Napinga fainali ya FA kufanyika Zanzibar, Kisoka Zanzibar ni Nchi nyingine wala haina timu kwenye michuano hiyo

Napinga fainali ya FA kufanyika Zanzibar, Kisoka Zanzibar ni Nchi nyingine wala haina timu kwenye michuano hiyo

Naona hakuna shida sana kama TFF wameona wana maslahi ya kifedha wakipeleka hiyo final huko ughaibuni Zanzibar.

Nchi za wenzetu makombe kama haya final zinaweza kuchezwa nje ya nchi. Mfano Egypt FA final kwa mwaka jana 2023, ilifanyika uwanja wa Al Awwal uliko Riyadh huko Saudi Arabia.

Hii inasaidia maslahi ya kifedha lakini pia kujenga ushawishi wa timu za Egypt huko Uarabuni penisula

So kwa maoni yangu ni sawa hizi final kufanyika Zanzibar ili kujenga ushawishi wa timu za Tanganyika huko Zanzibar lakini pia kusadia vilabu vyetu kimaslahi.
Zanzibar_Football_Association.svg.png

Acha shobo
 
Lakini pia Kwa maslahi ya Mapato Babati isingekuwa sehemu sahihi maana uwanja wa Babati hauna hata jukwaa la kukaa mashabiki.
Fainali ya muungano kati ya simba vs azam uwanja ulikuwa mweupe kama sembe, mashabiki kisoda,

Unazungumzia maslahi gani?

Tatizo huwa hamuangalii mpira mmetoka jukwaa la siasa mnakimbilia JF SPORTS baada ya kusikia issue za muungano
 
Kuipeleka fainali ya FA Zanzibar ni sawa na kuipeleka fainali hiyo Kenya, Somalia ama Uganda, hakuna timu yoyote kwenye Nchi ya Zanzibar inayosimamiwa na TFF kama zilivyo Nchi nilizozitaja

Wala hakuna sababu yoyote ile iwe ya kijinga au ya maana ya kupeleka fainali hiyo Zanzibar

Sisi wapenda soka wa Tanganyika tuliojiandaa kwenda viwanja vya Tanganyika kuangalia fainali hiyo hatutakubali na kuna mpango wa kwenda Mahakamani kuzuia jambo hilo haramu.

Rais wa TFF hana Mamlaka yoyote ile ya kuamua kuliendesha soka la Tanzania atakavyo yeye kwa sheria za mfukoni mwake

Ni kweli kwamba sisi ni Wajinga lakini siyo Wajinga kiasi hicho.
Hao TFF Bodi sijui ujinga gani ni wangese sana mam.........keehhhh.
 
Naona hakuna shida sana kama TFF wameona wana maslahi ya kifedha wakipeleka hiyo final huko ughaibuni Zanzibar.

Nchi za wenzetu makombe kama haya final zinaweza kuchezwa nje ya nchi. Mfano Egypt FA final kwa mwaka jana 2023, ilifanyika uwanja wa Al Awwal uliko Riyadh huko Saudi Arabia.

Hii inasaidia maslahi ya kifedha lakini pia kujenga ushawishi wa timu za Egypt huko Uarabuni penisula

So kwa maoni yangu ni sawa hizi final kufanyika Zanzibar ili kujenga ushawishi wa timu za Tanganyika huko Zanzibar lakini pia kusadia vilabu vyetu kimaslahi.
Punguza ujinga bro.
 
Kupitia uzi huu nimegundua kuwa watanganyika ni watu wanalazimisha muungano wakati wazanzibar hawautaki. Wazanzibar wakija bara hakuna masharti na wanaishi vizuri tu ila mtanganyika akienda Zanzibar unakutana na ubaguzi. Watanganyika ni full kujipendekeza kwa wazanzibar huu ni ujinga mwingine.
Wanajitongozesha.
 
Fainali ya muungano kati ya simba vs azam uwanja ulikuwa mweupe kama sembe, mashabiki kisoda,

Unazungumzia maslahi gani?

Tatizo huwa hamuangalii mpira mmetoka jukwaa la siasa mnakimbilia JF SPORTS baada ya kusikia issue za muungano
Kizimkazi baba! au hujui kama Ikulu imehamia Zenj kutoka Chattco?? Hii nchi ngumu.
 
Wewe ndiye uletae siasa za tundu lissu za zbar na Tanganyika kwenye soka
Kwa akili yako ndogo unadhani ni sahihi kwa ligi ya Tanganyika fainali kufanyika Zanzibar, au utuambie lini Uliona Kipanga na KMKM wakicheza Kwa Mkapa fainali ya Karume Cup?
 
Shida mijitu inajipendekeza mdogomdogo utasikia baadhi ya mechi za ligi kuu kupelekwa Zenji hapa wanatest tu ikikubali utasikia kikao cha TFF kimepitisha sheria ya ligi kuchezwa huko
 
Back
Top Bottom