Napingana na Tundu Lissu kuwa ugumu wa maisha umesababishwa na Katiba

Katiba inamsababishia mwananchi ugumu wa maisha moja kwa moja au sio moja kwa moja kutokana na utekelezaji wa sera na uwajibikaji na uwajibishwaji wa watawala na watunga sera kwa mujibu wa sheria iliyotokana na katiba ambayo ni sheria mama......
 
Wa kurudi kwao ni huyo
Lissu asije kutuchafulia amani ya nchi yetu hapa. Yani mtu anahangaika na wazungu kutwa, wanae kawaacha nje kaja kuwasomba wapumbavu hapa. Na nyie mnaingia kingi.

Kwa hiyo we unaamini lissu anauchungu na hili taifa? Pathetic
Unataka aende wapi acha ubaguzi wa kijinga wewe
 
Ishu sio katiba mpya tu, ishu ni usimamizi wa hio katiba. Mambo yakiendelea kama yalivyo hata zikija version mpya za katiba kila mwaka hatufiki popote.

Katiba iwe inasimamiwa na vyombo vya dola atakaekiuka anakula umeme chap.
Mkuu ukitoka mifano uangalia muktadha wa Africa, hivi Tanzania ukiweka katiba inayompa Rais mamlaka kama huyo wa China unadhani ufisadi utakuaje?

Kenya walau iwe mfano kidogo, najua ufisadi au umasikini haujaisha ila uwajikibaji walau umeongezeka. Umeona 80% ya wabunge na magavana hawakuchaguliwa tena!! bajeti na sera mbovu huwa zinapingwa mahakamani tofauti na hapa hata tukiona tozo zinatuumiza hatuna pa kufungulia kesi.

So tujifunze kwa jirani zetu au sauzi tuache mifano ya china sijui Saudi Arabia maana muktadha ni tofauti sana.
 
Inaonesha dhahiri waTanzania Wana uelewa mdogo sana juu ya masuala mbali mbali yanayohusu katiba......

Kama mwananchi hajui namna Gani au madhara ya katiba mbovu yanavyomgusa basi tuna wananchi wenye mitazamo ya mifano ya mbuzi wanaofugwa........

Ndio maana serikali inazidi kufifisha ubora wa elimu utawala wao uendelee.......

Ndio maana wananchi wanaamini kila wanachofanyiwa na serikali ni hisani na sio uwajibikaji
 
Swali lako namba 2 Lisu alijibu kwenye hotuba yake, kasikilize
 
Magazeti ya leo yamemnukuu Tundu Lissu akisema ugumu wa maisha hautokani na uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan bali ni unatokana na Katiba.

1. Lissu nakuuliza Kwani Katiba ndio imefungua mipaka ya nchi yetu na kuruhusu Wakenya,Wanyarwanda,Wakongomani na Warundi kumiminika hadi mashambani huko vijijini kulangua mazao? hali ilikuwaje miaka ya Magufuli?

2. Katiba ndio imeweka Tozo za miamala ya kibenki na mitandao ya simu? hali ilikuwaje miaka mitano ya Magufuli?

3. Je! Katiba ndio imesababisha wakulima kukosa mbolea na kusababisha kushuka kwa uzalishaji wa mazao?

4. Katiba ndio imesababisha umeme ukatike mara kwa mara na kusababisha uzalishaji viwandani kushuka na kupandisha bei za bidhaa?

Katiba mpya ni hitaji muhimu lakini kuna matatizo hayasababishwi na Katiba na wewe umekwepa kusema waliotufikisha hapa kwa sababu unazozijua wewe na kusingizia Katiba.

