Napinga hoja ya RC Makalla ya kulazimisha Mabasi yote ya Mikoani kupakia na kushusha abiria Stendi ya Magufuli pekee

Napinga hoja ya RC Makalla ya kulazimisha Mabasi yote ya Mikoani kupakia na kushusha abiria Stendi ya Magufuli pekee

Alichotamka RC Makala ni formality tu lakini practically ni ngumu kutekelezeka...

Na hii ndiyo shida ya matamko ya hisia binafsi, yaliyojaa usiasa na yasiyofanyiwa utafiti wa kutosha maana hayawezi kudumu kwa sababu ya ugumu ktk utekelezaji wake....

Ndivyo ilivyo ktk stendi zote katika miji yote nchini..

Kwani ukiachilia mbali uwepo wa STENDI KUU YA MABASI, vivyo hivyo wamiliki au kampuni hizi za mabasi zina ofisi zao kuu binafsi au yard zao za kupaki magari yao katika locations tofauti tofauti iwe jijini DSM au mikoani/miji mingine...

Sasa utawezaje kunizuia mimi abiria nisipandie bus linapolala karibu na mimi mita 100 tu na badala yake unilazimishe niende 30km ilipo stendi..?

Kauli au agizo la Makala ni formality tu lakini ukweli ni kuwa practicability yake ni ngumu sana...

Maagizo ya namna hii yasiyofanyiwa utafiti mara nyingi huwa hayadumu...
 
Naunga mkono hoja. Baadhi ta wenye mabasi wenye stendi zao pale Sinza Shekilango kama Kilimanjaro, Dar Lux, Marangu Coach na mengine, wenye mabasi zaidi ya moja kwa route ya Moshi Arusha, njia rahisi kwao ni route ya Bagamoyo Msata, na sio njia ya Chalinze, kuwalazimisha lazima waanzie Stendi mpya ni kuwatesa tuu bure abiria, after all, wengi wa abiria wa mabasi hayo, haswa wale abiria wa 1st Class, sio wa type ya kununua vitu kwa machinga au kula kwa Mama Ntilie! Hivyo kama nia ni kuwasaidia Machinga na mama ntilie, then, hizo ni sababu alizotoa Mkuu wa Mkoa ni sababu za kijinga sana!.

Hatuwezi kuendelea kuendesha nchi kijinga jinga hivi halafu utegemee tutapata mafanikio. Il tuendelee , la kupata maendeleo ya kweli de must stop such nonsense!.

p
Nakazia hoja zako mkuu........

Nadhani kuna ulazima wa kuanza kuwapima akili viongozi wa umma kabla ya kuwapa madaraka.......

Nachelea kuamini kuwa kiongozi mwenye dhamana ya mamilioni ya wananchi akaja na kauli ya kijinga hiyo........
 
mbona utaratibu uliokuwepo ulikua mzuri
kwa anayekaa karibu na ofice booking akitaka kuwah hilo gar anawah kum na moja alfajir anapata lift mpk maguful kisha wanapanda waliopo maguful na badae safar inaanza.ugum umetokea wap.mi naingia na gar saa tisa usik.hta nikishuka magufl siwez munua kiti chcochot nawaz kuhangaika na usafir wa iunifikisha manzese
gar wana ofis zao sheklngo kwa nn wasinipe rift?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Amos Makalla ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na Mfadhili wa zamani wa bendi ya FM ACADEMIA ya Kinondoni, bila kufanya utafiti wowote ule leo ametoa amri ya kulazimisha mabasi yote ya mikoani kuanzia safari zao kwenye kituo kikuu cha mabasi ya mikoani cha Mbezi Luis, kinachoitwa kituo cha mabasi cha Magufuli na kushushia abiria wake hapohapo.

Lengo kuu la kauli yake hii ni kujaribu kukusanya watu ili kuneemesha wafanyabiashara waliojazana kwenye stendi hiyo bila mpangilio wowote, Makalla anaamini kwamba abiria wote wakishushwa ama kuanzia safari zao hapo basi watanunua bidhaa za wamachinga waliojazana hapo, hivi ndivyo akili yake ilivyomtuma, kwamba abiria wakomeshwe ili kufurahisha wafanyabiashara, amesahau kwamba abiria ni bora kuliko wamachinga kwenye mustakabhali wa Safari, hata hivyo sikubaliani naye.

Mbezi Luis eneo ilikojengwa Stendi ya Mabasi ya Mikoani ni nje kabisa ya jiji la DSM , kulazimisha Mabasi yaliyokuwa yanaanzia safari zake Mbagala, Tandika au Kigamboni kuacha kazi hiyo na kulazimisha sasa lazima yote yaanzie Nje ya jiji ni sawa na unyama , kwamba sasa aliyekuwa anapandia basi Mbagala akodi teksi kwa zaidi ya gharama ya tsh elfu 30 ili kulifuata basi Mbezi Luis, kwa vile tu Amos Makalla kajisikia hivyo haikubaliki na ni lazima ipingwe kwa nguvu zote.

