Napinga kabisa dhana ya "Mume ni Provider" katika ndoa

Napinga kabisa dhana ya "Mume ni Provider" katika ndoa

Tuanzie hapo kwene WEAK MAN

we olewa tu hamna chochote tunaweza kukusikiliza
Zaidi ya 80% ya ndoa ulimwenguni zinaishi kulingana na nilichoongea,

Inshort sio jipya

Kuna wanaume wachache na wanawake wachache kwa hiari yao wameamua kuishi maisha ya " Only man to provide"

Sio shida ila wasitake kulazimisha kuwa ndio sheria ya ndoa!

Hawa ndio nawapinga hapa

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
MWANAUME UTAKULA KWA JASHO NA MWANAMKE UTAZAA KWA UCHUNGU.

basi zaa wewe kwa UCHUNGU, kuliko kuandika thread ndeeeeeeefu!
MAELEOZO MEENGI!
Eva mwenyewe alienda shamba kulima bega kwa bega na mumewe kipenzi Adam,

Wake wa manabii walilima na kuvuna mazao

Wala hakuna nabii aliyewaonya na kuwazuia

Na hata yule nabii hakuzaa kwa uchungu

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Zaidi ya 80% ya ndoa ulimwenguni zinaishi kulingana na nilichoongea,

Inshort sio jipya

Kuna wanaume wachache na wanawake wachache kwa hiari yao wameamua kuishi maisha ya " Only man to provide"

Sio shida ila wasitake kulazimisha kuwa ndio sheria ya ndoa!

Hawa ndio nawapinga hapa

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
we sema unataka kulelewa
Kumbuka kila jamii zinatamaduni zao
Sisi ni waafrica mwanaume ndo kichwaa

Sasa ww weak manmeanaume laini laini unaogopa majukumu
 
we sema unataka kulelewa
Kumbuka kila jamii zinatamaduni zao
Sisi ni waafrica mwanaume ndo kichwaa

Sasa ww weak manmeanaume laini laini unaogopa majukumu
Waafrika na duniani kote mume Ni kichwa,

Tangu zamani za kale, mume katika jamii za Afrika aliongoza familia yake kwa kulima, kufuga, kusuka na shughuli nyingi kwa kushirikiana na Mke na watoto

Leo tuna shughuli za viwandani, na ofisini wake kwa waume wenye ndoa zao wanashiriki kwa ajili ya kupata vipato vya kujenga familia zao

Ndoa zilizo nyingi zimejengwa kwa misingi ya ushirikiano wa baba na mama

Babu na bibi zetu walishirikiana

Baba na mama zetu wameshirikiana

Leo tunaozesha watoto wetu wanaenda kushirikiana

Ndoa za only man to provide zipo!

But nachopinga Ni chokochoko za kutaka kushinikiza kuwa only man to provide ndio msingi wa ndoa,

Ebu nikutafutie mwanamke wa haki sawa!!
Jitahidi uwe na sura sasa kwa sura hiyo afu udai haki sawa mkuu utakua unaachwa kila siku
 
Ni umaskini tu lakini wanaume walio "wengi" wanafurahia wanapokuwa na uwezo wa kuprovide kwaaajili ya familia zao fully.... wakishaga seti mipango na miundombinu yao vizuri nyumbani, popote wawapo utawaona Meno yote nje na confidence iko juu sana.

Kaka Weakman mwanaume ukimuondolea jukumu la kuprovide kwaajili ya familia yake anakuwa hana tofauti na Ashura, Mwajuma au Ceci... na hii haimaanishi mke hela yake akaigawe au akaichezee wapi huko.... maana yake hela ya mke ni hela ya mumewe indirect, akiitaka aipate ndio maana ya usaidizi.

Wanandoa punguzeni uchoyo, ubinafsi na uvivu muone kama hamjaishi kwa amani, ama lah mjiunge na Ney wa mitego.... kupanga ni kuchagua.
 
Ndio, napinga!,

Ni dhana ya uongo na inakiuka kabisa asili ya maisha ya ndoa!

