NASA mbona haieleweki kuhusu kupeleka watu mwezini?

Hakuna aliyewai kwenda mwezini, China na marekani kwenda mwezi ni uwongo wenye dhumni fulani.

Allah katika Qur'an tukufu anasema hapo juu kabla ya Atmosphere Kaweka uzio mkubwa ambao hauruhusu kitu chochote kuingia dunia wala kutoka Duniani.

So ikiwa utaamini NASA na CHINA kwenda mwezini basi utakuwa unamaanisha kuwa Allah na Qur'an ni uwongo.

Hao wanasayansi wanatunga uwongo uwongo ili kuwa poteza waja wa Allah.
Cc:&zurri
Hii nayo Chai
 
Bado hujajibu swali.

Mambo ya aina gani?
Na ni kivipi NASA wanapata faida mimi nikielekeza mambo yangu kwao?

Jibu na yale mengine usiishie kwenye "kuogopwa."
Wanapata faida ya kuogopwa na kurejelewa.

Swali gani sijajibu ?
 
Hakuna aliyewai kwenda mwezini, China na marekani kwenda mwezi ni uwongo wenye dhumni fulani.

Allah katika Qur'an tukufu anasema hapo juu kabla ya Atmosphere Kaweka uzio mkubwa ambao hauruhusu kitu chochote kuingia dunia wala kutoka Duniani.

So ikiwa utaamini NASA na CHINA kwenda mwezini basi utakuwa unamaanisha kuwa Allah na Qur'an ni uwongo.

Hao wanasayansi wanatunga uwongo uwongo ili kuwa poteza waja wa Allah.
Cc:&zurri
Mkuu habari za watu kufika mwezini si swali la kuamini au kutoamini, ni hali halisi. Ndiyo, wamekwenda na kurudi. Watu kwenye Mwezi ni Marekani pekee. Mashine zilifika kutoka Urusi na China na kurudi. Zilileta mawe yaliyochunguliwa duniani na kulinganishwa.
 
Hakuna aliyewai kwenda mwezini, China na marekani kwenda mwezi ni uwongo wenye dhumni fulani.

Allah katika Qur'an tukufu anasema hapo juu kabla ya Atmosphere Kaweka uzio mkubwa ambao hauruhusu kitu chochote kuingia dunia wala kutoka Duniani.

So ikiwa utaamini NASA na CHINA kwenda mwezini basi utakuwa unamaanisha kuwa Allah na Qur'an ni uwongo.

Hao wanasayansi wanatunga uwongo uwongo ili kuwa poteza waja wa Allah.
Cc:&zurri
Hizi ni sayansi za kwenye mashamba ya tende kama ile sayansi ya jua kuzama kwenye tope. Vitabu vingine ni masimulizi ya tamaduni za watu na vile walivyomfikiria Mungu na hakuna cha zaidi.
 
Hiyo siyo Sayansi, kama unaijua Sayansi huwezi kuandika haya. Huo ni uhalisia na ndiyo ukweli.

Ndiyo maana mpaka muda huu wanashindwa kuigiza tena tukio lile la mtu kwenda mwezini. Kingine imeonekana watu hawa kumbukumbu hawana, mzozo ni mkubwa sana juu ya tukio hili, baina wanao sadiki na tunao pinga, lakini sisi tunao pinga tuna hoja za kiakili, kimazingira na ufunuo, bali na hoja za kisayansi zinazo onyesha kutokuwezekekana kwa jambo hilo.

Tukirudi katika aya ya 86 katika sura 18, jambo liko wazi, aya inaelezea alichokiona Dhul-Karnain, na hichi ukienda katika sehemu za pwani karibu na fukwe ya bahari watu huwa wanaona jua linapozama upande wa Magharibi kama linazama baharini na ukweli si hivyo. Kwahiyo aya imeongelea kile alichokiona mja huyu mwema. Kwa maana nyingine upende huo ndiko jua lilikuwa linazama.

Sasa kama jambo hili rahisi linakushina hayo ya Wanasayansi utayaweza vipi wakati wao wenyewe washajua mnapenda maigizo.

Kauli yako ya mwisho huwezi kuithibitisha kama ni kweli mpaka unakufa, hasa kama ukiijumuisha katika kauli yako dini ya Kiislamu.

Vijana kwanini mnakuwa wajinga kiasi hiki ? Amkeni aisee mnaikosea sana akili mliyo pewa bure.
 
