Napinga hoja ya RC Makalla ya kulazimisha Mabasi yote ya Mikoani kupakia na kushusha abiria Stendi ya Magufuli pekee

Napinga hoja ya RC Makalla ya kulazimisha Mabasi yote ya Mikoani kupakia na kushusha abiria Stendi ya Magufuli pekee

Hili jambo halina afya kabisa kwa wananchi wa kipato cha chini, Mama Samia anatakiwa kuingilia kati kuwanusuru watu wake, wanaotoa hayo matamko hawatumii usafiri wa public, hawaonji machungu wanayopata wwananchi wa kipato cha chini

Kwa nn wazo lisiwe wamiliki wa mabus wawe na coaster maalum za kuwasogeza abilia maeneo ya mjini na kuwapeleka stand asubuhi?
 
Nchi zilizoendelea zimeruhusu makampuni ya usafirishaji kuwa na pick points zao ili wateja wapate unafuu kusafiri,hapa kwetu ni kinyume chake, tumecentralize stand bila kuweka mifumo mizuri wezeshi ya kuwafikisha abiria hapo

Umewahi kufika dubai mkuu?
 
Ni kweli. Lakini hapa tunasema wewe unaongea vile ilipaswa kuwa, sivyo ilivyo. Makalla angekuwa sahihi kama angefanya utafiti na kutoa suluhisho lisilowaumiza wadau. Aweke miundombinu sahihi kati ya kituo hiki kikuu na maeneo ya jiji. Kwa mfano, mimi ningefurahi kama mwendokasi ingeungwa moja kwa moja pale kituoni. Mgeni unadrop na kuingia mwendo kasi. Kwa hali ilivyo sasa, pale kituoni ni adhabu wallahi. Ile kushuka mpka upate daladala, unajuta kuja Dar!
Unajua mkuu, mimi sipingi unayosema hata mara moja.
Msafiri anayefika mwisho wa safari yake, anatakiwa apokelewe vizuri kumalizia safari yake hadi sehemu anakofikia.

Kiungo hiki ni muhimu sana kwa mtu anayesafiri, kama ilivyo kwa yule anayeanza safari ndefu, anavyotakiwa kuwa na utulivu anapoanza safari yake.

Hakuna jibu rahisi hapa, kwa sababu tunajua ufinyu wa uwezo tulionao kwa sasa. Tungeweza kwa mfano kupendekeza pawepo na "shuttle Bus" toka maeneo mbalimbali ya mji yakichukua na kuleta wasafiri kituo kikuu cha mabasi Mbezi, lakini pamoja na uwezo wa watu binafsi kuifanya kazi hiyo, miundombinu ya barabara inaweza kuwa kikwazo kikubwa, na hata hapo Mbezi Luis penyewe hapakujengwa kukiwepo na mipango ya aina hiyo!

Taxi zipo? Bei ni kikwazo?

Mimi situpi lawama kwa Makalla, kwa sababu yeye sasa hivi hana uwezo wa kubadili chochote, bali kupiga siasa tu!
 
Siku zote huwezi kujenga Bar bila kuwashirikisha walevi hiyo stend wadau wa secta ya usafiri hawakushirikishwa ipasavyo

NB: Baada ya miaka 10 ijayo hiyo stand itafanya kazi vizuri kama wataboresha usafiri wa kufika sehwm husika
Nimekuelewa Sana!
Yaani badala ya kusolve tatizo tumeongeza tatizo juu ya matatizo!!
Sidhani kama hiyo stendi itaendelea kufanya kazi in the next 5 years.
 
Naungana nawe Mkuu, ukienda Tanga RATCO ana shuttle buses zinawatowa abiria ofisini kwake mpaka Kange, japo kuwa mara kadhaa wamekuwa wakikamatwa na police

Ukisafiri kutoka Iringa ofisi za ABC wana shuttle bus japo nauli inaongezeka kwa sh. 1,000, lakini utaratibu huo unawaondolea usumbufu abiria waliotoka safari ndefu wana mizigo mingi na watoto, wengine ni walemavu na wengine ni wagonjwa.
 
Amos Makalla ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na Mfadhili wa zamani wa bendi ya FM ACADEMIA ya Kinondoni, bila kufanya utafiti wowote ule leo ametoa amri ya kulazimisha mabasi yote ya mikoani kuanzia safari zao kwenye kituo kikuu cha mabasi ya mikoani cha Mbezi Luis, kinachoitwa kituo cha mabasi cha Magufuli na kushushia abiria wake hapohapo.

