Narudi zangu kijijini, maisha ya mjini siyataki tena

Narudi zangu kijijini, maisha ya mjini siyataki tena

Mkuu nami plan zangu mwakani ni kwenda kuanzisha maisha Tukuyu!

Mji wa Dar es salaam umenikinai na sidhani tena napaswa kuishi hapa!,Zamani tulishindwa kukaa vijijini kwasababu hakukuwa na miundo mbinu Bora,Maji,Umeme na Hospitali nzuri!

Lakini hivi Sasa hata Wilayani huko Kuna maisha mazuri sana na watu Wana enjoy maisha kuliko tunaong'ang'ania hapa mjini!

Mungu akinipa Uhai mwakani nauhama huu mji rasmi!,Nipo kwenye mchakato wa kuuza Nyumba zangu Ili nikajenge huko Tukuyu Nika- enjoy maisha mazuri yenye Hali nzuri ya hewani!
Ni wazo zuri, ila kama utaweza hapo mjini weka kitega uchumi ambacho kitakuwa kinakutumia ata kilo ya nyama kule kijijini.
 
Basi kijijini kwenyewe iwe Mikoa ya Pwani,Lindi ama Mtwara.. watu hawalimi kazi kushinda kwenye bao tu.. unga wa sembe mpaka utoke Dar.. kila kitu kitoke mjini, kazi wanayoithaamini ni kurogana tu.. maisha ya vijijini mazuri yapo Usukumani unaamka asubuhi unakumbana na viazi unashushia na maziwa .. kufumba na kufumbua unaibukia kwenye (Ng'homele) nyama zilizokaushwa, hujagusa (Mashishanga) jibini huko ni full kujiachia utakumbuje Dar ya chai na slace mbili !?
 
Nimeamua nikazeekee kijijini kwa sababu zifuatazo:-​
  • Kule kijijini nitapata hewa safi isiyokuwa na mchafuko​
  • Kule kijijini nitapata majirani wema wasiokuwa na choyo​
  • Kule kijijini tutakuwa tunatembeleana bila chuki​
  • Kule kijijini tutakuwa tunakunywa togwa pamoja​
  • Kule kijijini tutapunguza msongo wa mawazo​
  • Kule kijijini tutaingia shamba lolote kuchuma matunda na kula​
  • Kule kijijini tutakuwa tunasikia milio ya ndege na viumbe mbali mbali​
  • Kule kijijini tutafurahia uoto wa asili​
  • Kule kijijini tutakuwa tunaenda kuwinda kama sehemu ya michezo​
  • Kule kijijini tutapata marafiki wengi ambao sio wanafiki​
  • Kule kijijini tutakuwa tunatembeleana panapotokea mmoja wetu anaumwa.​
  • Kukaa kwenye nyumba ya nyasi yenye hewa safi na ya kuvutia​
  • Kula vyakula vilivyopikiwa kwenye vyungu na kuwa na ladha nzuri​
  • Kendwa kuogelea mitoni na kuvua samaki kama sehemu ya michezo na uwindaji​
Kwa ujumla maisha ya kijijini yatakuwa ni mazuri sana

View attachment 3121969

Kwa nyie mnaobaki mjini, nawaachia mpambane na:-​
  • Majungu na fitina zenu​
  • Mchafuko wa hali ya hewa​
  • Jua kali​
  • Msongamano wa watu​
  • Makelele ya baa na kumbi za starehe zinazoharibu utulivu wa ubongo​
  • Misongo ya mawazo kutokana na changamoto za kimazingira​
  • Kudharauliwa na vijana​
  • Kununua kila kitu; nyanya, yai ,mchicha n.k​
  • Kutokuwa na marafiki wa kweli​
  • Kila mmoja kumuona mwenzie fursa​
  • Kuzeeka kabla ya umri wako​
  • Kupata magonjwa ya moyo na presha n.k​
  • Kula vyakula vyenye kemikali katika kukuzia au usindikaji​
View attachment 3121971

Fanya maamuzi mapema; njoo kijijini tukawinde kanga pori, sungura, n.k pamoja na kuongeza miaka mingi ya kuishi.
Utayamiss mishangingi yenye mitako...ewe die hard fan(s) wa mikalio😂
 
Home sweet home,
Umenikumbusha uliposema mayai ngoja nikacheki bandani walau nichemshe mawili
 

Attachments

  • 1722659574962.jpg
    1722659574962.jpg
    501.5 KB · Views: 3
Mji huu balaa lake siyo dogo,

tunakuwa bize kwelikweli cha ajabu hela inayopatikana ni kulakula tu, ukijisahau 40 hii hapa na upara juu wakati hata kipande cha ardhi huna
Maisha ya mjini kila siku ni mateso, muda mwingi unaupoteza bara barani; achilia mbali stress za hapa na pale
 
Back
Top Bottom