Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 128,308
- 245,426
Kuipeleka fainali ya FA Zanzibar ni sawa na kuipeleka fainali hiyo Kenya, Somalia ama Uganda, hakuna timu yoyote kwenye Nchi ya Zanzibar inayosimamiwa na TFF kama zilivyo Nchi nilizozitaja
Wala hakuna sababu yoyote ile iwe ya kijinga au ya maana ya kupeleka fainali hiyo Zanzibar
Sisi wapenda soka wa Tanganyika tuliojiandaa kwenda viwanja vya Tanganyika kuangalia fainali hiyo hatutakubali na kuna mpango wa kwenda Mahakamani kuzuia jambo hilo haramu.
Rais wa TFF hana Mamlaka yoyote ile ya kuamua kuliendesha soka la Tanzania atakavyo yeye kwa sheria za mfukoni mwake
Ni kweli kwamba sisi ni Wajinga lakini siyo Wajinga kiasi hicho.
PIA SOMA
- Kwanini TFF mnaipeleka fainali Zanzibar?
