Auz
JF-Expert Member
- Apr 6, 2016
- 13,539
- 11,419
Uongouongo na ujanja janja ndio propaganda za ccm kwa WaTz, kila siku kwenye runinga, radio na mitaani.Passport ni kitu muhimu sana. Lakini ukisikiliza ni malalamiko ya watu wengi kuwa upatikanaji wake ni mgumu.
Kutokuwa na passport ni moja ya sababu watanzania wengi kukoswa grobal mentality. Wengi mambo yakiwa magumu wanafikilia kurudi vijijini badala ya kutafuta fursa nje ya nchi.
Kigezo eti hadi uwe na sababu au muariko nje ya nchi umepelekea wengi kudanganya kwa kutunga miariko. Hii inasababisha taifa kuwa na watu waongowaongo na wajanjawajanja kitu ambacho dunia haikitaki.
Ushauri wangu kwa uhamiaji kama hakuna sababu nyingine basi iwekwe sharti kwa mtu kuanza chuo au kufungua biashara lazima awe na passport. Kuhusu gharama waangalie namna ya kufanya.
Ni hayo tu.
Sent from my moto g 5G (2022) using JamiiForums mobile app