Nashangaa bado kuna watu waamini kuna kiumbe kinaitwa Shetani

Nashangaa bado kuna watu waamini kuna kiumbe kinaitwa Shetani

Unadhani kila mtu ni muoga kama wewe?

Kama Shetani yupo lete formula za kumuita.
Maana kila jaribio nililofanya hakuwahi kutokea. Hizi stori za Shetani na Mungu hazina uhalisia.
Kuna mengine sio ya kujaribu, ni bora uyaache kwenye nadharia tu.

Utakuja kuita popobawa akufanye mchezo mbaya.

View attachment 3263495
 
Mara ya tatu shetan kuonekana ni katika kisa cha abu huraira r.a ambapo alimkamata mwizi alieiba chakula kutoka katika baytul mal yaani treasury house. Mwiz huyu alikuwa mzee na alijitetea kuwa ananjaa na maisha magum hivo abu huraira akamwonya asirudie tena kuiba kisha akamuachia, lakin mzee yule alirudia tena hadi mara ya tatu na ndipo abu huraira akamwambia saiz nakupeleka kwa mtume akakupe adhabu. Ikumbukwe kuwa kipind cha mtume adhabu ya mwiz ilikuwa kukatwa mkono mmoja, sasa yule mzee akaona akipelekwa huko atapata majanga akaona amalizane na abu huraira kimya kimya, alichokifanya yule mzee akamwambia abu huraira nikumbie jambo la kheri ili uniachie, basi abu huraira akamuliza jambo gan hilo? Yule mzee akasema soma aya ya mwisho katika suratul baqara ili kujikinga na shetan. Basi abu huraira akamuachia kisha akaenda kumsimulia mtume kisa kizima na mtume akasema huyo mzee ni shetan na hilo alilokufundisha ni kweli.
Achana na story za Quran
 
Hizi stori za vijiweni zimetosha sasa( over)
Shetan yupo ila yeye ni jini na hivo ili umuone ni lazima aje katika umbo bandia kama binadamu, paka, mbwa au nyoka. Ila katika maumbile yake asilia shetan hawez onekana.

Katika kipind cha mtume muhammad s.a.w shetani alishawahi kujitokeza mara tatu akaonekana ila katika maumbile ya binadamu katika nyakati tofauti.

Mara ya kwanza ilikuwa katika kikao cha makuraish wakijadili namna ya kumuua mtume, ghafla alikuja mtu akiwa katika mavaz maridad na muonekano nadhifu kuliko kawaida, makuraish wakajua kwa namna yeyote mtu huyo atakuwa na busara kias cha kuwa na mbinu bora ya kumuua mtume, hivo wakamshirikisha katika mpango huo na walipotaka kujua yeye ni nan na anatokea wap shetana aliwadanganya kwa kuwatajia jina la uongo na mji ambao wao hawaujui.

Mara ya pili ni katika vita wakat jesh la mtume lipo vitan, makafir walikuwa wakiongozwa na mtu wao, lakin baadae allah akashusha jesh la malaika kumsaidia mtume, na hapo yule mtu anaeongoza makafir akakimbia kuelekea baharin na hakuonekana tena, wenzake wakashangaa
 
Katika kisa hiki cha mwisho kuna dokezo mbili kuhusu shetan.

1. Moja ni kuwa shetan akiwa katika umbo bandia basi anaweza kupata athari za kimaumbile yaani pain and pleasure ndo mana yule mzee alipokamatwa na abu huraira alishindwa kupotea kimazingara na badala yake akaamua kujitetea ili asipelekwe kwa mtume mana kama mtume angeamua kukata mkono wa yule mzee basi shetan angepata madhara.

2. Dokezo la pili ni kuwa shetan anaweza kuongea ukwel ndo mana mtume alithibitisha yale maneno yule mzee. Japokuwa kwa asili yake shetan ni muongo haswa.
 
Kama kuna mapepo, majini na mizimu basi pia kuna ulimwengu wao wanaoishi. Hujawahi kuona watu wakipandisha mapepo au majini?
Viumbe vyote ulivyovyitaja hapo nishajaribu kuwaita Kwa kila namna lakini hakuna aliyetokea.
 
Binafsi nawezasema watu weng tu wameshawah kukutana na shetan ila hawajui kama ameshawahi kuonana nae kwa sababu shetan katika umbo la asili haonekan. Sasa hata akija katika umbo la bandia pia huwez mtambua kwa kuwa wewe utaona kiumbe cha kawaida kama mtu au mnyama tu wakawaida.

Mfano mzuri wa wakat ambao binadamu anakutana na shetan ni wakati wakwenda maliwaton, huko ndo makaz ya mashetan. Pia wakat wakula chakula, shetan hula nawewe na ndo mana kuna wakat unakula ila haushibi au unakunywa kinywaj lakin kiu haikat. Kiufup shetan yupo na tunakatana nae katika namna mbalimbali.
 
Nasikiaga nyie walokole mnamkanyaga Shetani!!!

Kwani Yuko wapi mbna sijawahi kumuona🤣🤣
Kwani shetani na Mungu ni vitu vya kuonekana mpaka utake kuviona au ni ishu ya imani. Wewe amini tu au usiamini lakini usitake kuona vitu visivyoonekana
 
Kwani shetani na Mungu ni vitu vya kuonekana mpaka utake kuviona au ni ishu ya imani. Wewe amini tu au usiamini lakini usitake kuona vitu visivyoonekana
Kama hawaonekani bora wangesikika basi.
Mda nilioufanya uchunguzi kwa hao viumbe Itoshe kusema hawapo.
 
Pengine walikuja katika umbo lingine huwezi jua. Halafu badala ufocus kwenye kutafuta hela wewe unafocus kwenye kuwaita majini shauri yako.
Sio lazima kila mtu awe na hela.

Priority yangu ni kutaka kufahamu kama hivi viumbe vipo ama ni story za kusadikika.
 
Back
Top Bottom