Lengo kuu la kauli yake hii ni kujaribu kukusanya watu ili kuneemesha wafanyabiashara waliojazana kwenye stendi hiyo bila mpangilio wowote, Makalla anaamini kwamba abiria wote wakishushwa ama kuanzia safari zao hapo basi watanunua bidhaa za wamachinga waliojazana hapo, hivi ndivyo akili yake ilivyomtuma, kwamba abiria wakomeshwe ili kufurahisha wafanyabiashara, amesahau kwamba abiria ni bora kuliko wamachinga kwenye mustakabhali wa Safari, hata hivyo sikubaliani naye.

Mbezi Luis eneo ilikojengwa Stendi ya Mabasi ya Mikoani ni nje kabisa ya jiji la DSM , kulazimisha Mabasi yaliyokuwa yanaanzia safari zake Mbagala, Tandika au Kigamboni kuacha kazi hiyo na kulazimisha sasa lazima yote yaanzie Nje ya jiji ni sawa na unyama , kwamba sasa aliyekuwa anapandia basi Mbagala akodi teksi kwa zaidi ya gharama ya tsh elfu 30 ili kulifuata basi Mbezi Luis, kwa vile tu Amos Makalla kajisikia hivyo haikubaliki na ni lazima ipingwe kwa nguvu zote.

Alichotakiwa kufanya Mh RC ni kuhakikisha kwamba basi lolote kutoka kwenye yard yoyote ile binafsi linakoanzia safari lisiondoke DSM bila ya kupita Stendi kuu ama lishushe litakako ila ni lazima lije stendi kuu, Vinginevyo Mh Makalla atamke hadharami Maslahi yake binafsi atakayopata kwa kuwatesa abiria wa Kigamboni, Vikindu , Chamanzi, Mbagala, Tandika na kwingineko waliokuwa wanapata ahueni ya kuanzia safari kwenye maeneo yao ya karibu.

Naomba kuwasilisha.

Gharama za kutoka nyumbani abiria anakotokea hadi Magufuli bus stand kuwahi gari inayoondoka saa 12 alfajiri zinaweza kuwa kubwa kuliko nauli yabkutoka dar kwenda Arusha
Hili ni la kufanyia kazi
 
Nimekuelewa Sana!
Yaani badala ya kusolve tatizo tumeongeza tatizo juu ya matatizo!!
Sidhani kama hiyo stendi itaendelea kufanya kazi in the next 5 years.
Five years kitakuwa bora zaid mkuu kumbuka stand ilivyo shift toka kisutu to ubungo
 
Siku zote huwezi kujenga Bar bila kuwashirikisha walevi hiyo stend wadau wa secta ya usafiri hawakushirikishwa ipasavyo

NB: Baada ya miaka 10 ijayo hiyo stand itafanya kazi vizuri kama wataboresha usafiri wa kufika sehwm husika
[emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122]
 
Amos Makalla ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na Mfadhili wa zamani wa bendi ya FM ACADEMIA ya Kinondoni, bila kufanya utafiti wowote ule leo ametoa amri ya kulazimisha mabasi yote ya mikoani kuanzia safari zao kwenye kituo kikuu cha mabasi ya mikoani cha Mbezi Luis, kinachoitwa kituo cha mabasi cha Magufuli na kushushia abiria wake hapohapo.

Lengo kuu la kauli yake hii ni kujaribu kukusanya watu ili kuneemesha wafanyabiashara waliojazana kwenye stendi hiyo bila mpangilio wowote, Makalla anaamini kwamba abiria wote wakishushwa ama kuanzia safari zao hapo basi watanunua bidhaa za wamachinga waliojazana hapo, hivi ndivyo akili yake ilivyomtuma, kwamba abiria wakomeshwe ili kufurahisha wafanyabiashara, amesahau kwamba abiria ni bora kuliko wamachinga kwenye mustakabhali wa Safari, hata hivyo sikubaliani naye.

Mbezi Luis eneo ilikojengwa Stendi ya Mabasi ya Mikoani ni nje kabisa ya jiji la DSM , kulazimisha Mabasi yaliyokuwa yanaanzia safari zake Mbagala, Tandika au Kigamboni kuacha kazi hiyo na kulazimisha sasa lazima yote yaanzie Nje ya jiji ni sawa na unyama , kwamba sasa aliyekuwa anapandia basi Mbagala akodi teksi kwa zaidi ya gharama ya tsh elfu 30 ili kulifuata basi Mbezi Luis, kwa vile tu Amos Makalla kajisikia hivyo haikubaliki na ni lazima ipingwe kwa nguvu zote.

Alichotakiwa kufanya Mh RC ni kuhakikisha kwamba basi lolote kutoka kwenye yard yoyote ile binafsi linakoanzia safari lisiondoke DSM bila ya kupita Stendi kuu ama lishushe litakako ila ni lazima lije stendi kuu, Vinginevyo Mh Makalla atamke hadharami Maslahi yake binafsi atakayopata kwa kuwatesa abiria wa Kigamboni, Vikindu , Chamanzi, Mbagala, Tandika na kwingineko waliokuwa wanapata ahueni ya kuanzia safari kwenye maeneo yao ya karibu.

