Napinga hoja ya RC Makalla ya kulazimisha Mabasi yote ya Mikoani kupakia na kushusha abiria Stendi ya Magufuli pekee

Kama kuna fani inadharauliwa ni ya mipango miji. Wao wanaonekana kuwa kazi yao kubwa ni kugawa viwanja tu. Walitakiwa saa hizi wawe wanatayarisha mazingira ya mji utakavyokuwa miaka 50 ijayo. Mipango hiyo inatakiwa iwasilishwe kwa wananchi ili wachangie mawazo na mawazo yao yatiliwe maanani. Mipango inayotarishwa sasa hivi ni academic na baada ya kupokelewa inatupwa kabatini na wana siasa wanafanya wanavyotaka. Mfano ni Dodoma. Mpango Mji wa awali umesahaulika bila wananchi kupewa sababu za kuuacha.

Amandla...
 
Hata stendi ya mabasi ya Mwanza kipindi inatolewa city center kupelekwa Nyegezi kulikuwepo hoja hizi hizi.

Leo hii Nyegezi siyo nje ya mji tena na uanzishwaji wa utitiri wa routes za daladala zimeifanya stand iwe kama IPO city center tu.

Miji "hupanuliwa" wa staili hiyo.

Labda hoja Ingekuwa uwepo wa miundombinu ya ku-accomodate watu wote watakaotumia be stendi hiyo
 
Jiwe alikuwa anaamini zaidi katika ku consolidate mambo kuliko kawaida.
 
Huu ni mfano mzuri. Shida ni kuwa watu walisumbuka sana kabla ya mji kupanuka kufika Nyegezi. hapakuwa na haja hiyo. Wangetenga eneo la kutosha kwanza, kufanya kituo cha kupitia (transit) na pale mji unapofika ndio inageuzwa kuwa terminal yenye nafasi ya kutosha tu. Sitashangaa kusikia kuwa tayari kituo kipya kimeisha elemewa wakati vingekuwa viwili shida isingekuwa kubwa kiasi hicho.

Amandla...
 
Aisee! Mkuu P, naona umerejea kwenye u bora wako sasa.
 
Hii kero pia iende kwa mikoa mingine mfano Iringa na Dodoma. Pale iringa stend kuu iko karibu kilometer 20 kutoka iringa mjini na mabasi yanalazimishwa kushusha abiria wote stend kisha yanaenda mjini yakiwa tupu na abiria wanalazimika kupanda dala dala kwenda mjini huko huko ambako mabasi yanaenda.
 
Kongole mkuu [emoji122][emoji122]
 
Suluhisho lilipaswa kwa serikali, wamiliki wa mabasi, wawakilishi wa abiria na wadau wengine kukaa chini kuzungumza kiuhalisia na kuafikiana, kisha wataalamu wakae chini ili kuja na mapendekezo mahususi kwa mamlaka husika.
 
Sasa hii ni akili au tope yaani bus inakwenda mjini tupu wakati huo huo Kuna abiria wanakwenda mjini pia[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kinachotakiwa ni kampuni za usafirishaji kuanzisha shuttle bus kwaajili ya kukusanya abiria wake maeneo husika kama vile shekilango lakini mabasi yanatakiwa kuanzia na kumalizia safari kwenye stendi kuu “Terminal” hivi ndivyo hata majiji yaliyoendelea yalivyopangwa.
Hata Malaori kuingia mpaka ndani ya mji au bandarini ni udhaifu wa watu wa mipango miji.Reli ilitakiwa itumike kutoa mizigo bandarini mpaka kwenye ICD zilizopo nje ya mji.
 
Suluhisho lilipaswa kwa serikali, wamiliki wa mabasi, wawakilishi wa abiria na wadau wengine kukaa chini kuzungumza kiuhalisia na kuafikiana, kisha wataalamu wakae chini ili kuja na mapendekezo mahususi kwa mamlaka husika.
Tatizo la Tanzania ni hili , Mtu anapokuwa kiongozi ghafla anabadilika na kuwa mwenye akili kuliko yeyote yule
 

Hii itafungua hata biashara za motels na lodges .
 
Jiwe alikuwa anaamini zaidi katika ku consolidate mambo kuliko kawaida.

