Napinga kabisa dhana ya "Mume ni Provider" katika ndoa

Ndoa ni kichaka cha mwanamke kujitajirisha.... Kataaa
Kukataa ndoa ni kukwepa majukumu na wajibu wa msingi kama wanadamu, iwe mwanamke ama mwanaume.

Bila ndoa uwezekano wa kujenga familia na taifa imara na bora ni mdogo sana.

Familia ndiyo msingi na muhimili muhimu sana katika taifa. Mtu anayepinga ndoa, anapinga pia familia. Hao ni agents wa anarchy and chaos katika jamii yoyote ile.

Bila ndoa, mtoto atafaidikaje na upendo wa wazazi, ndugu, jamaa, marafiki na majirani - jambo ambalo ni muhimu sana kwa malezi, makuzi, maendeleo ya kijamii na kielimu kwa mtoto, na mafanikio yake hatimaye maishani?

Kwa ufupi, Chama cha Kataa Ndoa (CHAKANDO), kama lilivyo jina husika, ni chaka la visingizio na kukwepa uwajibikaji, huku wakikimbilia vitu vya kando.

Serikali iliangazie suala hili kwa jicho la tatu na tena kwa mawanda yote, na wanachama wake wote wakabiliwe na mkono wa sheria kwa kuihujumu nchi rasilimali watu bora, kwa namna moja au nyingine.

Chama cha Kataa Ndoa ni adui namba moja dhidi ya mustakabali bora wa taifa.
 
Umewahi kuwaza siku uki R.I.P unaacha familia ya aina Gani? Au unadhani unamkataba na Mungu wa kuishi milele? Jamaa Yuko Sahihi,hasa situation ambayo wote mnafanyakazi,na Mwanamke hawajibiki Kwa chochote,akiamini ni kazi ya mume.
 
Be a gentleman,achana na wamarekani 50/50 haipo
50/50 is real
Ilikuwepo tangu Karne nyingi zilizopita
Tatizo fedha inawafanya mfikiri kuwa 50/50 haikuwepo
Lakini ilikuwepo katika kulima pamoja na kuhudumia mifugo pamoja
 
Hahaaaaaa huo ndio ukweli dogo. Nina watoto 4, wa kwanza ni umri wako. Nina enjoy kwenye ndoa japo hujajibu, baba yako hakuwa lijali kumuoa mama yako?
Umechanganyikiwa ww nina miaka 57+ naongea kitu ninachokifahamu.
 
Umewahi kuwaza siku uki R.I.P unaacha familia ya aina Gani? Au unadhani unamkataba na Mungu wa kuishi milele? Jamaa Yuko Sahihi,hasa situation ambayo wote mnafanyakazi,na Mwanamke hawajibiki Kwa chochote,akiamini ni kazi ya mume.
Mnajidanganya sana kuwa ukifa familia yako haitaishi kama mama hafanyi kazi au kuwa na ajira rasmi. Je kabla hujakutana na huyo mkeo alikuwa anaishije?
 
Umeandika kwa hasira mkuu

Anyway understood
 
Uko Sahihi Kwa Hilo,asilimia mia,sikuwa na Hela ya kulipia Ada za Watoto,mpaka nakopa Kwa ndugu,kumbe mke ana Hela nyingi tu benki! Yuko lazi alipie ada watu Baki lakini sio Watoto wetu! Alaaniwe aliyefundisha ujinga huo wanawake.
Wanaume wengi Wana stress za Maisha na kufa mapema kwakuwa hawana Msaada toka Kwa anayepaswa kuwa Msaidizi.
 
🀣🀣🀣🀣🀣🀣🀣🀣
 
Mkuu umeongea kwa uchungu sana ila ukweli utabaki palepale NDOA NI UTAPELI
 
No matter what,a man is a man Wacha kuwa legelege iba pora wewe ndio Kichwa Cha family
Kuna vijana wanapenda maisha tulivu Tanzania hii isiyo na kichwa wala miguu yaani ikienda kama inarudi ikirudi kama inaenda,nani atakupa hayo maisha kama hujapambana jinsi natural inavyotaka?

Ujinga sana mtoto wa kiume kulia lia atunzwe na mkewe,siku mkewe maisha yatakuwa magumu ndani amshauri wakaoelewe wote akubali.
 
Acha uongo dogo. Hii ni Chai, kwa uandikacho hata 20's huna na kama una hiyo miaka badi ni yale mazee mahuni, mamaskini, malevi na mazee yasiyojitambua. πŸ˜€πŸ˜ƒπŸ˜„πŸ˜πŸ˜†
Huna akili! Nashang'aa sana unavyokazania suala la umaskn??! Unanijua? Au ndo ujinga umekujaa u ignorant fool.
 
Kwanini yeye afanywe kuwa special namna hiyo na sio mimi mwanaume?

Kwani mimi sinawaacha wazazi wangu?

Kuishi na sisi wanawake wanataka hata bila ushawishi wa maneno
 
Analeta pigo za ki rainbow
 
Hili suala nishaliongelea sana humu ndani. Ikiwa tupo kwenye ulimwengu wa 50/50 ambapo mwanamke kapewa uhuru na access zote za kujitafutia inakuaje mwanaume abebeshwe jukumu la kumuhudumia? Mwanamke kapewa ajira, ukishapewa ajira maana yake automatically unaondolewa kwenye kundi la watu tegemezi sasa kivipi mwanamke huyu bado anataka kuhudumiwa. Wanaume dhaifu wanaotegemea kuficha udhaifu wao kwa kutoa pesa na wadangaji wakaishia kuniambia "tafuta hela". Katika suala la mapenzi mimi kanuni yangu ni kwamba kama unajiuza taja bei twende lodge tukamalizane na kama unataka tuingie kwenye mahusiano ya kimapenzi basi kila mtu awajibike kuleta kitu mezani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…