Sasa mbona unapingana wa neno tena?
Kwani mtu akisema nitakwenda kuangalia Kama kuna usalama wa kupitika tena wewe unaelewaje.
Kwa uelewa wangu ni kwamba alishawahi kwenda kwa kipindi au wakati funani akapita. Sasa je, kutokana na muda wa miaka 53 (sambamba na mabadiliko pengine ya tabianchi tunayokutana nayo, mfano China joto Kali kwa uchache), je bado kuna usalama wa kupitika, kuendeka? Je! kuna mabadiliko au hatari za kiusalama?

Ashakum si matusi, kwani demu uliyekutana naye miaka kumi iliyopita ukimtaka tena huweki tahadhari ya kuvaa sox ya mguu mmoja?
Kupitika wapi?
Mabadiliko ya tabia nchi yanahusika vipi na space travel?
Hiyo ni safari ya outer space hakuna njia kusema kwamba unapita vichochoro, bali ni nafasi tu isiyo na chochote na njia pekee ya kwenda huko ni kwa kutumia precise mathematical calculations.
 
Wanapata faida ya kuogopwa na kurejelewa.

Swali gani sijajibu ?
Naona unatafuta njia ya kukimbia.

Jibu hili swali: point ipo wapi hapo kwenye kusifiwa, kuogopwa na kutukuzwa kama unavyosema na kunawafaidisha vipi NASA developmentally, Physically, Economically na Scientifically?
Na thibitisha kwamba NASA walishindwa kwenda mwezini?

Haya ndiyo madhara ya kupinga mambo ambayo hamna uelewa nayo mwisho wa siku unakimbia sababu huna majibu ya maswali unayoulizwa na vitu unavyopinga.
 
Naona umegota na umeshindwa kwenda mbele kutokea hapo, unarudia rudia jambo ambalo umeshajibiwa.

Kuogopwa ni faida na kurejelewa pia ni faida, tena kubwa sana. Sasa unapotaka point ndiyo uniambie wewe kugopwa na kurejelewa siyo faida. Usitake tena ujibiwe jambo ambali ushajibiwa.

Unataka nikuthibitishie mara ngapi ya kuwa hawajaenda ? Jambo lile linapigwa na Sayansi yao wenyewe kuanzia katika tabia za mwezini na kile kilicho tokea au kuonyeshwa kwenye tukio husika.

Kadhalika umewekewa aya kutoka kwenye Qur'aan, huu ndiyo uthibitisho mkubwa kuzidi ithibati nyingine.

Sasa wewe unae amini ya kuwa walienda na huna ushahidi unaonyesha huitumii akili yaki vyema kwa kuamini jambo amball huna ushahidi nalo.

Kingine onyesha wapi nimekimbia katika swali lako ?
 
precise mathematical calculations
Hizi "Precise Mathematical Calculations" huko mwanzo hawakuzifanya ? Kama walizifanya walizifanya under "Assumptions" au bila "Assumptions" kama ndani yake kuna "Assumptions" hapo hakuna uhalisia na suala la "Precise Mathematical Calculations" kinabaki katika vitabu tu, mengine yanakuwa maigizo.

Unaweza kutuonyesha hizo "Precise Mathematical Calculations" katika safari ya "Outer Space" ?
 
Ami malizia unachotaka kusema
Ninachotaka kusema ni kuwa iwapo walishakwenda mwezini mara nyingi mpaka wakachoka mwaka 1972 hizi mbwembwe za sasa za nini kwenda kukagua wanasema juu na karibu ya mwezi halafu safari yenyewe wanayokusudia kuifanya eti ni mwaka 2024.ingekuwa rahisi tu kwa vifaa vya kisasa kuruka na kumtulisha mtu mwaka huu huu. Mbona pale mwaka 1969 wanapojidai Neil Armstrong alikwenda hakukuwa na mbwembwe hizo. Tuliletewa video keshatua zamani.
 
Kupitika wapi?
Mabadiliko ya tabia nchi yanahusika vipi na space travel?
Kwani walivyo enda mwanzo walipitia wapi ? Hawakuweka point au vituo ? Sababu hata mwezi na jua vina vituo vyake katika safari zake.

Unaulizwa maswali ya msingi badala ya kujibu unauliza tena maswali yasiyo kuwa na msingi.

Kwanza sehemu yoyote ambayo kuna muda ujue kuna nafasi yaani ni space hiyo.

Huku pia kutuambia "outer space" kuna hitaji mjadala. Mwezi uko wapi ? Nje ya mbingu hii kwanza au ndani ya ombwe hili ? Kama ni ndani vipi kusiwe na mabadiliko ya tabia nchi ? Kama ni nje ya ombwe hili, huo ni uongo tunaona Mwezi upo ndani ya mbingu ya kwanza.
 
Hakuna aliyewai kwenda mwezini, China na marekani kwenda mwezi ni uwongo wenye dhumni fulani.