Nadhani zaidi alikuwa haamini katika Planning. Aliona ni kupoteza muda na ni njia ya kuiba pesa. K.m. mradi wa bwawa la Nyerere unafanyika bila tafiti za kutosha za awali kuhusua challenges zilizoainishwa katika taarifa za kimazingira n.k. za awali ambazo zilifanya wenzie kusita kuendelea nao. Hakuwa sahihi katika hili.

Amandla...
 
Jiwe alikuwa anaamini serikali inajua na inaweza kila kitu
Suluhisho lilipaswa kwa serikali, wamiliki wa mabasi, wawakilishi wa abiria na wadau wengine kukaa chini kuzungumza kiuhalisia na kuafikiana, kisha wataalamu wakae chini ili kuja na mapendekezo mahususi kwa mamlaka husika.
 
Pamoja Sana mkuu
 
Duh!! Ni wewe kweli? Mbona lugha kali sana umetumia kama mwandishi mwandamizi?

Ni kweli kauli ya mkuu wa mkoa haikubaliki kisiasa, kijamii, kiusalama, kiafya na kiuchumi, lakini michang ya maoni na ushauri iwe ni ya kistaarabu kwa nia ya kujenga. Mkuu huyo wa mkoa walimleta hapo Dar kwa kuwa kuna 'elites' walimtaka kwa kuwa anaweza kunyumbulika watakavyo kwa manufaa yao, lakini ukweli hauwezi mkoa huo kwa vyovyote na matokeo mtaanza kuyashuhudia kadri siku zinavyosogea.

The only solution is to agree in common that Magufuli Bus Terminal is retained where it is and to prevail its intended purposes as an iconic central surface land transportation hub to both upcountry and across the borders (Ugana, Congo, Zambia, Kenya, Malawi, Zimbabwe, Rwanda, Msumbiji, South Sudan and Burundi).

However, the infrastructure feeding the bus terminal is not convenient and friendly.. therefore as the construction continues at Mbezi Louis, the transporters have to be permitted to do what is beneficial to the passengers, bus owners, and government on the other hand on revenue collection through a well-streamlined plan.

Meanwhile, the government of the United of Tanzania is solemnly requested to process for the new backup bus terminals built at Tegeta/Boko or Bunju and Mbagala to consistently provide quality services to the passengers as diversified significant stakeholders for the economic generation by the investors in the transport sectors and common citizens with small business operations.
 
Stand ya kimataifa wakati wateja wako na utaratibu siyo wakimataifa.
Tuna safari ndefu.
Hilo Jjji lilitakiwa liwe na stand kuu 3 kwa jiografia yake.
1.Mbagala
2.Mbezi
3.Tegeta/kawe
Basi likipita stand kuu mojawapo ndipo lielekee kwenye ofisi yake

Hungesikia matamko ya ajabu yasiyomsaidia msafiri
 
Ni sawa na uwanja wa ndege, ambako ukitaka kusafiri, kama unatokea Kawe, ni lazima utafute usafiri wa kukufikisha JKNIA,
Usifananishe usafiri wa anga na ardhini ni vitu viwili tofauti, utaratibu huu wa Makalla utakua ni usumbufu kwa baadhi ya abiria wanaotokea ktkt ya mji kesi za kuchelewa usafiri zitakua nyingi kutokana na foleni
 
Kiukweli hata mimi nimemshangaa sana huyu jamaa lakini ikiwa amaeshindwa kuwapanga vizuri watu wanaofanya biashara kiholela nje ya ofisi yake mweneyewe hawezi kua na mpango mzuri kwa mkoa mzima.

Kwanza anachoshindwa kuelewa makala ni kua ile stendi haitoshi kwa mabasi yote kuingia mle tofauti na iliyvyokua ubungo,Pili logistic za Mbezi ni tofauti na Ubungo kabisa hivyo kwa abiria kulazimishwa kushuka mbezi wakati basi linakuja mjini ni kulazimisha watu kuteseka bila sababu na kama kiongozi wa umma alipaswa kuwatazama abiria sio kama kipato cha mamantilie au machinga walijazana pale.

Sijui kwanini viongozi wetu wa sasa kila maamuzi wanayofanya yanawaumiza wananchi.Tumsihi mkuu wa mkoa kuupanga kwanza mji vizuri mbezi yenyewe haina hata accomodation za kutosha kwa abiria wanaoingia usiku sana.
 
kwa hiyo sasa yale mabasi ya abiria wa mikoa ya Lindi na mtwara sasa waje kushukia mbezi ili kutoa fursa kwa daladala.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…