Naomba kuwasilisha.
Mpuuzi huyu mkuu wa mkoa, yaani mie naenda moshi nakaa tegeta na nimekata tiketi ya dar express inapita mlango wa nyumbani kwangu niende mbezi??? Pumbavu!
Yaani mie nakaa shekilango nimetoka mbeya na ne force inashushia kituo cha mwisho parking yao mita 50 toka nyumbani kwangu eti nishuke mbezi..nyambafu!
Naenda tanga na tahmeed ila dar nakaa bunju gari zinapita hapa unaniambia niende nikaifuate mbezi...shit...
Waendelee kuupiga mwingi...
 
Aliyejenga hakujua hilo??
Gharama za kutoka nyumbani abiria anakotokea hadi Magufuli bus stand kuwahi gari inayoondoka saa 12 alfajiri zinaweza kuwa kubwa kuliko nauli yabkutoka dar kwenda Arusha
Hili ni la kufanyia kazi
 
Naunga mkono hoja. Baadhi ta wenye mabasi wenye stendi zao pale Sinza Shekilango kama Kilimanjaro, Dar Lux, Marangu Coach na mengine, wenye mabasi zaidi ya moja kwa route ya Moshi Arusha, njia rahisi kwao ni route ya Bagamoyo Msata, na sio njia ya Chalinze, kuwalazimisha lazima waanzie Stendi mpya ni kuwatesa tuu bure abiria, after all, wengi wa abiria wa mabasi hayo, haswa wale abiria wa 1st Class, sio wa type ya kununua vitu kwa machinga au kula kwa Mama Ntilie! Hivyo kama nia ni kuwasaidia Machinga na mama ntilie, then, hizo ni sababu alizotoa Mkuu wa Mkoa ni sababu za kijinga sana!.

Hatuwezi kuendelea kuendesha nchi kijinga jinga hivi halafu utegemee tutapata mafanikio. Il tuendelee , la kupata maendeleo ya kweli de must stop such nonsense!.

p
NB: sinza inaishia mto ng'ombe, ukivuka mto ng'ombe kuja barabara ya morogoro huko sio sinza ni shekilango, urafiki nk
 
Basi kama hutaki kulipa hizo gharama za kwenda stendi baki na [emoji90] yako nyumbani.
Jifunze kutumia akili basi[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Yaani hoja zako zimejaa aibu sana
 
Unajua mkuu, mimi sipingi unayosema hata mara moja.
Msafiri anayefika mwisho wa safari yake, anatakiwa apokelewe vizuri kumalizia safari yake hadi sehemu anakofikia.

Kiungo hiki ni muhimu sana kwa mtu anayesafiri, kama ilivyo kwa yule anayeanza safari ndefu, anavyotakiwa kuwa na utulivu anapoanza safari yake.

Hakuna jibu rahisi hapa, kwa sababu tunajua ufinyu wa uwezo tulionao kwa sasa. Tungeweza kwa mfano kupendekeza pawepo na "shuttle Bus" toka maeneo mbalimbali ya mji yakichukua na kuleta wasafiri kituo kikuu cha mabasi Mbezi, lakini pamoja na uwezo wa watu binafsi kuifanya kazi hiyo, miundombinu ya barabara inaweza kuwa kikwazo kikubwa, na hata hapo Mbezi Luis penyewe hapakujengwa kukiwepo na mipango ya aina hiyo!

Taxi zipo? Bei ni kikwazo?

Mimi situpi lawama kwa Makalla, kwa sababu yeye sasa hivi hana uwezo wa kubadili chochote, bali kupiga siasa tu!
Tunahitilafiana padogo tu. Huoni nilipokujibu nilianza na "Ni kweli"? Hii ni dhahiri ninakubaliana na hoja yako hasa ile ya kuhakikisha mabasi yanashusha na kupakia pale Mbezi. Maana ninaona changamoto ya kila basi kushusha holela. Tunapohitilafiana ni namna ya utekelezaji. Wewe unaona Makalla yupo sahihi kwa kauli yake. Mimi ninaona hayupo sahihi kwa sababu hajaweka mazingira rafiki katika hili. Wewe mwenyewe unaliona hili na umefafanua vema tu kuhusu mazingira ya stend na hali ya jiji kwa sasa. Angepigana kuboresha haya kisha akapiga hilo biti.