Ndoa ni muunganiko wa mtu mume na mtu mke na kuzaa watoto kisha kuwatunza. Jumuia hii ya familia inahitaji mahitaji mbalimbali ya maisha kwa maendeleo yake.

Kuna watu wachache wanaibuka hapa bila hata chembe ya aibu na kutaka kuuaminisha umma kuwa mtu mume yampasa kutafuta mahitaji ya familia but mtu mke pamoja na watoto hawawajibiki.

Wanaume wanapolalamika kwamba wanawake kwenye ndoa wanapenda kuhudumiwa zaidi kuliko kuhudumia, wanaibuka watu hawa na vicomment vyao eti ni jukumu la mume kuprovide, na hiari ya mke kuprovide! Salaleee!

Najaribu kujiuliza hii dhana wanaitoa wapi? Ni taasisi gani imefundisha hivi? Au ni ubunifu katika fikra zao?

Katika Ukristo haipo sijui kule kwa wenzetu!

Kwa Wakristo ipo wazi;

"Zaeni mkaongezeke, mkaijaze dunia na kuimiliki"

Kauli ya Mungu kwa mume na mke ikiashiria ushirikiano wa pamoja katika kuijenga familia na dunia kwa ujumla.

"Si vema mwanaume awe pekeyake, nitamfanyia msaidizi wake"

Kauli ya Mungu ikiashiria matakwa yake ya mke kuwa msaidizi kwa mume. Then why mume awe provider bila kusaidiwa?

"Mume na mke watawaacha wazazi na kuungana na kuwa mwili mmoja"

Kauli ya Mwana wa Mungu ikiashiria ndoa ni mshikamano kwa raha na shida hadi kifo kiwatenganishe.

Then mshikamano gani huo wa mmoja kuprovide?

"Mwanamke amtii mumewe na mwanaume ampende mkewe"

Kauli ya mtume wa Mwana wa Mungu ikiashiria kuwa mwanamke awe tayari kutumika kwa hali na mali mbele ya mumewe.

Maisha halisi ya mwanadamu tangu kale yapo wazi. Mwanaume na mwanamke wamefanya kazi pamoja kwa ajili ya maisha yao.

Tangia enzi za Adam na Eva, enzi za manabii, enzi za Yesu Kristo, nyakati za mitume, nyakati za mwanzo za kanisa Katoliki, nyakati za mtume Mohammed hadi leo, mume na mke wameshirikiana katika kazi.

Wamelima pamoja, wamefuga pamoja.

Mume alivua samaki na mke aliwapika wakala,

Mume alitengeneza visu na mke alitengeneza vyungu na makapu wakauza na kupata riziki ya maisha yao.

Hayo yote yalifanyika kwa maelfu ya miaka iliyopita!

Vipi wewe leo kisa una kijikampuni chako unapata fedha, eti unaanza kuleta propaganda kuwa mahitaji ya familia ni jukumu la mume!

Ikumbukwe dunia imebadilika.

Kwa sasa uchumi hauna mwenyewe tena.

Mwanaume au mwanamke aweza kuhodhi uchumi mkubwa.

Leo hii mke aweza kuwa waziri au raisi na akapata mamilioni ya fedha.

Je, hayo mamilioni ya fedha apeleke wapi iwapo hapaswi kuprovide na kujenga familia yake?

Leo una mshahara mnono au kampuni inakupa fedha nyingi halafu unahisi unaweza kuhudumia familia kwa 100%, then unaanza kuwatukana waume wenzako kuwa hawatakiwi kushirikiana na mke katika kuhudumia familia.

What if mtu kama JPM anakufukuza kazi au anaifilisi kampuni yako, yule mke wako afisa maendeleo ya jamii pale Halmashauri asihudumie familia yenu?

Unajua wakati mwingine watu wakiwa na pesa, pesa zinawalevya na wanaongea vyovyote!

Hii dhana ya wanawake kupenda kuhudumiwa tu bila kuwajibika hata kama uwezo wanao ni dhana mpya! Na imejengwa na waume wenye fedha pale wanapowarubuni kwa kuwaambia, "We mtoto mzuri hautakiwi kupata shida, wakati mwanaume nipo kwa ajili yako, nitakuhudumia chochote utakacho!"

