Ami unajua ile ilikuwa project iliyohusisha mamia ya watu? Wangeweza kweli kuua watu wote hao bila USSR kujua?
Kumbuka USSR walikuwa tayari wana very advance technology kwenye mambo ya anga na waliweza ku intercept radio transmission toka mwezini wakati kina Armstrong wanawasiliana na wenzao duniani. Pia kumbuka USSR hata picha za re-entry ya capsule ya kina Neil kuja duniani walirecord na picha wanazo au nao walikuwa collaborator wa uongo?
Kama ingekuwa fake unadhani kweli USSR wasingesema? Maana walijua kilichotokea. Au walihongwa wafunge mdomo?
USA walirudi na rocky samples ambazo maabara sehemu mbalimbali duniani walipewa hata pale Makumbusho Dar walipewa sample. Unataka kusema dunia nzima wameshindwa kuprove kuwa yale mawe ni fake?
Mwisho unajua kwa nn USSR waliachana na mpango wa kwenda mwezini? Ni kwa sababu waliona wamepoteza kwa kushindwa kwenda wa kwanza kabla ya USA. Waliona haina maana japo wao walikuwa wa kwanza kupeleka chombo mwezini kwao waliona inatosha. Haikuwa na maana tena wao kupeleka mwanadamu