Kuhusu taxi,ni sawa. Lakini, watu wote wana uwezo wa taxi? Njia ziwepo nyingi, zote zikiwa zinaridhisha ili mtu afanye uchaguzi sahihi kulingana na kipato, muda na mahali anakokusudia kufika. Wengi tunaongelea usafiri wa wengi kama vile daladala na mwendokasi kutokana na kugusa kundi kubwa. Nimesafiri mara kadhaa, pale Mbezi bado hapajatulia. Ni vurugu tu.

Yaweza kuwa ni mtazamo wangu lakini, huenda kuna wengi mnaona mambo ni super! Nisikaze misuli ya shingo tu.
 
Ni sawa na uwanja wa ndege, ambako ukitaka kusafiri, kama unatokea Kawe, ni lazima utafute usafiri wa kukufikisha JKNIA, na hivyo hivyo, kama unaingia, utapata usafiri toka hapo kukupeleka Kawe.

Mimi naona la msingi zaidi ni Makala kuhakikisha sehemu zote za mji wake zipo huduma za kuwafikisha wananchi Stendi kuu ya mabasi, Mbezi Luis.

Lakini pia inabidi niulize swali hapa: kuna ubaya wowote kwa mfano kuwepo kwa vituo kadhaa vya mabasi mjini Dar, kwa mfano kituo cha mabasi yanayoelekea kusini mwa nchi kikawepo Mbagala; kituo cha mabasi yaendayo Nyanda za juu yakaanzia, tuseme Gongo La Mboto, n'k.?

Vipi, mbona hujachangamkia fursa ya Hotel/Guest maeneo hayo mkuu Erythrocyte!
Kufananisha Uwanja wa Ndege na Stendi ya Mabasi si busara hata kidogo....au Kufananisha Abiria wa Ndege na Basi nako si busara pia.

Hata kwa Abiria wa Treni utaona karibia asilimia 90 ya abiria, haswa wale wa daraja la chini(economic class) hulazimika kulala hapohapo Kituoni kungoja safari au kama wamefika husubiri kupamabazuke ndio waende wakatafute usafiri wa kwenda kwao.

Abiria anayemudu kusafiri kwa Ndege itakuwa ni ajabu kama atashindwa kulipia Taxi hata sh 50,000 kwenda au kutoka Airport.

Abiria wengi Wanaochagua usafiri wa Mabasi pia wapo wa makundi tofauti....wapo ambao wako tayari kulipa ziada ili tu kusafiri kwa amani na starehe (Luxury)...ila pia wapo wanalazimika kupanda basi lolote lile ali mradi wafike waendapo.

Maamuzi ya Mheshimiwa hayakujali yote hayo zaidi ya kutafuta tu njia ya mkato kuwafurahisha Wamachinga, Mamalishe au Watu fulani kama sio maslahi yake binafsi...na ukifuatilia utagundua yeye hajatumia huu usafiri kwa miaka 20 kama sio 30 iliyopita.

Abiria wengi wanaotumia Mabasi ya Luxury sidhani kama wanatumia chakula cha Mama Lishe, wengi wakishakula Mchana njiani (Korogwe/Mombo kwa watokao Kaskazini) hawatohitaji tena kula....huenda hilo nalo yeye hajui.

Au la Kama Mkuu ndio kaamau basi yale Mabasi ya Luxury yaruhusiwe kufika vituo vyao kwa tozo za ziada kama shida ni pesa ili Kampuni zifanikishe lengo lao la kuwahudumia Abiria wao wa daraja la Luxury....au hilo nalo hataki? kama hataki ana ajenda gani fiche huyu?

Option nyingine inayobaki ni kwa Wenye Mabasi kuandaa usafiri Mbadala wa Minibus kuwatoa na kuwapeleka Abiria wao wa Daraja la Luxury hapo stendi, ingawa kutakuwa tena na kero ya kuhamisha mizigo.

Mkuu atambue kama ambavyo yeye anavyopenda kusafiri kwa raha mustarehe basi wapo pia Wanachi Wenzake waliotayari kulipa ziada hata kwa kushinda njaa safari nzima ili tu wasafiri kwa amani na starehe bila ya kero.

Kwa wale Abiria wa madaraja ya kawaida a.k.a kajambanani ni bahati mbaya kwao kwani hiyo ndio njia pekee Kiongozi wenu kaona inawafaa kwa kushinikiza mkarundikane pale Kituoni na kina Wamachinga, Mamalishe, Wapagazi na Mikokoteni yao, Wapiga debe/Wakatisha tiketi n.k. kama sehemu ya kudumisha ujamaa.

Naomba nimkumbushe Mkuu kuwa Wapo Abiria hawapendi kupitia hayo yote....sasa je wao wafanyeje?.

Na kama Waziri husika naye ataridhia hili basi naye atakuwa na akili hizohizo za RC.
 
Back
Top Bottom