uthibitishwe kwamba nyote mmeonewa au wale wa vyuo vingine wamependelewa!!
 
Sasa Chifu lengo la kuanzisha hiyo tume si ndo hicho unachosema?!

Wewe kama Mwanasheria unatakiwa kujikita kwenye hoja zilizotolewa na Erythrocyte.
Ni sawa kabisa, kamati imeanzishwa kwa lengo la kuchunguza malalamiko.

Na kama nilivyosema hapo kabla, Mwakyembe sio tu hana sifa za kuongoza hiyo tume, hana sifa hata za kuwa mjumbe!!
Mkuu, ukisoma comment/post no. 98 katika thread hii utaona mchango wangu kuhusu mada, nimeunga mkono uharamu wa Mwakyembe kuwa hata mjumbe katika kamati hii.

Kui-counter attack hoja hiyo ya LST ulitakiwa kutupatia percentage ya waliofeli kutoka kila chuo au at least percentage ya waliofeli na kufaulu kupitia makundi mbalimbali ya vyuo...
Mkuu, mimi sina access ya kutoa hizo takwimu kwa percentage kama ambavyo unahisi kuwa labda LST waliangalia ufaulu wa wanafunzi wakahusisha na vyuo na ndio wakafikia hitimisho. Tumebaki kuhisi hisi kwa kuwa LST hawajatoa base ya hitimisho walilofikia.

Kwa kuwa wewe ni mtu wa nje ya shule, basi unapaswa kujua kuwa hata hizo takwimu za wanafunzi wangapi wamefaulu na kufeli, huwa hazitoki kwa wakati. Yaani takwimu za matokeo haya, zingeweza kuwekwa wazi mwakani kupitia taarifa ya chuo, lakini kwenye matokeo mwanafunzi hawezi kuona, kuna usiri wa ajabu hata kuona tu matokeo ya jumla. Hizi takwimu za mwaka huu, ukiangalia hutapata taarifa popote pale ikiwa ni rasmi ya LST, utaona ni kama mtu alipiga picha juu ya skrini ya kompyuta na ndipo ikasambaa mpaka kwenye media. Hakuna Taarifa kwa Umma au kwa wanafunzi kuhusu matokeo na ufaulu wake. Katika mazingira hayo ni jambo gumu sana kutegemea counter yangu kwa LST iwe ni ya kitakwimu kama unavyosajesti, kwanza sina access lakini pia wao wametoa taarifa kwa ujumla.

Ila wao kama taasisi hawapaswi kushindana na wanafunzi kienyeji kama hivi ilivyo, walipaswa kuwa wawazi kwa kuzingatia sheria na kuonesha booklet. Wao hawaingii hasara kwa kuonesha booklet ila mwanafunzi anapata hasara ya hofu nk kwa kunyimwa booklet inayomfanya aamini ameonewa.
 
Kwahiyo bora umfichie siri boss wako aliye na hatia kumsingizia asiye boss wako asiye na hatia?
ikibidi fanya ivo! Akajitetee huko haiwezi itakula kwake tuuu! lkn Boss wangu apone!...Mfano si unamuona Shetani bado anapeta tuuu!! mpaka leo hii! na anweza kukuua lkn yeye akabaki salama.

Hata shetani ni mtoto wa Mungu usijidai kuwa weye ni mteule!.......Mungu hapangiwi fikiria tu hivi akitoa msamaha wa jumla si mtaumia sana!...halafu mwenzenu yule anapiga story na Mungu km kawa! ile mitaa yote anaijua!
 
Ila wao kama taasisi hawapaswi kushindana na wanafunzi kienyeji kama hivi ilivyo, walipaswa kuwa wawazi kwa kuzingatia sheria na kuonesha booklet. Wao hawaingii hasara kwa kuonesha booklet ila mwanafunzi anapata hasara ya hofu nk kwa kunyimwa booklet inayomfanya aamini ameonewa.
Unajua ile jana nilikuwa na swali kichwani ambalo nilidhani nilikuuliza lakini baada ya kutoona jibu, ikabidi nipitie upya posts zangu lakini nikagundua kumbe sikuwahi kuuliza.

