Napinga Masheikh sita wa Kiislamu kupewa adhabu ya kunyongwa hadi kufa

Unahisi hukumu imekosewa?Nimejaribu tafuta logic yako bado nimetoka kapa ni kheri ungetulia tu maana hasa umeandika kwa emotions
There are so many angles in legal arguments to distinguish between the act of murder, and voluntary manslaughter (i.e loss of control and/or diminished responsibility).

Hukumu ya kifo sio jambo rahisi kwenye murder case katika mazingira mengine. But then I am not interested in the legal arguments in this case anymore; my prejudice has taken over (doesn’t mean I am right legally).

Mradi kuna watu walifariki, someone has to pay for their demise in my books (it’s a bias reasoning, nothing to do with legal arguments).

Baada ya kusoma hiyo hukumu, ignore what I wrote first. Mradi kuna maiti; kwa wahusika someone has to pay for the unnecessary loss of lives. Who is guilty depends on the quality of their defence lawyers (personally I don’t care).

Morally sina huruma na watu wanaochukua maisha ya watu bila ya sababu, kisa misimamo ya itikadi zao.
 
Nimepita pale mahakamani jana nikamuona yule mama Analia,nikauliza,"Huyu analia nini?". Najua jambo kama lile siyo
Mashekhe ndio wanafanya ugaidi?! Waumini wa dini hii wajitafakari sana!
 
Huu ni Ugaidi na haupaswi kuchekewa, utaota mizizi na kusababisha taabu siku za usoni.

Kulipua Bomu kwenye Mkusanyiko wa watu wasio na hatia ni vitendo vya kigaidi na vinatakiwa kupewa adhabu kali sana ili liwe funzo kwa wengine.
 
Hii ni fundisho kwa magaidi hapa nchini .
 
Naanza kuhisi hata kuunguzwa kwa shule za Shauritanga vilikuwa ni vitendo vya Kigaidi kama hivi ila havikustukiwa.
Maana hata wahusika wake hawajakamatwa hadi hii leo.

Sisi sote tupo hapa duniani kwa ridhaa ya Mungu mmoja.
 
Kwanza adhabu iliyofaa kwa hawa magaidi ilikuwa ni kuwapiga risasi hadharani! Wasubiri msahama kutoka kwa ndugu yao!
Magaidi sio wa kuonea huruma au kuwapeleka mahakamani ni kuwachapa shaba on the spot!
 
Kwanini usije na hoja yako ya: kuwafufua baada kunyongwa hadi kufa kuliko huu utopolo uliokuja nao?
 
Hiyo ni hukumu tuu kuna nafasi ya rufaa na rufaa ikidunda kuna nafasi ya msamaha wa raisi hapo baadae ama kubadilishiwa hukumu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pia nchi ingekuwa inaongozwa kwa sheria za kiislamu na hao masheikh ni viongozi wa kikristo wamechoma msikiti dunia ingekuwa imeshawasahau

Siupendi uislamu kwa sababu hiyo tu
Wanajihesabia haki sana
 
Unamaanisha nini ukisema mtu kuhukumiwa kifo bila maiti?

Tukio lilipotokea walikuwepo marehemu eneo la tukio, polisi wakathibitisha, wewe ulitaka maiti zikabebwe mochwari zipelekwe mahakamani kama ushahidi?

Kwamba ndugu wa marehemu wazuiwe kuzika ndugu zao wakisubiri ushahidi ukatolewe mahakamani?

Hujui hata kuna imani za wengine zinawataka kuwahifadhi marehemu wao ndani ya muda mfupi toka walipofariki?

Ajabu unaiuliza mahakama kama ipo serious!, mimi nakuona wewe ndie haupo serious, umekurupuka kutupa lawama kwa mahakama bila sababu zozote za msingi.

Ajabu zaidi unakiri hao jamaa wanastahili adhabu kali morally, lakini hutaki kukubali pia kama wanastahili adhabu kali kisheria kutokana na uhuni waliofanya.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Mie naamini Kuna watu au nchi wanapenda sana kudhamini ugaidi wa namna hii, Kuna nchi kama Iran na Qatar hizi nchi ni hatari sana. Kuna funds wanatuma Kwa baadhi ya waislam wanaoishi nchini Ili kuwatafuta vijana wa Kiislam wasio na ajira Kwa kuwapa fedha Ili watekeleze unyama huo Kwa mgongo wa Uislam.
Ukiua Kwa upanga utakufa Kwa upanga.Mie naona hiyo hukumu ni sahihi maana Kuna watu walikufa na ndugu zao walitoa machozi,hivyo na yule mama kulia ni sahihi tumfananishe na waliokufa Kwa kupigwa mabomu.
Mie naona walicheleweshwa sana,walitakiwa wahukumiwe mapema sana na nashukuru mahakama Kwa kutimiza wajibu wake kikamilifu.
 
Katika shambulio hilo la bomu waliua mwanamke mmoja hapo hapo. Bomb lilimlipukia mgongoni. Alikuwa ni mwanakwaya na kama lisinge ingia kwenye joho lake bomu lineuwa wengi sana. Na kibaya zaidi aliyetumwa kurusha bomu ni mtoto na alithibitiwa na waumini. Bomu lile lillirushwa katikati ya mkusanyiko liliuwa na kuwapa waamini vilema vya Maisha. Ile ni kesi tu ya mauaji wala si tu ugaidi. Tena washukuru hawajakuta sheria mpya ya ugaidi wa kimataifa. Wasingefika mahakamani wangeishia vituo vya police kwenda Motuary.
Kama kawaida kusamehe ni Moja nguzo ya Ukristo. Pia kufa kanisani kwa dhuruma ya imani ni utakatifu. Hilo jambo lilibakia Mahakamani serikalini.

Ugaidi haubadilishi chochote Duniani unabadilisha watu kuwa maiti tu. Ungekuwa unalipa basi Osama bin laden angekuwepo anamalizia Uzee wake.
 
Wacha mahakama ifamye kazi yake.

Pale wapo Mahakimu wenye weledi na hakuna uonevu wa kidini kwasababu Hakimu aliyetoa hukumu mwenyewe ni MUISLAM

UGAIDI ni hatari kwa maisha yetu sote sio Wakristo tu ila kwa wote

Usitake ionekane kama Uislam ndio unatetea Ugaidi, unachafua Dini ya Hakhi
 
Kuna wakati nilikuwa nikidhani watumiaji wa JamiiForums wote wana akili sana, mpaka nilipoanza kuwagawa kutokana na michango yao.
 
Kama hujaridhika kawakatie rufaa, huku jf inapoteza mda wako, hutasaidiwa
 
Huu ni Ugaidi na haupaswi kuchekewa, utaota mizizi na kusababisha taabu siku za usoni.

Kulipua Bomu kwenye Mkusanyiko wa watu wasio na hatia ni vitendo vya kigaidi na vinatakiwa kupewa adhabu kali sana ili liwe funzo kwa wengine.

Magaidi siyo watu wa kuchekewa. Hao magaidi, kunyongwa hadi kufa ni adhabu halali kabisa kwa uovu wao.

Jitu linaandaa na kisha linatekeleza uovu wake kwa kurusha bomu kwenye kundi la watu, hilo jitu kweli ni la kuonewa huruma?

Vyombo vya usalama viendelee na uchunguzi. Huenda bado kuna mabaki. Mleta mada anaweza kuwa miongoni. Mtu mwema kabisa huwezi kumwonea huruma gaidi linalotumia mwavuli wa dini ya Kiislam.
 
Kwa hiyo ni sawa kulipua Kanisa na kuua watu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…