Evelyn Salt
JF-Expert Member
- Jan 5, 2012
- 70,916
- 141,437
Bro ilibaki kidogo mpate shemegi/wifi kanikataa tenaMnafiki wewe! ππππ akiii nimecheka sana bro!
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Bro ilibaki kidogo mpate shemegi/wifi kanikataa tenaMnafiki wewe! ππππ akiii nimecheka sana bro!
Haunitaki tena? Mbona nkua nshaanza kukupendaNaona kila dalili kuwa ndoa yetu yataishia katika migogoro mizito,
Kwani umeshaanza vijineno vya kashfa!
Naona neno kushirikiana limekukwaza Evelyn Salt
Acha niendelee kutafuta anayeelewa umuhimu wake wa kushiriki kikamilifu katika kujenga familia ya pamoja
Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Ahudumiwe yeye ni mlemavu wa mwili au akili!! Kwa wazazi wake mwanamke alikuwa akilima, akichunga mbuzi, akienda mtoni kuteka maji, kuuza mazao yanayozalishwa,Kwa nini ukamtwae nyumbani mwa wazazi wake, kama huwezi ama hutaki kumtunza?
Kwao alikuwa anakula na kuvishwa vizuri hadi siku ulivyomtia maneno maneno yako ya ushawishi hadi akakubali kuishi na wewe.
Mwanaume anayekwepa majukumu yake, hana sifa za kuitwa mwanaume. Shame on you!
Aaah, mwanamke wa design yako hanifai!Haunitaki tena? Mbona nkua nshaanza kukupenda
Nimefanyaje tena jamani mbona ghafla
Yes, haya madini!Hii dhana inatumiwa kama kigezo cha kujustify ukahaba (prostitution) kwa waliolewa, utasikia "mume hanipi hela ndiyo maana najiuza" wenyewe wanaita kudanga au kula vichwa. Wakati tangu enzi za babu zetu wanawake walikuwa wakifanya kazi nyingi za kuzalisha na kukuza uchumi wa familia. Hii dhana ya wanawake kuhudumiwa kama watoto wachanga au walemavu wa akili au malkia wa mchwa, nia yake ni kuwafanya wanaume mabwege na kujistify prostitution tu. Kahaba ni kahaba tu hata umhudumie vipi, kuna wanawake waume matajiri wanawapa hela na huduma zote ila wanatumia hela hizo hizo kuhonga bodaboda na ving'asti (gigillos/Male prostitutes) wazini nao.
Kama hujui mantiki ya mume kumhudumia mkewe au mke kuitunza familia yake (akiwemo mumewe), kila mmoja akitekeleza wajibu wake, sidhani kama hata maana ya familia unaijua wewe.Ahudumiwe yeye ni mlemavu wa mwili au akili!! Kwa wazazi wake mwanamke alikuwa akilima, akichunga mbuzi, akienda mtoni kuteka maji, kuuza mazao yanayozalishwa,
Ndio maana unajiita weakman. Alisaidiwa ulikuwepo? Ma bachelor kibao wanamafanikio na hawajaoa. Usikariri.Baba Yako alisaidiwa kujenga familia na mama yako
1. Babu yangu was a real man, alikuwa na watoto 12 na alibeba majukumu ya kumtunza bibi na baba zangu na mashangazi. ndio maana na babangu kawa real man.Babu yako ulimtoa kwenye kundi?
Baba yako ulimtoa kwenye kundi?
Hao wote si walisaidiana na wenza wao kujenga familia?
Mbona unakomment Kama Jambo nililoongea ni jipya machoni mwako?
Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
umejuaje ππkama je anatania apoπππ huyu jamaa jau anazingua wifi
Ushaachiwa sasa umeanza vurugu πππumejuaje ππkama je anatania apo
shogha weeee niliishiwa bando ππnna mtoto mdogo uzinzi nmepumzka shooUshaachiwa sasa umeanza vurugu πππ
Wajinga ndio wanakomaa,Mimi mwanamke hawezi kuwa na pesa asitumie kwenye familia namtimua Bora nikae peke yanguNdio, napinga!,
Ni dhana ya uongo na inakiuka kabisa asili ya maisha ya ndoa!
Ndoa ni muunganiko wa mtu mume na mtu mke na kuzaa watoto kisha kuwatunza. Jumuia hii ya familia inahitaji mahitaji mbalimbali ya maisha kwa maendeleo yake.
Kuna watu wachache wanaibuka hapa bila hata chembe ya aibu na kutaka kuuaminisha umma kuwa mtu mume yampasa kutafuta mahitaji ya familia but mtu mke pamoja na watoto hawawajibiki.
Wanaume wanapolalamika kwamba wanawake kwenye ndoa wanapenda kuhudumiwa zaidi kuliko kuhudumia, wanaibuka watu hawa na vicomment vyao eti ni jukumu la mume kuprovide, na hiari ya mke kuprovide! Salaleee!
Najaribu kujiuliza hii dhana wanaitoa wapi? Ni taasisi gani imefundisha hivi? Au ni ubunifu katika fikra zao?
Katika Ukristo haipo sijui kule kwa wenzetu!
Kwa Wakristo ipo wazi;
"Zaeni mkaongezeke, mkaijaze dunia na kuimiliki"
Kauli ya Mungu kwa mume na mke ikiashiria ushirikiano wa pamoja katika kuijenga familia na dunia kwa ujumla.
"Si vema mwanaume awe pekeyake, nitamfanyia msaidizi wake"
Kauli ya Mungu ikiashiria matakwa yake ya mke kuwa msaidizi kwa mume. Then why mume awe provider bila kusaidiwa?
"Mume na mke watawaacha wazazi na kuungana na kuwa mwili mmoja"
Kauli ya Mwana wa Mungu ikiashiria ndoa ni mshikamano kwa raha na shida hadi kifo kiwatenganishe.
Then mshikamano gani huo wa mmoja kuprovide?
"Mwanamke amtii mumewe na mwanaume ampende mkewe"
Kauli ya mtume wa Mwana wa Mungu ikiashiria kuwa mwanamke awe tayari kutumika kwa hali na mali mbele ya mumewe.
Maisha halisi ya mwanadamu tangu kale yapo wazi. Mwanaume na mwanamke wamefanya kazi pamoja kwa ajili ya maisha yao.
Tangia enzi za Adam na Eva, enzi za manabii, enzi za Yesu Kristo, nyakati za mitume, nyakati za mwanzo za kanisa Katoliki, nyakati za mtume Mohammed hadi leo, mume na mke wameshirikiana katika kazi.
Wamelima pamoja, wamefuga pamoja.
Mume alivua samaki na mke aliwapika wakala,
Mume alitengeneza visu na mke alitengeneza vyungu na makapu wakauza na kupata riziki ya maisha yao.
Hayo yote yalifanyika kwa maelfu ya miaka iliyopita!
Vipi wewe leo kisa una kijikampuni chako unapata fedha, eti unaanza kuleta propaganda kuwa mahitaji ya familia ni jukumu la mume!
Ikumbukwe dunia imebadilika.
Kwa sasa uchumi hauna mwenyewe tena.
Mwanaume au mwanamke aweza kuhodhi uchumi mkubwa.
Leo hii mke aweza kuwa waziri au raisi na akapata mamilioni ya fedha.
Je, hayo mamilioni ya fedha apeleke wapi iwapo hapaswi kuprovide na kujenga familia yake?
Leo una mshahara mnono au kampuni inakupa fedha nyingi halafu unahisi unaweza kuhudumia familia kwa 100%, then unaanza kuwatukana waume wenzako kuwa hawatakiwi kushirikiana na mke katika kuhudumia familia.
What if mtu kama JPM anakufukuza kazi au anaifilisi kampuni yako, yule mke wako afisa maendeleo ya jamii pale Halmashauri asihudumie familia yenu?
Unajua wakati mwingine watu wakiwa na pesa, pesa zinawalevya na wanaongea vyovyote!
Hii dhana ya wanawake kupenda kuhudumiwa tu bila kuwajibika hata kama uwezo wanao ni dhana mpya! Na imejengwa na waume wenye fedha pale wanapowarubuni kwa kuwaambia, "We mtoto mzuri hautakiwi kupata shida, wakati mwanaume nipo kwa ajili yako, nitakuhudumia chochote utakacho!"
Kauli hizi zimewaharibu wanawake wengi sana.
Mabibi na mabibi zao tangu kale hawakujua huu ujinga. Wao walijua kuolewa ni kazi! Kuamka, kufanya usafi, kwenda kushirikiana na mume shambani, au malisho ya ng'ombe! Leo mwanamke anamshahara wake hataki utumike nyumbani!
Kwani kuna tofauti gani na bibi yetu aliyesuka kapu akauza na pesa ikatumika nyumbani?
Hivi nyie wanaume muliyewapotosha wanawake kwa dhana potofu ya mume ni provider, mumetumia msingi gani wa elimu?
Hapana, mume na mke wawajibike pamoja kuijenga familia. Mume ukiamua kuwa provider, na iwe kwa maamuzi yako, na usishinikize kuwa principle ya ndoa. Kwani maisha hayo si asili ya mwanadamu tangu kale. Labda kama unakusudia kuleta mapinduzi ya mfumo wa uwajibikaji katika ndoa!
Kuna sehemu nilisoma andiko la mwanamke akiwahoji wanaume kwanini awajibike kumtii mume wakati anasaidia kuprovide mahitaji ya ndani?
Swali hili ni sawa na kumhoji mkurugenzi kwanini umtii wakati unachangia maendeleo ya taasisi? Swali hili alitakiwa aliulize Eva kwa Mungu wake.
Bahati mbaya cheo hiki alishapewa mwanamume tayari. Ukimtii Mungu utatii na neno lake. Familia ni taasisi ambayo lazima awepo kiongozi wakuweka direction za maisha. Hata hivyo haulazimiki kutii chochote. Unapaswa kumtii mume kwa yote yaliyomema. Mungu alishafanya uteuzi, labda tusubiri utenguzi na ateuliwe mwanamke siku za usoni!
Mke wajibika kuprovide kwa familia yako pale inapowezekana. Usikwepe wajibu ilihali mukiachana unadai mgao hamsini kwa hamsini.
Mume akifa unadai urithi wa mali zote!
Hata hivyo, hapa, nikiri kwamba asilimia kubwa ya wanawake wanajitoa na kuprovide kwa familia zao. Asanteni sana!
Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Unaishiwaje bando na kaka mkubwa tajiri la kkoo Mpaji Mungu yupo?? πππshogha weeee niliishiwa bando ππnna mtoto mdogo uzinzi nmepumzka shoo
oooh kumbe wewe ni walewale ombaomba crewππUnaishiwaje bando na kaka mkubwa tajiri la kkoo Mpaji Mungu yupo?? πππ
Acha kutufhalilisha
Wanakomaa wakati huo huo wanaona familia zote mtaani kwake zinavyopambana kwa umoja wa baba na mama!Wajinga ndio wanakomaa,Mimi mwanamke hawezi kuwa na pesa asitumie kwenye familia namtimua Bora nikae peke yangu