Napoteza pesa bila kuelewa

Napoteza pesa bila kuelewa

Pole sana mkuu,mambo haya yanawakumba sana hata Tellers wa bank,ni mambo ya mauzauza,wanapoteza pesa na kujikuta wana shoti zisizoisha kila wakati,matokeo yake wanajikuta pesa zao za mishahara zinaishia kulipa hizo shoti.Cha muhimu mkuu fanya maombi ya kuombea eneo lako la kazi,vifaa vyako,line zako,simu,kibanda n.k.kinyume cha hapo hutakaa ufanikiwe kwenye biashara zako,ni damu ya Yesu tu ndio inakuhusu ili kuweza kuvunja hizo nguvu za giza....

Sent using Jamii Forums mobile app
Asante mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
But sijaelewa pia namna inavyofanya kazi hii chuma ulete, unaweza kuelewesha mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
Weee kijana vipi? Mbona unag'ang'ania kujua chumaulete inafanyajekazi? Chuma ulete ni uchawi! Nenda kwa waganga wa kienyeji ukaununue na wewe iitumie kwa wengine upate pesa kama unaona ni deal! Umeishapata ushauri wa kutosha akili kichwani mwako kunyoa au kusuka!
 
mbona unaongea kwa ukali hivyo mkuu, kuna sehem nimeku offend!, ilitosha useme ni uchawi hauna maelezo nje ya ulimwengu wa ushirikina, sioni sababu ya wewe kuwa mkali
 
mbona unaongea kwa ukali hivyo mkuu, kuna sehem nimeku offend!, ilitosha useme ni uchawi hauna maelezo nje ya ulimwengu wa ushirikina, sioni sababu ya wewe kuwa mkali
Chuma ulete ni uchawi,mtu anakuja na pesa yake anakupa,ukiichanganya tu na hela zako zingine inaanza kuzinyonya(kuzisomba) pesa zako mdogomdogo kimazingara,inaweza ikawa inapotea bukubuku kila baada ya masaa mawili bila wewe kujua
 
Ila hizi imani potofu haziachi hi nchi salama kabisa tutabaki hivo hivo.......Africa bado sanaaaaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nakushauri utafute mtumishi aliyesimama ufanyiwe maombi, hizo roho chafu zipo sana, hayo yashamkuta sana mama angu karibia afungwe na taasisi za mikopo, wengne wanarushiwa pepo la madeni kila kukicha ni kukopa hata ufanyeje visa vya kukulia pesa haviishi.
Kuna watumishi wanafanya maombi hawaangalii dini ya mtu.

Sent using Jamii Forums mobile app
mkuu wako wapi hao watumishi au unaweza kudokeza walipo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Poleni kwa majukumu ya ujenzi wa Taifa wana bodi, mimi ni wakala wa m-pesa, kwa muda mrefu nimekuwa naingia hasara bila kujua inatokana na nini, kwa mfano, nina laki tano kwenye sim na nina lako tano mkononi, nikifanya mzuguko ndani ya wiki moja, najikuta nina laki mbili kwene sim na laki tatu mkononi, so hapo kuna jumla ya laki tano sijui imepoteaje.

Nimebadili laini ya uwakala nikidhani ile laini ya kwanza kuna namna aliyeniuzia anaiba, kadhalika na hii line mpya nimeyonunua mwenyewe bado tatizo lipo.

Msaada tafadhari. Natanguliza shukrani

Sent using Jamii Forums mobile app

=====
hakikisha miamala yote unayo halafu nenda voda makao makuu!!!! KAMA MIAAMALA HUNA NENDA NA LINE YAKO WAO LAZIMA WANA MIAMALA.......... Wafanyakazi wa vodacom hasa aliyekusajilia hiyo line wanajua tatizo na wao ndio wanakuibia....... KOMAA NAO MAANA HAKUNA NAMNA ZAIDI YA WAO.
 
1. Hiyo fremu uliyopangisha una muda gani..?
2. Hapo biashara yako ni M-Pesa pekee au kuna bidhaa zingine..?
3. Kama kuna bidhaa zingine, je pesa inapotea kwenye mpesa pekee..?

Jibu maswali hayo kisha nitarejea.
 
Nina miaka mitatu kwenye frame, ni nyumbani, frame niliijenga mwenyewe, ni yangu mkuu, kuna bidhaa nyingine nafanya hapa, mojawapo ndiyo M-pesa, ndiyo bidhaa nyingine sipati hasara, ni kwenye mpesa tu ndo zinapotea

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom