Hivi kwa nini huwa hamumlinganishi na sifa za wizi, ula rushwa, ufitini na ukandamizaji wa haki na vitu kama hivyo? Mbona mara zote mnakuja na ajenda za kitoto toto kwa huyu mama? Hivi mnajua jinsi gani anagusa maisha ya watu wanyonge zaidi? Waulize watu wa chini kabisa. Vema tuungane naye kwenye SMAUJATA tukapinge ukatili, tutangaze naye namba 116 Ili watu wakiona dalili za ukatili au ukatili watoe taarifa na kama hawapokelewi huko wamtumie ujumbe yeye binafsi kwenye 0734124191 au 0765345777 halafu Sasa mtaona moto wake.
Acheni wazalendo wachache waliobakia wafanye kazi walau wanyonge wasio na simu janja za kupiga porojo kama nyie humu wapate faraja. Hiyo afya kaeni nayo wenyewe maana alipoanzisha ukaguzi wa dawa na ukaguzi wa huduma za tiba na hela zikiwemo za bima aligusa mifuko yenu na mkasikilizwa. Sasa si mlishinda yamepita, yamekuwa mapya, shida nini sasa? Tulieni au jiungeni na SMAUJATA fomu hiyo hapo.