My qiestion is: Hivi hapo LST mnafundishwa Lecturers wenye field experience, espcially Mawakili na Majaji au mnafundishwa na watu aina ya Kabudi?!

Kuna mahali nakumbuka nilisema hili la unapokuwa mahakamani, pale ni battle ground na kama unaandaa watu wa kuwa field, especially mahakamani, natarajia aina fulani ya lecturers and not just any lecturer kwa sababu tu ni Professor!

Please.
 
My qiestion is: Hivi hapo LST mnafundishwa Lecturers wenye field experience, espcially Mawakili na Majaji au mnafundishwa na watu aina ya Kabudi?!
LST wanasema walimu wanatakiwa wawe ni mawakili wenye uzoefu wa miaka 5 na kuendelea pamoja na wengine wenye sifa kama hizo (mahakimu, majaji nk) na wawe active (wanafanya kazi). Lakini uhalisia ni kuwa wanaofundisha ni watu wasioenda mahakamani, ni mawakili ndio kwa kuwa wapo kwenye daftari la usajili, ila hawaendi mahakamani au wakienda ni kwa uchache sana. Ndio maana nikasema kwenye baadhi ya post kuwa, wanashindwa ama hawataki kuwaleta kina TAL au Kibatala au Fatma Karume kufundisha pale labda kwa sababu ya misimamo yao dhidi ha serikali nk.

Ukiingia tovuti ya THE LAW SCHOOL OF TANZANIA ukascroll mpaka chini kabisa kuna majina ya STAFF, waangalie uone kama kwako majina yao ni maarufu kwenye praktisi ya Sheria. Halafu ingia Home | Tanzlii (online library ya Mahakama ya Tanzania) tafuta majina ya walimu hao uone namba za kesi walizosimamia, utakuta ni hamna au ni chache sana. Ukitafuta maamuzi ya Mahakama ya Rufani ndio hutawaona kabisa. Kwa hiyo walimu wengi pale ni aina ya Kabudi, walimu wapo 11 na watumishi wasio walimu wapo 41. Kuna kipindi huwa zinasomwa module huwa wanakuja watu nje ya walimu walioajiriwa pale, hapo ndio kuna majaji wawili, Jaji Fauz na Jaji Luhangisa huja (wapo vizuri sana), na mawakili wa serikali (miyeyusho), na baadhi ya walimu washkaji zao kutoka vyuo vikuu vichache (hivi hivi vinavyotuhumiwa kutoa elimu duni).
 
Asante sana mkuu
 
Mwenyekiti wa Tume ya Kuchunguza masuala ya Law school, ikiwemo wanafunzi wengi kufeli mitihani, anapaswa kuwa mtu Muungwana, Mtulivu, Msikivu na asiye na makuu, anapaswa kuwa mkweli, Mwakyembe hana sifa hizi.

Napinga uteuzi wa Harisson Mwakyembe kuwa Mwenyekiti wa Tume hii kwa vile Haaminiki, si mkweli na ni mpenda sifa.

Kwa mfano, alipokuwa Mwenyekiti wa Tume ya bunge kuchunguza Richmond, katika Taarifa yake aliyoisoma bungeni ALIFICHA BAADHI YA TAARIFA ILI KUOKOA SERIKALI, maana yake ni kwamba alificha taarifa za Mhusika Mkuu wa Jambo lile na kuangushia jumba bovu wasiohusika, leo huyu awezaje kuaminika na kukabidhiwa tume nyingine? JE, SAFARI HII HATOFICHA TAARIFA ILI KUIOKOA SERIKALI?

Mwakyembe akiwa mgombea Ubunge wa Jimbo la Kyela kupitia CCM, aliwaahidi watu wa Jimbo lake kwamba AMEPATA SOKO LA UHAKIKA LA MCHELE WAO NCHINI MAREKANI (ikumbukwe kwamba mchele wa Kyela ndio unaoongoza kwa utamu duniani)

Lakini hadi anang'olewa kwenye ubunge hakuwahi kusaidia hata kilo 10 za mchele wa Kyela kuuzwa Marekani, Mtu kama huyu hastahili kuaminiwa kuongoza tume yoyote ile.

