Nashauri awamu ya sita agombee Rais Mstaafu Ndg. Jakaya Kikwete

Nashauri awamu ya sita agombee Rais Mstaafu Ndg. Jakaya Kikwete

Trust None

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2018
Posts
1,260
Reaction score
4,419
Pamoja na mapungufu yake katika awamu ya nne, Rais Kikwete aliweza kujenga mshikamano kwa Watanzania kwa asilimia kubwa jambo ambalo kwa sasa hivi limepungua sana.

Uchumi ulizidi kuimarika, deni la taifa lilikuwa chini, miundombinu ilizidi kujengwa, Watumishi wa Umma walipata increment na walipanda madaraja, ajira zilitolewa bila kutuma maombi. Kwa ufupi, pesa ilikuwepo mtaani.

Hata pale alipoenda kufanyiwa operesheni ya tezi dume hakuna aliyemuombea kifo.

Mungu ndiye muweza wa yote, nakuomba ndg JK pindi ikifika muda muafaka, chukua fomu upeperushe bendera ya CCM kuwania urais.
 
Pamoja na mapungufu yake katika awamu ya nne, Rais Kikwete aliweza kujenga mshikamano kwa watanzania kwa asilimia kubwa jambo ambalo kwa sasa hivi limepungua sana.
Bado miaka 4 wewe unawaza uchaguzi Leo? Kwamba Watanzania hadi 2025 hatatokea mwingine mwenye uwezo isipokuwa kumrudisha mzee Kikwete?
 
Yaan Kama kunawatu ni wanafik duniani ni watanzania mtu anathubutu kusema kikwete arudi madarakani Yaan wanasahau wale viongozi wao njaa kali walivyokuw wanambeza hadharani kwamba hafai Mara Hana msimamo, Hakai Tanzania akatulia anasafiri kilacku Mara nchi ilikuw masikini twiga wanabebwa kwa ndege na kupelekwa nje ya nchi.

Alafu Leo et Bora arudi Yaan celew ni hamna ubongo mkumbuke maneno yenu au. Kiufupi mtake mctake Rais magu Anaendelea na atapitishwa mwngne kutoka CCM wakati ukifika.

kiufupi tuacheni ubishi Hakuna mtu yeyote kutoka upinzani anayeweza kuongoza hii nchi hao wanapigaga lomoni tuu hamna chochote ikifika wakati wa uchaguzi wanatafuta walio hama ccm ndo wanawaweka wagombee urais ..inaonyeshaje walivyo hawajiamin naishia hapo tuu

Nipeni chai kwanza
 
Kikwete Zana na Tunu ile tumwacheni apumzike.
 
Back
Top Bottom