Kwa katiba yetu tunayoitumia sasa, waziri siyo lazima awe mtaalam wa wizara husika. Waziri ni mwanasiasa, kwa sababu ili uwe waziri lazima uwe mbunge (mwanasiasa). Kazi ya waziri ni kuhakikisha anasimamia ilani ya chama chake kimesema kitafanya nini kuhusu wizara husika.
Huko ndani ya wizara wamo wataalam wa wizara husika, hao hushughulika na mambo ya kitaalam ya uendeshaji wa wizara.
Wizara ya afya imewahi kuwa na mawaziri wenye taaluma ya afya, mfano kina Dr. Aaron Chiduo, Prof. Sarungi, Prof.Mwakyusa, Dr. Hussein Mwinyi na wengine, wote hao pamoja na taaluma zao walikuwa wanasiasa. Wakati mwingine hutokea hao unaowaita mawaziri wataalam huboronga sana kwa kujidai wanajua kuliko wote kwenye wizara kisa cheo.
Angalia wizara ya ulinzi ilivyotulia, sidhani kama huyo mama waziri ni mwanajeshi, hata hivyo jeshi linaboreka kiutendaji kupita wataalam wa kijeshi waliopo. Ummy ni mwasheria bila shaka, chini yake kuna wataalam wa kutosha ukianzia na katibu mkuu wake. Kama wizara haifanyi ni issue ya leardeship tu na wala siyo professionalism. Hukutenga fedha za kutosha kwenye afya unategemea nini!!
Mwanasiasa huangalia upepo unakoelekea basi. Kama Kuna korona na Rais kaibuka na hoja ya nyungu, haijalishi waziri ni taaluma gani, ndiye atakayeongoza japo anajua kiafya siyo, tulimuona Gwajima enzi hizo.
Aliyejaribu kusimama kwenye taaluma nadhani naibu wake Dr. Ndungulile alijaribu kupinga aliishia kuondolewa.
Tubadili katiba tuondoe kipengele cha waziri lazima awe mwanasiasa (mbunge) labda watateuliwa kwa kuzingatia professionalism. Asante.