UNAPODANGANYA NYUMBANI KWENU HUWEZI KUAMINIKA UGENINI.

Harrison Mwakyembe ni mtu aliyejaa dharau kubwa sana , huyu hawezi kuwatendea haki watu wenye digrii moja wanaopigania haki yao ya matokeo.

ALIWAHI KUKATAA MASWALI KWAO KYELA kwa kisingizio kwamba wanaomhoji ni Darasa la 7, wakati yeye anamiliki digrii 4 na kwamba watu wasio na elimu wanachopaswa kumhoji ni kuhusu kama hawana hela mifukoni mwao na labda awasaidie. Huyu hafai kuongoza Tume ya kufuatilia haki popote duniani.

Tunamuomba Waziri wa Sheria ATENGUE HARAKA UTEUZI WAKE.

NITASEMA KWELI DAIMA FITNA KWANGU MWIKO.
Time yenyewe haikutakiwa hata kuundwa in first place, hii ni professional exam Ina viwango vyake. Mbona hatukusikia kuunda tume wakati CPA walivyokuwa wakitaga. Watoto Kayumba Sec huko wanapata zero kibao sikuwahi kusikia habari ya tume wala bibi yake tume kuundwa. What's so special on this?
 
Special ni kwa kuwa malalamiko ni ya muda mrefu na maisha ya watu yanaharibika sababu ya kinacholalamikiwa. Hizo professional boards nyingine kutolalamika hakufanyi iwe ndio uhalali wa LST kuminya wanafunzi. Halafu lazima tuwe na mahali pa kuanzia, sasa tumeanza na LST huko kwingine kutafuata. Haki inatakiwa kuonekana imetendeka
 
Amina
 
Mwakyembe na Waziri wamekaza, hawajataka kupokea ushauri juu ya Kamati na uundwaji wake. Sasa Mwakyembe ataiongoza Kamati yake kupokea maoni na ushauri juu ya uendeshaji na ufundishaji wa LST na taaluma ya uwakili kwa ujumla. Maoni yatumwe kabla au ifikapo tarehe 24 Oktoba 2022 kupitia barua pepe: km@sheria.go.tz

Mambo ya uchunguzi wa uhalali wa matokeo na malalamiko, nafikiri ndiyo yanayoitwa "mambo mengine"
brazaj
 
Attachments

  • Screenshot_2022-10-18-18-55-45-515_com.google.android.apps.docs.jpg
    Screenshot_2022-10-18-18-55-45-515_com.google.android.apps.docs.jpg
    119.4 KB · Views: 6
Mwakyembe na Waziri wamekaza, hawajataka kupokea ushauri juu ya Kamati na uundwaji wake. Sasa Mwakyembe ataiongoza Kamati yake kupokea maoni na ushauri juu ya uendeshaji na ufundishaji wa LST na taaluma ya uwakili kwa ujumla. Maoni yatumwe kabla au ifikapo tarehe 24 Oktoba 2022 kupitia barua pepe: km@sheria.go.tz

Mambo ya uchunguzi wa uhalali wa matokeo na malalamiko, nafikiri ndiyo yanayoitwa "mambo mengine"
brazaj
Hii professional exam inavuruga watu na resources bure tu wacha wafu wazikane. Waache wakamatwe tu,vau hapo wamekamatwa wake za wakubwa? Si kwa nguvu na kasi hii wallah ...
 
Hii professional exam inavuruga watu na resources bure tu wacha wafu wazikane. Waache wakamatwe tu,vau hapo wamekamatwa wake za wakubwa? Si kwa nguvu na kasi hii wallah ...
Ndio matokeo ya nguvu ya umma, UMMA ukiamua, mabadiliko hutokea ndani ya sekunde chache tu
 
Back
Top Bottom