Miaka 5 ya Magufuli tulikuwa tunatumia Katiba gani wakati mchele ukiuzwa 900 hadi 1,200 na sasa tunatumia Katiba gani mchele ukiuzwa 4,000
Unapokosa check and balance kwenye mfumo.wa katiba ,automaticaly utasababisha matatizo kwa raia .
Ndo lissu alilpojikita hapo!
Hayo matatizo yoote uliyoorodhesha yanatokana na viongozi wabovu ambapo kwa katiba yetu si rahisi kuwagusa
 
Kwa wachumba zake anako isemeleaga Tanzania. Baba zima linaisemelea nchi yake twitter ndo mnategemea aje awe rais. Si wataongoza wazungu
Magufuri hakumtaka hata kifdogo lakini kafa kibudu pia na wewe humtaki kumbuka korona ipo hata mafua ya ndege yapo,kumbuka Lisu ni chaguo la Mungu kwa sababu anatetea wananchi wazalendo na siyo wezi.
 
Inaonesha dhahiri waTanzania Wana uelewa mdogo sana juu ya masuala mbali mbali yanayohusu katiba......

Kama mwananchi hajui namna Gani au madhara ya katiba mbovu yanavyomgusa basi tuna wananchi wenye mitazamo ya mifano ya mbuzi wanaofugwa........

Ndio maana serikali inazidi kufifisha ubora wa elimu utawala wao uendelee.......

Ndio maana wananchi wanaamini kila wanachofanyiwa na serikali ni hisani na sio uwajibikaji
Inasikitisha sana mkuu, imagine mtu anaongelea shida ya umeme ilhali anajua kabisa top wa hiyo wizara hagusiki , kwa sababu ya katiba mbovu!
 
Magazeti ya leo yamemnukuu Tundu Lissu akisema ugumu wa maisha hautokani na uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan bali ni unatokana na Katiba.

1. Lissu nakuuliza Kwani Katiba ndio imefungua mipaka ya nchi yetu na kuruhusu Wakenya,Wanyarwanda,Wakongomani na Warundi kumiminika hadi mashambani huko vijijini kulangua mazao? hali ilikuwaje miaka ya Magufuli?

2. Katiba ndio imeweka Tozo za miamala ya kibenki na mitandao ya simu? hali ilikuwaje miaka mitano ya Magufuli?

3. Je! Katiba ndio imesababisha wakulima kukosa mbolea na kusababisha kushuka kwa uzalishaji wa mazao?

4. Katiba ndio imesababisha umeme ukatike mara kwa mara na kusababisha uzalishaji viwandani kushuka na kupandisha bei za bidhaa?

Katiba mpya ni hitaji muhimu lakini kuna matatizo hayasababishwi na Katiba na wewe umekwepa kusema waliotufikisha hapa kwa sababu unazozijua wewe na kusingizia Katiba.

Miaka 5 ya Magufuli tulikuwa tunatumia Katiba gani wakati mchele ukiuzwa 900 hadi 1,200 na sasa tunatumia Katiba gani mchele ukiuzwa 4,000
Tundu lissu ni jinga lenye kujiamini sana. Nasema jinga kwa sababu licha ya ujuzi wake wa sheria na ujanja mkubwa kwenya kuzitafsiri sheria kwenye siasa ni bomu kubwa. Huwezi kuleta ujanjaujanja wa kiwakili kwenye siasa.
Ni vema kujihadhari sana na huyu mtu wakati tunarekebisha katiba.
Dhana yake kwamba rais ana madaraka makubwa mno inabidi kuiendea kwa tahadhari. Fisadi wapigaji na wanyonyaji kwenye jamii kwa kawaida wanapendelea utawala legelege uliyojaa malumbano na hakuna uamuzi thabiti unachukuliwa.
Tutofautishe madaraka ya rais na jinsi rais anayatumia.
Wanajidai kuleta uongo eti magufuli alitumia ubabe tu kufanya maamuzi wakati kila uamuzi ulikua wa kisheria na uamuzi ulikua kwa manufaa ya umma wa wananchi
 
Wakenya Wana katiba mpya
Je imerahisisha maisha yao?
Its a long process, wakenya wanaweza wasiwe na maisha mazuri leo , ila wapo kwenye right track.
Uhuru kenyatta alikuwa na interest kwwnye uchaguzi uliopita lakini katiba haikumpa favour ya alichotaka kufanya,
Hii pekee ni world class standard in democracy.
 
