Nashauri magari yote ya Serikali na Taasisi za Umma yapakwe rangi za nembo zao kupunguza ukiritimba

Magari yote ya serikali yapakwe rangi ya bendera ya taifa hii itasaidia kupunguza matumizi mabaya ya magari hayo
 
V8 likiisha badilik plate number inakua mali ya dereva,muhimu kupiga kaunda suit safiii anakula maisha mjini na watoto wazuri.
Kuna mmoja yupo Dodoma huwa anatoa kibao cha STK na kuweka T ... DB.
 
Magari yote ya serikali yapakwe rangi ya bendera ya taifa hii itasaidia kupunguza matumizi mabaya ya magari hayo
Yapakwe rangi ya nembo kama ilivyo mengine
 
Ongezea, weekend madereva wengi wa serikali wasio waaminifu wana weka plate number feki, alafu wanauza mafuta hasa Jpili jioni na kubakiza mafuta kidogo kwani Jumatatu huwa wanajaza full tank, pia wakitumia hizo plate number feki, wanaweza uza spares original na kununua feki kisha kuharibu gari.

Hili suala muhimu sana kwa serikali kulifanyia kazi, ikiwemo kuacha kununua ma VX V8 kwa viongozi ngazi za chini ya Waziri, wengine wote chini ya Waziri hata Naibu Waziri awe na prado au Land cruiser standard tu.
 
Suzuki Jimmy zinawatosha sana
 
Ni kweli. Kuna ujinga mwingi sana wa matumizi ya magari ya Serikali.
Sahivi wanataka wawakopeshe! Ebu fikilia kama mwenye gari atachelewa kulifanyia matengenezo huoni itaathili safari za huyo mkurugenzi
 
Kuwakopesha magari ni wazo zuri lakini itaathili utendaji kwasababu hawatakubali magari yao yakalale kwa dereva, kwa hofu ya kupigwa spea
 
Sahivi wanataka wawakopeshe! Ebu fikilia kama mwenye gari atachelewa kulifanyia matengenezo huoni itaathili safari za huyo mkurugenzi
## fikilia (fikiria) ### itaathili (itaathiri?

Mkulungwa, kichwani upo sawa sawa kweli?[emoji3][emoji3]
 
Shabiby kaongea point sana Jana kuhusu magari! Pamoja na yote msiache kuyapakaa rangi za nembo
 
Duniani umefika jana?Unamjua binadamu vizuri kweli na mbinu zake kwa kadiri unavyomletea mikingamo?Utajua hujui!
 
Unafikiria hawawezi? Ni boss wa kuwawajibisha hayuko
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…