Nasema hivi, Mume anauma!

Nasema hivi, Mume anauma!

Duh pole sana kumbe watu mna visa na mikasa ya kuogofyaa
Acha tu mkuu. Yaani mimi hakuna cha kunishtua. Nipo cool hadi mwenyewe anashangaa. Sina wivu hata arudi asubuhi siulizi chochote maisha yanaenda.
Kila mtu na atafakari matendo yake bila kupigizana kelele.
 
Nimemulika mwizi!!! Fakeni kabisa

Miaka yote nasikia mume anauma mume anauma nikawa nasema wanaume hawa walivyo wengi anauma nini bwana?? Leo yamenikuta.

Kama mwezi umepita nilikuwa nahisi naibiwa. Kuna ile female intuition tu unajua hapa tuko watatu kwenye huu uhusiano.

Sasa mi si ndio mtaalamu wa IT, nikafanya timing karibu wiki 2 hadi nikafanikiwa kuweka mtego wangu. Lahaula nimekutana na mke mwenzangu mtoto wa 2000.

My analysis of the situation;

Binti sio mtaalamu wa masuala ya kula waume za watu. Sio kwamba namu-underestimate, najua ana power yake. Ila nashukuru Mungu hayuko at war, anatreat huu uhusiano kama mwingine wowote yaani anamuona kama mpenzi wake peke yake. She is at ease.

Nilichofanya ni sijataka mambo yawe mengi, nimemtafuta ex wangu mmoja anapenda chini, anapenda watoto wenye rangi za Mtume maana hata mi alinifatiaga hicho hicho. Nimempa namba, jina, anapopatikana na nimempa pesa (kwa hasira nimemuomba huyu huyu anayenitia hekaheka) amuachanishe huyu mtoto kwa my wangu. Nimemwambia amchanganye apeleke hata posa mi nitagharamia.

Ubaya wa issue hizi bwana yaani tangu nimejua kama wiki 2 zilizopita kila anachoniambia naona uongo. Akijifanya kutaka kukulana namwambia niko period. Hadi jana kauliza “period haiishi?” Nikamwambia “nina stress labda imesababisha”. Akale huko huko nje aache uroho, alaaa…

Sometimes nikioga nalia sio utani. Mume anauma kweli!
Wee wakati huko mtaani wanasema hawajali wala nini!!!

Eti mwingine anatafuta kidumu alipize kisasi... Hapo ndo ninapochoka..

MUME ANAUMA NAKAZIA

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Zurie pole kwa changamoto.

Je, umewahi kuwaza ikitokea mmeo akajua kuwa uliwasiliana na Ex wako kupanga mipango mliyopanga atajisikiaje!!!?

Atafikri nini juu ya hayo mawasiliano na huyo Ex Wako!?

Nadhani hukupaswa kumuingiza mtu mwingine kweye hili suala lako wachilia Ex wako.

Bado naamini njia nzuri ilikuwa kumtafuta hiyo binti (kwa siku au physically) na kumpa onyo kali ambalo litamfanya amwambie mmeo kuwa IMETOSHA.
 
Akikujibu unitag chief
 
Niwe tu mkweli, kwa ninavyojisikia hili wazo limenipitia mara kadhaa kwamba labda nitajisikia better.

Akija mtu na usiriazi anaweza kuniangusha (Mungu anitangulie). Nina hasiraa
Watakuambia hujalipia hili tangazo
 
Zurie pole kwa changamoto.

Je, umewahi kuwaza ikitokea mmeo akajua kuwa uliwasiliana na Ex wako kupanga mipango mliyopanga atajisikiaje!!!?

Atafikri nini juu ya hayo mawasiliano na huyo Ex Wako!?

Nadhani hukupaswa kumuingiza mtu mwingine kweye hili suala lako wachilia Ex wako.

Bado naamini njia nzuri ilikuwa kumtafuta hiyo binti (kwa siku au physically) na kumpa onyo kali ambalo litamfanya amwambie mmeo kuwa IMETOSHA.
I will be everything in this world except a woman who confronts another woman kuhusu mwanaume. Hii ni principle yangu, najua ndivyo watu hufanya ila mimi milele sitofanya.

Kuhusu kinachopaswa kufanywa i think tumeshapita hiyo point maana hata yeye hakupaswa kufanya anayoyafanya.

Kuhusu atakachofikiria kuhusu mimi kuwasiliana na ex wangu sidhani kama ni shida zangu kwakweli. Anaruhusiwa kufikiria chochote kile.

Wengi mtahisi labda nafanya yote kung’ang’ania mume sijui ndoa lakini najaribu kufanya my part kama mke ya kutulinda (mimi na mwanae) from external parties ambayo yeye kama our protector ameshindwa. So, atakachoamua akijua kitakuwa ndio hicho, nitaumia nitalia ila maisha yataendelea vile vile.
 
Wee wakati huko mtaani wanasema hawajali wala nini!!!

Eti mwingine anatafuta kidumu alipize kisasi... Hapo ndo ninapochoka..

MUME ANAUMA NAKAZIA

Sent using Jamii Forums mobile app
Na ni haki yao kulipiza au kutojali sababu inakera sana, inaumiza na it is sooo unnecessary.

Wanaume watatetea hapa watasema sijui ndo waliumbwa hivyo ila najiuliza why wanafunga ndoa na kuapa uaminifu kama wanajua wazi hawakuumbwa kuwa na mtu mmoja?
 
Back
Top Bottom