Hii imenikumbuaha Wakati Prof. Wangari Mathai ameanzisha vuguvugu la kutunza mazingira. Kiongozi mmoja anauliza, eti mwanamama mmoja anasema mvua inatoka kwenye miti wakati mvua inatoka mawinguni.

Unahutaji kuwa smart to grasp the concept of causation.
 
Umeeleza vizuri sana,ila sijui kama atakuelewa
Hawezi kueleweka kwa sababu kama wengi kama yeye anafikiri katiba ni jibu la kila kitu.
Katiba ni mwongozo na msingi mkuu wa sheria za nchi. Mara nyingi kitu watu wanalalamikia ni sheria na taratibu wala sio katiba. Kwa hivyo ya kurekebishwa huenda ni sheria na pengine taratibu tu zilizowekwa chini ya dheria husika.
 
ipo siku watalalamika kuwa hata ndoa kuvunjika kunasababishwa na kukosekana katiba mpya
 
Magufuri hakumtaka hata kifdogo lakini kafa kibudu pia na wewe humtaki kumbuka korona ipo hata mafua ya ndege yapo,kumbuka Lisu ni chaguo la Mungu kwa sababu anatetea wananchi wazalendo na siyo wezi.
Kwakuwa yeye ni mwanadamu mkamilifu au sio. Ndo maana akafika nchi za nje na kuanza kumchamba marehemu. Sawa
 
Magazeti ya leo yamemnukuu Tundu Lissu akisema ugumu wa maisha hautokani na uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan bali ni unatokana na Katiba.

1. Lissu nakuuliza Kwani Katiba ndio imefungua mipaka ya nchi yetu na kuruhusu Wakenya,Wanyarwanda,Wakongomani na Warundi kumiminika hadi mashambani huko vijijini kulangua mazao? hali ilikuwaje miaka ya Magufuli?

2. Katiba ndio imeweka Tozo za miamala ya kibenki na mitandao ya simu? hali ilikuwaje miaka mitano ya Magufuli?

3. Je! Katiba ndio imesababisha wakulima kukosa mbolea na kusababisha kushuka kwa uzalishaji wa mazao?

4. Katiba ndio imesababisha umeme ukatike mara kwa mara na kusababisha uzalishaji viwandani kushuka na kupandisha bei za bidhaa?

Katiba mpya ni hitaji muhimu lakini kuna matatizo hayasababishwi na Katiba na wewe umekwepa kusema waliotufikisha hapa kwa sababu unazozijua wewe na kusingizia Katiba.

Miaka 5 ya Magufuli tulikuwa tunatumia Katiba gani wakati mchele ukiuzwa 900 hadi 1,200 na sasa tunatumia Katiba gani mchele ukiuzwa 4,000
Sasa wewe kwa kabichwa kako hako ka gb 1 utaweza kweli kuelewa hoja za Lissu?
 
Mkuu ukitoka mifano uangalia muktadha wa Africa, hivi Tanzania ukiweka katiba inayompa Rais mamlaka kama huyo wa China unadhani ufisadi utakuaje?

Kenya walau iwe mfano kidogo, najua ufisadi au umasikini haujaisha ila uwajikibaji walau umeongezeka. Umeona 80% ya wabunge na magavana hawakuchaguliwa tena!! bajeti na sera mbovu huwa zinapingwa mahakamani tofauti na hapa hata tukiona tozo zinatuumiza hatuna pa kufungulia kesi.

So tujifunze kwa jirani zetu au sauzi tuache mifano ya china sijui Saudi Arabia maana muktadha ni tofauti sana.
Utafungua kesi wakuangalie tu, si jalada la kesi itazungushwa na unaweza ukapandikiziwa bangi kwako ili wakuharibie maana raisi yuko juu ya Judge. Nani atakubali mwenyekiti asumbuliwe na kajamba nani.

Reforms zianzie kwenye Judiciary judge asimtegemee raisi kwenye kula yake. Hapo ndio tutaona mabadiliko ya kweli ila kuundwe chombo ambacho kinaweza mwajibisha judge akidodge kufanya maamuzi ambacho ni private kwa kutumia katiba.
 
Back
Top Bottom