Nashangaa bado kuna watu waamini kuna kiumbe kinaitwa Shetani

Nashangaa bado kuna watu waamini kuna kiumbe kinaitwa Shetani

Shetan yupo ila yeye ni jini na hivo ili umuone ni lazima aje katika umbo bandia kama binadamu, paka, mbwa au nyoka. Ila katika maumbile yake asilia shetan hawez onekana.

Katika kipind cha mtume muhammad s.a.w shetani alishawahi kujitokeza mara tatu akaonekana ila katika maumbile ya binadamu katika nyakati tofauti.

Mara ya kwanza ilikuwa katika kikao cha makuraish wakijadili namna ya kumuua mtume, ghafla alikuja mtu akiwa katika mavaz maridad na muonekano nadhifu kuliko kawaida, makuraish wakajua kwa namna yeyote mtu huyo atakuwa na busara kias cha kuwa na mbinu bora ya kumuua mtume, hivo wakamshirikisha katika mpango huo na walipotaka kujua yeye ni nan na anatokea wap shetana aliwadanganya kwa kuwatajia jina la uongo na mji ambao wao hawaujui.

Mara ya pili ni katika vita wakat jesh la mtume lipo vitan, makafir walikuwa wakiongozwa na mtu wao, lakin baadae allah akashusha jesh la malaika kumsaidia mtume, na hapo yule mtu anaeongoza makafir akakimbia kuelekea baharin na hakuonekana tena, wenzake wakashangaa
 
downloadfile-15.jpg
 
Kama ni mishumaa nimeshawasha sana ili nione kama Shetani atakuja lakini wapi. Kama ni chanting nimeshafanya ili nithibitishe kama Lucifer ama Shetani yupo bado niliambulia patupu.

Nimethibitisha Shetani hayupo
Usitafute sababu ya kufanya dhambi. Moto upo palepale.
 
Mara ya tatu shetan kuonekana ni katika kisa cha abu huraira r.a ambapo alimkamata mwizi alieiba chakula kutoka katika baytul mal yaani treasury house. Mwiz huyu alikuwa mzee na alijitetea kuwa ananjaa na maisha magum hivo abu huraira akamwonya asirudie tena kuiba kisha akamuachia, lakin mzee yule alirudia tena hadi mara ya tatu na ndipo abu huraira akamwambia saiz nakupeleka kwa mtume akakupe adhabu. Ikumbukwe kuwa kipind cha mtume adhabu ya mwiz ilikuwa kukatwa mkono mmoja, sasa yule mzee akaona akipelekwa huko atapata majanga akaona amalizane na abu huraira kimya kimya, alichokifanya yule mzee akamwambia abu huraira nikumbie jambo la kheri ili uniachie, basi abu huraira akamuliza jambo gan hilo? Yule mzee akasema soma aya ya mwisho katika suratul baqara ili kujikinga na shetan. Basi abu huraira akamuachia kisha akaenda kumsimulia mtume kisa kizima na mtume akasema huyo mzee ni shetan na hilo alilokufundisha ni kweli.
 
Back
Top Bottom