Fundi Mchundo
Platinum Member
- Nov 9, 2007
- 10,448
- 8,705
Kama kuna fani inadharauliwa ni ya mipango miji. Wao wanaonekana kuwa kazi yao kubwa ni kugawa viwanja tu. Walitakiwa saa hizi wawe wanatayarisha mazingira ya mji utakavyokuwa miaka 50 ijayo. Mipango hiyo inatakiwa iwasilishwe kwa wananchi ili wachangie mawazo na mawazo yao yatiliwe maanani. Mipango inayotarishwa sasa hivi ni academic na baada ya kupokelewa inatupwa kabatini na wana siasa wanafanya wanavyotaka. Mfano ni Dodoma. Mpango Mji wa awali umesahaulika bila wananchi kupewa sababu za kuuacha.Mimi kinachonisikitisha ni kukosa viongozi wanaoweza kuja na plan za miaka angalau 50 mbele... mbona kina Mwalimu Nyerere waliweza kuweka mipango inayoishi hadi leo? Ukiangalia kituo cha Ubungo hakina miaka mingi tayari kimebomolewa. Hata hiyo ya Magufuli usishangae baada ya miaka mitano ikabomolewa na kuhamishwa tena. Kuhusu aliyoamrisha Makala ni upuuzi kama upuuzi mwingine. Sio lazima mabasi yarundikwe sehemu moja. Labda wangejenga stendi angalau nne jijini Dsm ili kwenda sawa na uhitaji. Hao mama ntilie wangetafutiwa utaratibu mzuri wa kuongeza thamani za biashara zao ingevutia hata wasafiri wasiopenda kula njiani kununua vyakula vyao. Huwezi kunilazimisha kula kwa mama ntilie ambaye uchafu ni mojawapo ya sifa ya yeye kuwa mama ntilie.
Amandla...