Toyota Celica ilikua inatakiwa irudiwe rangi mi nilikua nyokaa kwa fundi hata kazi siijui vizuri akaniuliza naweza kuivua kioo Cha nyuma nikamwambia ndiyo nikafikiri ni vioo kama vya hiace, wakat natoa kioo nigangonga sehem flan ndogo tu aise kioo kikachanikachanika chote
tukatafuta kioo cha nyuma Cha Celica town hamna kila sehem alaf bei yake tukaambiwa ni ghali sana inazidi hata ghrama ya kurudia rangi, nikaona fundi wangu machozi yanamlenga huku ananiambia kmmae mtalipa na familia yako, tulivyorud gerej nikaona hii ni jela nikamvizia fundi kazubaa nikajidai naenda chooni nikaruka ukuta wa nyuma nikatoka nduki na mkoa nikahama kwa muda sijui kilitokea nini kwa fundi ila kazi ya gereji nikaacha