Alichotakiwa kufanya Mh RC ni kuhakikisha kwamba basi lolote kutoka kwenye yard yoyote ile binafsi linakoanzia safari lisiondoke DSM bila ya kupita Stendi kuu ama lishushe litakako ila ni lazima lije stendi kuu, Vinginevyo Mh Makalla atamke hadharami Maslahi yake binafsi atakayopata kwa kuwatesa abiria wa Kigamboni, Vikindu , Chamanzi, Mbagala, Tandika na kwingineko waliokuwa wanapata ahueni ya kuanzia safari kwenye maeneo yao ya karibu.

Naomba kuwasilisha.
Hiyo kauli ni ya kimhemko, wala isikupe shida. Kwa sababu stendi ya mbagala kwa mabasi ya mikoa ya kusini ina kazi gani?
Je, na wale waliokodishwa ofisi shekilango na maeneo jirani walipanga hapo kwa sababu ipi?
Pia stendi ya mabasi ya mikoani ilihamishwa nje ya jiji kuruhusu mji kukua na kupanuka vizuri.
Hivyo hii kauli haina mashiko na haina maisha marefu.
 
Lakini kweli najaribu kufikiria kwa mfano mtu kapitia njia ya bagamoyo stendi ya mwenye gari kama kilimanjaro pale shekilango anapitia mwenge alafu abiria wake wengi wanakuja hadi shekikango alafu eti arudi nao hadi mbezi wakashukie huko alafu gari sasa lutoke mbezi lije shekilango tena wakati huo huo kuna abiria wanahitaji kuja kushukuia tena shekilango wao sasa inabidi waoande tena daladala. Hapana hapo kakosea sana kwa kweli huu ni usumbufu mkubwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
gapohapo wese linalika balaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dar es Salaam haihitaji kuwa na stendi kuu ya mabasi.Ukosefu wa uelewa wa biashara ya usafiri na akili ndogo za wapanga mji zinazopenda centralization na kuona majengo makubwa makubwa ndizo zimetufikisha katika matatizo kama haya.
Labda tutofautishe kati ya jiji na mkoa, jiji sio lazima liwe na centralized system kwa sababu husababisha misongamano isiyo ya lazima.
Pia kwa kuongezea ingetakiwa kila eneo la Dar es Salaam liwe na kila kitu muhimu sio lazima ukihitaji kitu uende kariakoo au posta
 
Kufananisha Uwanja wa Ndege na Stendi ya Mabasi si busara hata kidogo....au Kufananisha Abiria wa Ndege na Basi nako si busara pia.

Hata kwa Abiria wa Treni utaona karibia asilimia 90 ya abiria, haswa wale wa daraja la chini(economic class) hulazimika kulala hapohapo Kituoni kungoja safari au kama wamefika husubiri kupamabazuke ndio waende wakatafute usafiri wa kwenda kwao.

Abiria anayemudu kusafiri kwa Ndege itakuwa ni ajabu kama atashindwa kulipia Taxi hata sh 50,000 kwenda au kutoka Airport.

Abiria wengi Wanaochagua usafiri wa Mabasi pia wapo wa makundi tofauti....wapo ambao wako tayari kulipa ziada ili tu kusafiri kwa amani na starehe (Luxury)...ila pia wapo wanalazimika kupanda basi lolote lile ali mradi wafike waendapo.

Maamuzi ya Mheshimiwa hayakujali yote hayo zaidi ya kutafuta tu njia ya mkato kuwafurahisha Wamachinga, Mamalishe au Watu fulani kama sio maslahi yake binafsi...na ukifuatilia utagundua yeye hajatumia huu usafiri kwa miaka 20 kama sio 30 iliyopita.

Abiria wengi wanaotumia Mabasi ya Luxury sidhani kama wanatumia chakula cha Mama Lishe, wengi wakishakula Mchana njiani (Korogwe/Mombo kwa watokao Kaskazini) hawatohitaji tena kula....huenda hilo nalo yeye hajui.

Au la Kama Mkuu ndio kaamau basi yale Mabasi ya Luxury yaruhusiwe kufika vituo vyao kwa tozo za ziada kama shida ni pesa ili Kampuni zifanikishe lengo lao la kuwahudumia Abiria wao wa daraja la Luxury....au hilo nalo hataki? kama hataki ana ajenda gani fiche huyu?

Option nyingine inayobaki ni kwa Wenye Mabasi kuandaa usafiri Mbadala wa Minibus kuwatoa na kuwapeleka Abiria wao wa Daraja la Luxury hapo stendi, ingawa kutakuwa tena na kero ya kuhamisha mizigo.

Mkuu atambue kama ambavyo yeye anavyopenda kusafiri kwa raha mustarehe basi wapo pia Wanachi Wenzake waliotayari kulipa ziada hata kwa kushinda njaa safari nzima ili tu wasafiri kwa amani na starehe bila ya kero.

Kwa wale Abiria wa madaraja ya kawaida a.k.a kajambanani ni bahati mbaya kwao kwani hiyo ndio njia pekee Kiongozi wenu kaona inawafaa kwa kushinikiza mkarundikane pale Kituoni na kina Wamachinga, Mamalishe, Wapagazi na Mikokoteni yao, Wapiga debe/Wakatisha tiketi n.k. kama sehemu ya kudumisha ujamaa.

Naomba nimkumbushe Mkuu kuwa Wapo Abiria hawapendi kupitia hayo yote....sasa je wao wafanyeje?.

Na kama Waziri husika naye ataridhia hili basi naye atakuwa na akili hizohizo za RC.

Acha nadharia nyingiii wewe sio msemaji wa kila mtu. Mimi pia ni abilia binafsi naridhika na kuwapo kwa utaratibu wa kushusha na kupakia stand ili kupunguza foleni zisizo za lazima pia dar kuna makampuni zaidi ya 50 ya mabus yote yakitumia utaratibu unaotaka kutakarika mjini? Eti abilia wanaopanda Luxury wana pesa hawaitaji huduma ya mama lishe huu uchunguzi ulifanya lini? Naweza kuona Questionnaire?
 
Mpuuzi huyu mkuu wa mkoa, yaani mie naenda moshi nakaa tegeta na nimekata tiketi ya dar express inapita mlango wa nyumbani kwangu niende mbezi??? Pumbavu!
Yaani mie nakaa shekilango nimetoka mbeya na ne force inashushia kituo cha mwisho parking yao mita 50 toka nyumbani kwangu eti nishuke mbezi..nyambafu!
Naenda tanga na tahmeed ila dar nakaa bunju gari zinapita hapa unaniambia niende nikaifuate mbezi...shit...
Waendelee kuupiga mwingi...

Acha kujijaza umuhim we ni nani kuzidi wengine? Panda ndege kama hutakj usumbufu! Maskini mna taabu sana
 
Ni upuuzi tuu. kinacholengwa hapo ni usafiri wa bajaji na daladala na taksi. zaidi ya hapo sijaona biashara nyingine inayoathirika.
Mimi nikisafiri ninapofika mbezi hata ukinishusha hakuna nitakachonunua zaidi sana labda maji.. ambayo ni nadra sana kwa sababu nia nzima ninakuwa nimeshahudumiwa kwa maji na chakula. Labda niwe na tumbo la kuhara nitaenda choo cha kuipia.
 
Kwanza alitakiwa akae na wadau kabla ya kutoa amri zake.amewahi Kujiuliza ni kwa nini mabasi mengi yana booking ofisi na huchukua abiria nje ya kituo?
Ni mbinu ya kibiashara hii.nowdays magari ni mengi na yote mazuri.So Ili ku add value kampuni zenye mabasi mengi zimeyagwa mabasi karibu Kila wilaya Ili kuwavutia wasafiri wa sehemu husika..mfano mimi ninaishi kigamboni.nikiwa na safari huwa sifikirii mara mbili nakara tiketi z kilimanjaro cause katuletea gari huku.so asubuhi badala ya kuliwahi mbezi nalisubiri tu hapo darajani safari inaanza ..na nikirudi badala ya kuachwa mbezi linatuleta hadi home huku kmboni .vivyo hivyo kwa maeneo mengine..watu huoanda magari yanayofika maeneo wanyoshi..
Hivi makala hakumsikiliza shabiby au ndio dharau
 
Tunahitilafiana padogo tu. Huoni nilipokujibu nilianza na "Ni kweli"? Hii ni dhahiri ninakubaliana na hoja yako hasa ile ya kuhakikisha mabasi yanashusha na kupakia pale Mbezi. Maana ninaona changamoto ya kila basi kushusha holela. Tunapohitilafiana ni namna ya utekelezaji. Wewe unaona Makalla yupo sahihi kwa kauli yake. Mimi ninaona hayupo sahihi kwa sababu hajaweka mazingira rafiki katika hili. Wewe mwenyewe unaliona hili na umefafanua vema tu kuhusu mazingira ya stend na hali ya jiji kwa sasa. Angepigana kuboresha haya kisha akapiga hilo biti.