Kauli hizi zimewaharibu wanawake wengi sana.

Mabibi na mabibi zao tangu kale hawakujua huu ujinga. Wao walijua kuolewa ni kazi! Kuamka, kufanya usafi, kwenda kushirikiana na mume shambani, au malisho ya ng'ombe! Leo mwanamke anamshahara wake hataki utumike nyumbani!

Kwani kuna tofauti gani na bibi yetu aliyesuka kapu akauza na pesa ikatumika nyumbani?

Hivi nyie wanaume muliyewapotosha wanawake kwa dhana potofu ya mume ni provider, mumetumia msingi gani wa elimu?

Hapana, mume na mke wawajibike pamoja kuijenga familia. Mume ukiamua kuwa provider, na iwe kwa maamuzi yako, na usishinikize kuwa principle ya ndoa. Kwani maisha hayo si asili ya mwanadamu tangu kale. Labda kama unakusudia kuleta mapinduzi ya mfumo wa uwajibikaji katika ndoa!

Kuna sehemu nilisoma andiko la mwanamke akiwahoji wanaume kwanini awajibike kumtii mume wakati anasaidia kuprovide mahitaji ya ndani?

Swali hili ni sawa na kumhoji mkurugenzi kwanini umtii wakati unachangia maendeleo ya taasisi? Swali hili alitakiwa aliulize Eva kwa Mungu wake.

Bahati mbaya cheo hiki alishapewa mwanamume tayari. Ukimtii Mungu utatii na neno lake. Familia ni taasisi ambayo lazima awepo kiongozi wakuweka direction za maisha. Hata hivyo haulazimiki kutii chochote. Unapaswa kumtii mume kwa yote yaliyomema. Mungu alishafanya uteuzi, labda tusubiri utenguzi na ateuliwe mwanamke siku za usoni!

Mke wajibika kuprovide kwa familia yako pale inapowezekana. Usikwepe wajibu ilihali mukiachana unadai mgao hamsini kwa hamsini.

Mume akifa unadai urithi wa mali zote!

Hata hivyo, hapa, nikiri kwamba asilimia kubwa ya wanawake wanajitoa na kuprovide kwa familia zao. Asanteni sana!

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
hata kuku, jogoo huwa anaprovide kwa tetea na anamlinda, wewe kama ni mwanaume unapenda usiprovide unataka tukutoe kwenye kundi?
 
Kama aliyeandika uzi ni mwanaume basi asubiri kura ila kama ni mwanamke imepita bila kupingwa
 
Kiufupi mtoa mada sio muwajibikaji ndio maana anaogopa ndoa na Mwanaume kama hujaoa wewe ni muhuni tu. Ndoa ni kipimo cha Uanaume
 
Usijali, hadi boxa zako ni jukumu langu my.
Naona kila dalili kuwa ndoa yetu yataishia katika migogoro mizito,

Kwani umeshaanza vijineno vya kashfa!

Naona neno kushirikiana limekukwaza Evelyn Salt

Acha niendelee kutafuta anayeelewa umuhimu wake wa kushiriki kikamilifu katika kujenga familia ya pamoja

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Kiufupi mtoa mada sio muwajibikaji ndio maana anaogopa ndoa na Mwanaume kama hujaoa wewe ni muhuni tu. Ndoa ni kipimo cha Uanaume
Bro, Babu yako hakuwa muajibikaji?
Baba yako hakuwa muajibikaji?
Hao wote si walisaidiana na wenza wao kujenga familia?

Mbona unakomment Kama Jambo nililoongea ni jipya machoni mwako?

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
hata kuku, jogoo huwa anaprovide kwa tetea na anamlinda, wewe kama ni mwanaume unapenda usiprovide unataka tukutoe kwenye kundi?
Babu yako ulimtoa kwenye kundi?
Baba yako ulimtoa kwenye kundi?
Hao wote si walisaidiana na wenza wao kujenga familia?

Mbona unakomment Kama Jambo nililoongea ni jipya machoni mwako?

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom