Napinga hoja ya RC Makalla ya kulazimisha Mabasi yote ya Mikoani kupakia na kushusha abiria Stendi ya Magufuli pekee

Alichotamka RC Makala ni formality tu lakini practically ni ngumu kutekelezeka...

Na hii ndiyo shida ya matamko ya hisia binafsi, yaliyojaa usiasa na yasiyofanyiwa utafiti wa kutosha maana hayawezi kudumu kwa sababu ya ugumu ktk utekelezaji wake....

Ndivyo ilivyo ktk stendi zote katika miji yote nchini..

Kwani ukiachilia mbali uwepo wa STENDI KUU YA MABASI, vivyo hivyo wamiliki au kampuni hizi za mabasi zina ofisi zao kuu binafsi au yard zao za kupaki magari yao katika locations tofauti tofauti iwe jijini DSM au mikoani/miji mingine...

Sasa utawezaje kunizuia mimi abiria nisipandie bus linapolala karibu na mimi mita 100 tu na badala yake unilazimishe niende 30km ilipo stendi..?

Kauli au agizo la Makala ni formality tu lakini ukweli ni kuwa practicability yake ni ngumu sana...

Maagizo ya namna hii yasiyofanyiwa utafiti mara nyingi huwa hayadumu...
 
Nakazia hoja zako mkuu........

Nadhani kuna ulazima wa kuanza kuwapima akili viongozi wa umma kabla ya kuwapa madaraka.......

Nachelea kuamini kuwa kiongozi mwenye dhamana ya mamilioni ya wananchi akaja na kauli ya kijinga hiyo........
 
mbona utaratibu uliokuwepo ulikua mzuri
kwa anayekaa karibu na ofice booking akitaka kuwah hilo gar anawah kum na moja alfajir anapata lift mpk maguful kisha wanapanda waliopo maguful na badae safar inaanza.ugum umetokea wap.mi naingia na gar saa tisa usik.hta nikishuka magufl siwez munua kiti chcochot nawaz kuhangaika na usafir wa iunifikisha manzese
gar wana ofis zao sheklngo kwa nn wasinipe rift?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hiyo kauli ni ya kimhemko, wala isikupe shida. Kwa sababu stendi ya mbagala kwa mabasi ya mikoa ya kusini ina kazi gani?
Je, na wale waliokodishwa ofisi shekilango na maeneo jirani walipanga hapo kwa sababu ipi?
Pia stendi ya mabasi ya mikoani ilihamishwa nje ya jiji kuruhusu mji kukua na kupanuka vizuri.
Hivyo hii kauli haina mashiko na haina maisha marefu.
 
gapohapo wese linalika balaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dar es Salaam haihitaji kuwa na stendi kuu ya mabasi.Ukosefu wa uelewa wa biashara ya usafiri na akili ndogo za wapanga mji zinazopenda centralization na kuona majengo makubwa makubwa ndizo zimetufikisha katika matatizo kama haya.
Labda tutofautishe kati ya jiji na mkoa, jiji sio lazima liwe na centralized system kwa sababu husababisha misongamano isiyo ya lazima.
Pia kwa kuongezea ingetakiwa kila eneo la Dar es Salaam liwe na kila kitu muhimu sio lazima ukihitaji kitu uende kariakoo au posta
 

Acha nadharia nyingiii wewe sio msemaji wa kila mtu. Mimi pia ni abilia binafsi naridhika na kuwapo kwa utaratibu wa kushusha na kupakia stand ili kupunguza foleni zisizo za lazima pia dar kuna makampuni zaidi ya 50 ya mabus yote yakitumia utaratibu unaotaka kutakarika mjini? Eti abilia wanaopanda Luxury wana pesa hawaitaji huduma ya mama lishe huu uchunguzi ulifanya lini? Naweza kuona Questionnaire?
 

Acha kujijaza umuhim we ni nani kuzidi wengine? Panda ndege kama hutakj usumbufu! Maskini mna taabu sana
 
Ni upuuzi tuu. kinacholengwa hapo ni usafiri wa bajaji na daladala na taksi. zaidi ya hapo sijaona biashara nyingine inayoathirika.
Mimi nikisafiri ninapofika mbezi hata ukinishusha hakuna nitakachonunua zaidi sana labda maji.. ambayo ni nadra sana kwa sababu nia nzima ninakuwa nimeshahudumiwa kwa maji na chakula. Labda niwe na tumbo la kuhara nitaenda choo cha kuipia.
 
Kwanza alitakiwa akae na wadau kabla ya kutoa amri zake.amewahi Kujiuliza ni kwa nini mabasi mengi yana booking ofisi na huchukua abiria nje ya kituo?
Ni mbinu ya kibiashara hii.nowdays magari ni mengi na yote mazuri.So Ili ku add value kampuni zenye mabasi mengi zimeyagwa mabasi karibu Kila wilaya Ili kuwavutia wasafiri wa sehemu husika..mfano mimi ninaishi kigamboni.nikiwa na safari huwa sifikirii mara mbili nakara tiketi z kilimanjaro cause katuletea gari huku.so asubuhi badala ya kuliwahi mbezi nalisubiri tu hapo darajani safari inaanza ..na nikirudi badala ya kuachwa mbezi linatuleta hadi home huku kmboni .vivyo hivyo kwa maeneo mengine..watu huoanda magari yanayofika maeneo wanyoshi..
Hivi makala hakumsikiliza shabiby au ndio dharau
 
Mkuu, hatutofautiani, ila nadhani ni kutoelewa tu.

Mimi sijasema popote toka mwanzo kuwa Makalla yupo sahihi, bali ninachosema ni kwamba sababu alizoshirikisha ni za kisiasa tu. Sababu muhimu zipo kwa nini hayo mabasi yanatakiwa kupakia na kushusha abiria Stendi Kuu, na nimekwishazitaja katika maandiko yangu humu.

Sijaandika sehemu yoyote kupinga kuwepo kwa usafiri mwingine wanaoweza kuumudu wasiokuwa na uwezo wa taxi. Sote tunajua uwezo mdogo uliopo kuondoa matatizo yanayowakabili wananchi, siyo wasafiri pekee. Kuwepo kwa kituo cha mabasi ni hatua moja, tuendelee kutafuta njia za kufanikisha kitupo hicho kifanye kazi kwa ufanisi. Yote hayawezi kuja kwa wakati mmoja.
 
Usikose maana ya mfananisho ilianzia wapi.
Sio mfananisho wa uwezo wa wasafiri wa vyombo hivyo; ni mfananisho wa miundo mbinu na sehemu zilipo.
 
Ujumbe uu apelekewe Makalla auone kwenye file, tafadhali. Nakala kwa SSH
 
What useless notion!
 
Huu utaratibu upo mikoa yote, Ila Dar ilikuwa haijaguswa, Sasa mmeguswa full matusi, mbona mnajiona special Sana, waliotembea kidogo duniani wanasema utaratibu huu upo miji mingi mikubwa duniani, nyie mnataka kila mtu Basi limshushe nyumbani kwake.

Mbona wenzenu wa mkoa tunavumilia, tukiingia saa nane usiku, tunakodi bajaji hadi home!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…