Napinga GSM kuingia mkataba na NBC ili kuendesha ligi kuu ya soka Tanzania

Mkuu, ukijua tofauti iliyopo kati ya KUENDESHA LIGI na KUDHAMINI LIGI, utakua "MTU SANA"
 
Kwa ufala uliofanyika juzi pale ilulu, tutarajie kuona mengi, binafsi maji yakizidi unga naachana kabisa na ushabiki wenyewe naanza kuangalia game za mbele tu ..
Mkuu unaonekana una hasira sana, Relax, ligi yetu kupata wadhamini wengi isiwe sababu ya wewe kutaka kutapika nyongo, mie napenda sana mpira wa miguu sifungamani na upande wa timu yoyote na ninaona fahari na furaha sana ligi yetu sasa inachanja mbuga kwa kuwa na wadhamini wengi ambapo itapelekea hata timu zetu kuwa na fedha na hata wachezazji watafaidi vipaji vyao kwa kulipwa kwa wakati na timu zao wanazozotumikia,hata uko mbele unapopasema kuna kampuni kibao zinadhamini ligi za huko na ndo maana ligi zao ni bora na hii inatokana na kuwepo kwa udhamini katika hizo ligi,ungekuwa umekasirikia viwanja vyetu ningeungana na wewe maana kuna viwanja miundombinu haipo njema.
 
NBC hawajaomba colabo
 
Sijui lakini naona hata Ulaya kuna wadhamini wengi tu kwenye ligi moja, hapa suala ni WELEDI tu. Kama GSM wanaingia wakiwa na MALENGO JIFICHI, basi ligi itaharibika licha ya kuwa na mapesa mengi. GSM wanatoa 2.1B/= ambazo wanasema - wao, GSM na TFF - kuwa ni kwa ajili ya wachezaji kupitia kwa viongozi wa hizo timu. Binafsi sioni shida, ila twende nao, kama SI WELEDI tutawaona mapema tu na madudu yao. Subira huvuta heri!
 
Nadhani kuna tatizo hapa la kuelewa malengo ya GSM na malengo yako, wewe kama shabiiki wa Yanga na GSM! Wewe una malengo yako na GSM ana malengo yake ingawa mnatofautiana kwenye kuyawasilisha kwetu. GSM kafanya kwa vitendo na wewe unafanya kwa maneno ya ushabiki. Hiyo ndiyo tofauti yenu! Nembo, nembo, what is nembo!? Wewe nembo ya GSM pale ilipokuwa HOME SHOPPING CENTRE (HSC) unaijua au ni ushabiki tu?
 
Tueleweshe basi

Sent from my SM-J500H using JamiiForums mobile app
Anayeendesha ligi ni BODI YA LIGI. Hiki ni chombo kilichoundwa na vilabu ili kuendesha ligi kwa niaba ya shirikisho la mpira Tanzania (TFF).

Anayedhamini ligi ni mfanyabiashara yeyote aliyeweka fedha yake katika ligi kwa lengo la yeye kupata faida.
Faida hii inaweza kuwa ni in terms of kujitangaza na hivyo kuongeza mauzo yake au kupata fedha kupitia malipo ya vifurushi vya visimbuzi.

Kwa sasa ligi yetu ina wadhamini watatu:-
1. NBC, mdhamini mkuu.
2. Azam TV, Mdhamini mtangazaji.
3. GSM, Mdhamini mwenza.

Bado kuna nafasi kwa makampuni, taasisi au watu binafsi wengine kudhamini ligi yetu.

Watu hao wanaweza kuwa:-
4. Erythrocyte Co. Ltd
5. Mzee Mpili enterprises
6. BongoZozo Sports
7. Tozo & Mgawo Associates
8. Metacha Mnata industries
9.
......
Hawa ni wadhamini na kamwe sio waendeshaji wa ligi.

Nitasikitika sana kama ukitumia maneno "kudhamini ligi" na "kuendesha ligi" interchangeably.
 
Ni kweli kila ulichoandika isipokuwa huna jicho la 3
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…