Ni sawa na uwanja wa ndege, ambako ukitaka kusafiri, kama unatokea Kawe, ni lazima utafute usafiri wa kukufikisha JKNIA, na hivyo hivyo, kama unaingia, utapata usafiri toka hapo kukupeleka Kawe.
Mimi naona la msingi zaidi ni Makala kuhakikisha sehemu zote za mji wake zipo huduma za kuwafikisha wananchi Stendi kuu ya mabasi, Mbezi Luis.
Lakini pia inabidi niulize swali hapa: kuna ubaya wowote kwa mfano kuwepo kwa vituo kadhaa vya mabasi mjini Dar, kwa mfano kituo cha mabasi yanayoelekea kusini mwa nchi kikawepo Mbagala; kituo cha mabasi yaendayo Nyanda za juu yakaanzia, tuseme Gongo La Mboto, n'k.?
Vipi, mbona hujachangamkia fursa ya Hotel/Guest maeneo hayo mkuu Erythrocyte!
Kufananisha Uwanja wa Ndege na Stendi ya Mabasi si busara hata kidogo....au Kufananisha Abiria wa Ndege na Basi nako si busara pia.
Hata kwa Abiria wa Treni utaona karibia asilimia 90 ya abiria, haswa wale wa daraja la chini(economic class) hulazimika kulala hapohapo Kituoni kungoja safari au kama wamefika husubiri kupamabazuke ndio waende wakatafute usafiri wa kwenda kwao.
Abiria anayemudu kusafiri kwa Ndege itakuwa ni ajabu kama atashindwa kulipia Taxi hata sh 50,000 kwenda au kutoka Airport.
Abiria wengi Wanaochagua usafiri wa Mabasi pia wapo wa makundi tofauti....wapo ambao wako tayari kulipa ziada ili tu kusafiri kwa amani na starehe (Luxury)...ila pia wapo wanalazimika kupanda basi lolote lile ali mradi wafike waendapo.
Maamuzi ya Mheshimiwa hayakujali yote hayo zaidi ya kutafuta tu njia ya mkato kuwafurahisha Wamachinga, Mamalishe au Watu fulani kama sio maslahi yake binafsi...na ukifuatilia utagundua yeye hajatumia huu usafiri kwa miaka 20 kama sio 30 iliyopita.
Abiria wengi wanaotumia Mabasi ya Luxury sidhani kama wanatumia chakula cha Mama Lishe, wengi wakishakula Mchana njiani (Korogwe/Mombo kwa watokao Kaskazini) hawatohitaji tena kula....huenda hilo nalo yeye hajui.
Au la Kama Mkuu ndio kaamau basi yale Mabasi ya Luxury yaruhusiwe kufika vituo vyao kwa tozo za ziada kama shida ni pesa ili Kampuni zifanikishe lengo lao la kuwahudumia Abiria wao wa daraja la Luxury....au hilo nalo hataki? kama hataki ana ajenda gani fiche huyu?
Option nyingine inayobaki ni kwa Wenye Mabasi kuandaa usafiri Mbadala wa Minibus kuwatoa na kuwapeleka Abiria wao wa Daraja la Luxury hapo stendi, ingawa kutakuwa tena na kero ya kuhamisha mizigo.
Mkuu atambue kama ambavyo yeye anavyopenda kusafiri kwa raha mustarehe basi wapo pia Wanachi Wenzake waliotayari kulipa ziada hata kwa kushinda njaa safari nzima ili tu wasafiri kwa amani na starehe bila ya kero.
Kwa wale Abiria wa madaraja ya kawaida a.k.a kajambanani ni bahati mbaya kwao kwani hiyo ndio njia pekee Kiongozi wenu kaona inawafaa kwa kushinikiza mkarundikane pale Kituoni na kina Wamachinga, Mamalishe, Wapagazi na Mikokoteni yao, Wapiga debe/Wakatisha tiketi n.k. kama sehemu ya kudumisha ujamaa.
Naomba nimkumbushe Mkuu kuwa Wapo Abiria hawapendi kupitia hayo yote....sasa je wao wafanyeje?.
Na kama Waziri husika naye ataridhia hili basi naye atakuwa na akili hizohizo za RC.