Kuhusu taxi,ni sawa. Lakini, watu wote wana uwezo wa taxi? Njia ziwepo nyingi, zote zikiwa zinaridhisha ili mtu afanye uchaguzi sahihi kulingana na kipato, muda na mahali anakokusudia kufika. Wengi tunaongelea usafiri wa wengi kama vile daladala na mwendokasi kutokana na kugusa kundi kubwa. Nimesafiri mara kadhaa, pale Mbezi bado hapajatulia. Ni vurugu tu.

Yaweza kuwa ni mtazamo wangu lakini, huenda kuna wengi mnaona mambo ni super! Nisikaze misuli ya shingo tu.
Mkuu, hatutofautiani, ila nadhani ni kutoelewa tu.

Mimi sijasema popote toka mwanzo kuwa Makalla yupo sahihi, bali ninachosema ni kwamba sababu alizoshirikisha ni za kisiasa tu. Sababu muhimu zipo kwa nini hayo mabasi yanatakiwa kupakia na kushusha abiria Stendi Kuu, na nimekwishazitaja katika maandiko yangu humu.

Sijaandika sehemu yoyote kupinga kuwepo kwa usafiri mwingine wanaoweza kuumudu wasiokuwa na uwezo wa taxi. Sote tunajua uwezo mdogo uliopo kuondoa matatizo yanayowakabili wananchi, siyo wasafiri pekee. Kuwepo kwa kituo cha mabasi ni hatua moja, tuendelee kutafuta njia za kufanikisha kitupo hicho kifanye kazi kwa ufanisi. Yote hayawezi kuja kwa wakati mmoja.
 
Kufananisha Uwanja wa Ndege na Stendi ya Mabasi si busara hata kidogo....au Kufananisha Abiria wa Ndege na Basi nako si busara pia.

Hata kwa Abiria wa Treni utaona karibia asilimia 90 ya abiria, haswa wale wa daraja la chini(economic class) hulazimika kulala hapohapo Kituoni kungoja safari au kama wamefika husubiri kupamabazuke ndio waende wakatafute usafiri wa kwenda kwao.
Usikose maana ya mfananisho ilianzia wapi.
Sio mfananisho wa uwezo wa wasafiri wa vyombo hivyo; ni mfananisho wa miundo mbinu na sehemu zilipo.
 
Naunga mkono hoja. Baadhi ta wenye mabasi wenye stendi zao pale Sinza Shekilango kama Kilimanjaro, Dar Lux, Marangu Coach na mengine, wenye mabasi zaidi ya moja kwa route ya Moshi Arusha, njia rahisi kwao ni route ya Bagamoyo Msata, na sio njia ya Chalinze, kuwalazimisha lazima waanzie Stendi mpya ni kuwatesa tuu bure abiria, after all, wengi wa abiria wa mabasi hayo, haswa wale abiria wa 1st Class, sio wa type ya kununua vitu kwa machinga au kula kwa Mama Ntilie! Hivyo kama nia ni kuwasaidia Machinga na mama ntilie, then, hizo ni sababu alizotoa Mkuu wa Mkoa ni sababu za kijinga sana!.

Hatuwezi kuendelea kuendesha nchi kijinga jinga hivi halafu utegemee tutapata mafanikio. Il tuendelee , la kupata maendeleo ya kweli de must stop such nonsense!.

p
Ujumbe uu apelekewe Makalla auone kwenye file, tafadhali. Nakala kwa SSH
 
Mkuu, hatutofautiani, ila nadhani ni kutoelewa tu.

Mimi sijasema popote toka mwanzo kuwa Makalla yupo sahihi, bali ninachosema ni kwamba sababu alizoshirikisha ni za kisiasa tu. Sababu muhimu zipo kwa nini hayo mabasi yanatakiwa kupakia na kushusha abiria Stendi Kuu, na nimekwishazitaja katika maandiko yangu humu.

Sijaandika sehemu yoyote kupinga kuwepo kwa usafiri mwingine wanaoweza kuumudu wasiokuwa na uwezo wa taxi. Sote tunajua uwezo mdogo uliopo kuondoa matatizo yanayowakabili wananchi, siyo wasafiri pekee. Kuwepo kwa kituo cha mabasi ni hatua moja, tuendelee kutafuta njia za kufanikisha kitupo hicho kifanye kazi kwa ufanisi. Yote hayawezi kuja kwa wakati mmoja.
What useless notion!
 
Huu utaratibu upo mikoa yote, Ila Dar ilikuwa haijaguswa, Sasa mmeguswa full matusi, mbona mnajiona special Sana, waliotembea kidogo duniani wanasema utaratibu huu upo miji mingi mikubwa duniani, nyie mnataka kila mtu Basi limshushe nyumbani kwake.

Mbona wenzenu wa mkoa tunavumilia, tukiingia saa nane usiku, tunakodi bajaji hadi home!!!
 
Back
Top Bottom