Napinga kabisa dhana ya "Mume ni Provider" katika ndoa

Haunitaki tena? Mbona nkua nshaanza kukupenda
 
Wanandoa punguzeni uchoyo, ubinafsi na uvivu muone kama hamjaishi kwa amani, ama lah mjiunge na Ney wa mitego.... kupanga ni kuchagua.

Hiki ulichoandika ndio maudhui ya andiko langu

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Ahudumiwe yeye ni mlemavu wa mwili au akili!! Kwa wazazi wake mwanamke alikuwa akilima, akichunga mbuzi, akienda mtoni kuteka maji, kuuza mazao yanayozalishwa,
 
Hii dhana inatumiwa kama kigezo cha kujustify ukahaba (prostitution) kwa waliolewa, utasikia "mume hanipi hela ndiyo maana najiuza" wenyewe wanaita kudanga au kula vichwa. Wakati tangu enzi za babu zetu wanawake walikuwa wakifanya kazi nyingi za kuzalisha na kukuza uchumi wa familia. Hii dhana ya wanawake kuhudumiwa kama watoto wachanga au walemavu wa akili au malkia wa mchwa, nia yake ni kuwafanya wanaume mabwege na kujistify prostitution tu. Kahaba ni kahaba tu hata umhudumie vipi, kuna wanawake waume matajiri wanawapa hela na huduma zote ila wanatumia hela hizo hizo kuhonga bodaboda na ving'asti (gigillos/Male prostitutes) wazini nao.
 
Yes, haya madini!
Na wazee zamani waliwachagulia vijana wa kiume mabinti wa kuwaoa!
Sifa kuu za binti Bora wa ndoa zamani zile ni heshima na bidii ya kazi,

Binti mvivu hakupata soko la kuolewa!

Wazazi wenye mabinti walijitahidi kuwafundisha heshima na bidii ya kazi ili binti auzike

Mwanamke ni mwajibikaji wa moja kwa moja wa familia yake

Hapa tutofautishe na mahusiano na kahaba ambapo Mwanaume anawajibika kugharamia kila kitu
Bahati mbaya mentality ya Mahusiano ya kikahaba yanaletwa kwenye ndoa!

Mwanamke awajibike vile alivyo

Kama Ni mama wa nyumbani atawajibika kwa kazi za msingi za ndani

Kama mfanya kazi au biashara, basi kipato chake kinapaswa kuja kuongeza nguvu ya familia
Siku hizi, waume wengi wanapambana kuwafungulia miradi wake zao. Yes, hio ni namna ya kumfanya mke awajibike katika kujenga familia.


Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Ahudumiwe yeye ni mlemavu wa mwili au akili!! Kwa wazazi wake mwanamke alikuwa akilima, akichunga mbuzi, akienda mtoni kuteka maji, kuuza mazao yanayozalishwa,
Kama hujui mantiki ya mume kumhudumia mkewe au mke kuitunza familia yake (akiwemo mumewe), kila mmoja akitekeleza wajibu wake, sidhani kama hata maana ya familia unaijua wewe.

Hakika bado tuna safari ndefu kama taifa, iwapo watu sampuli yako wangalipo.
 
Kuna 50/50 ya aina mbili.

Traditional 50/50

Mama anafanya kazi (akipenda, na hela ni ya matumizi anayotaka) na mara nyingi si kazi nzito, akili yake inakuwa kwenye kutunza mume na watoto watakaojaliwa huku mwanaume akihudumia familia kila kitu.

50/50 modern imbalanced (napenda kuiita 70/30)

Hii wote mnafanya kazi na kuleta hela nyumbani.
Ila mwanamke bado anafanya kazi ya kubeba mimba, kuzaa kwa uchungu, kulea, kupika na kulipia watoto Ada, kodi n.k (70%)

Mwanaume akichangia mbegu na pesa kwa jinsi awezavyo pekee (30%)

Wewe unataka 50/50 ipi?

Kwa mwanamke kubeba mimba na kuzaa, kisha kulea , tayari anaanza na 50% ya mchango wake kwa familia, hivyo ungependa aongeze ngapi kusaidia zaidi?
 
Babu yako ulimtoa kwenye kundi?
Baba yako ulimtoa kwenye kundi?
Hao wote si walisaidiana na wenza wao kujenga familia?

Mbona unakomment Kama Jambo nililoongea ni jipya machoni mwako?

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
1. Babu yangu was a real man, alikuwa na watoto 12 na alibeba majukumu ya kumtunza bibi na baba zangu na mashangazi. ndio maana na babangu kawa real man.

2. Babangu alikuwa real man, alikuwa na watoto 8, wote alitutunza na alibeba majukumu yote kama provider kwa mama na kwetu na akanisomesha pia.

3. Mimi ni real man, nina watoto 6, mke wangu namtunza na nafurahia ninavyokuwa provider, watoto pia. in reality, mke wangu akiwa na hela huwa sihesabu sana kama yetu, mimi ndiye provider hiyo ya kwake, najiona kidume zaidi anapotumia pesa zangu na mimi natafuta kwa bidii kwaajili yake na watoto.


4. wewe inawezekana sio real man, ndio maana unakwepa majukumu, unataka kulelewa na wanawake. Mwanaume halisi hayupo hivyo. badilika.
 
Wajinga ndio wanakomaa,Mimi mwanamke hawezi kuwa na pesa asitumie kwenye familia namtimua Bora nikae peke yangu
 
Wajinga ndio wanakomaa,Mimi mwanamke hawezi kuwa na pesa asitumie kwenye familia namtimua Bora nikae peke yangu
Wanakomaa wakati huo huo wanaona familia zote mtaani kwake zinavyopambana kwa umoja wa baba na mama!
Wanajisahaulisha jinsi neno golikipa lilivyotrend katika kuwadiscourage wanawake wasiojishughulisha katika kujenga familia

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…