Allah katika Qur'an tukufu anasema hapo juu kabla ya Atmosphere Kaweka uzio mkubwa ambao hauruhusu kitu chochote kuingia dunia wala kutoka Duniani.

So ikiwa utaamini NASA na CHINA kwenda mwezini basi utakuwa unamaanisha kuwa Allah na Qur'an ni uwongo.

Hao wanasayansi wanatunga uwongo uwongo ili kuwa poteza waja wa Allah.
Cc:&zurri
Huo ukanda unaosema nadhani ni Allen belt. Wanasayansi wa kimarekani kwenyewe wametoa maelezo ya kisayansi kwa urefu kuonesha hakuna yeyote aliyepenya mwaka huo kufika mwezini na wakasema ni kitu haikiwezekani. Kwa uwezo wa Allah hapo baadae inaweza kuwa kwa kupata teknolojia mpya.Lakini kwa mwaka ule wanasema hakukuwa na utaalamu wowote wa kutua na kurudi na haiwezekani kuchukua picha kwa kamera za kodak ukarudi na picha duniani bila kuunguzwa na mionzi ya jua.
 
Ninachotaka kusema ni kuwa iwapo walishakwenda mwezini mara nyingi mpaka wakachoka mwaka 1972 hizi mbwembwe za sasa za nini kwenda kukagua wanasema juu na karibu ya mwezi halafu safari yenyewe wanayokusudia kuifanya eti ni mwaka 2024.ingekuwa rahisi tu kwa vifaa vya kisasa kuruka na kumtulisha mtu mwaka huu huu. Mbona pale mwaka 1969 wanapojidai Neil Armstrong alikwenda hakukuwa na mbwembwe hizo. Tuliletewa video keshatua zamani.
Kwa hiyo ile 1969-1972 ilikuwa fake hawakutua mwezini? Au walitua majangwa ya Arizona huko wakapiga picha wakatuletea?
 
Huyo kilaza Kisai ni mlevi wa dini mpaka amebakia na kichwa kama mfuko wa kubeba meno tu.
Mimi nimeshajiuliza kwanini waongope na jibu nililopata ni hakuna faida yoyote watakayopata wakiongopa.

Sasa niambie point ipo wapi hapo kwenye kusifiwa, kuogopwa na kutukuzwa kama unavyosema na kunawafaidisha vipi NASA developmentally, Physically, Economically na Scientifically?
 
Wewe, Mathanzua na wenzako wengi walio walevi wa dini ambao ni wanaamini wa kila conspiracies ni watu wa hovyo sana kuwahi kutokea katika jamii ya binadamu.
Hiyo siyo Sayansi, kama unaijua Sayansi huwezi kuandika haya. Huo ni uhalisia na ndiyo ukweli.

Ndiyo maana mpaka muda huu wanashindwa kuigiza tena tukio lile la mtu kwenda mwezini. Kingine imeonekana watu hawa kumbukumbu hawana, mzozo ni mkubwa sana juu ya tukio hili, baina wanao sadiki na tunao pinga, lakini sisi tunao pinga tuna hoja za kiakili, kimazingira na ufunuo, bali na hoja za kisayansi zinazo onyesha kutokuwezekekana kwa jambo hilo.

Tukirudi katika aya ya 86 katika sura 18, jambo liko wazi, aya inaelezea alichokiona Dhul-Karnain, na hichi ukienda katika sehemu za pwani karibu na fukwe ya bahari watu huwa wanaona jua linapozama upande wa Magharibi kama linazama baharini na ukweli si hivyo. Kwahiyo aya imeongelea kile alichokiona mja huyu mwema. Kwa maana nyingine upende huo ndiko jua lilikuwa linazama.

Sasa kama jambo hili rahisi linakushina hayo ya Wanasayansi utayaweza vipi wakati wao wenyewe washajua mnapenda maigizo.

Kauli yako ya mwisho huwezi kuithibitisha kama ni kweli mpaka unakufa, hasa kama ukiijumuisha katika kauli yako dini ya Kiislamu.

Vijana kwanini mnakuwa wajinga kiasi hiki ? Amkeni aisee mnaikosea sana akili mliyo pewa bure.
 
Kwa hiyo ile 1969-1972 ilikuwa fake hawakutua mwezini? Au walitua majangwa ya Arizona huko wakapiga picha wakatuletea?
Ndio kilichotokea.Wahusika wote wa mchezo ule baadae wote walipotea na waliobaki hai walikuwa kama wafungwa,hawakuruhusiwa kuonana na watu wala kuhojiwa na vyombo vya habari.
 
Back
Top Bottom