Nashauri magari yote ya Serikali na Taasisi za Umma yapakwe rangi za nembo zao kupunguza ukiritimba

Nashauri magari yote ya Serikali na Taasisi za Umma yapakwe rangi za nembo zao kupunguza ukiritimba

unaku na ukuda.hujafikiria suala la usalama. kaz hizi muda mwingine zimahitaji kutotambulika hv nikupe mfano we unafikr gar flan ikujulikana huona kama inahatarisha usalama wa wafanyakaz
unafikir watu wote wanapenda maamuz ya taasisi mbalimbal.hujafikria vizur labda kwa vile haupo huko

Namba haifamahishi kuwa ni ya serikali? Lini polisi wameenda kukamata watu na gari yenye muonekano wa private?
 
  • Thanks
Reactions: Cyb
Dawa ya matumizi mabaya ya hizi v8 za serikali ni kuzipaka zote rangi ya bendera ya taifa hii itaepuka zisitumike kupelekea watoto shule, kupaki kwenye majumba ya starehe au safari zisizo husu shughuli za serikali.
 
Plate number wanabandika private number zingine juu yake. Dawa yapigwe rangi ya bendera ya taifa hii ndo dawa komesha ya matumizi mabaya ya magari ya serikali.
 
Ukiondoa magari ya IKULU na yale ya Viongozi wa kitaifa;

Naishauri ofisi ya waziri mkuu ikiongozwa na Mh Majaliwa Kassimu kwa kushirikiana na Tamisemi chini ya Bashungwa!

Waelekeze magari yote ya serikali yapakwe rangi ya nembo ya taasisi husika kama ilivyo kwa taasisi chache kama (Polisi,Tanesco, NHC, NSSF n.k)

Na hili lisiishie tu kupaka magari ya SITE na kuacha mashangingi au magari mengine ya mameneja na wakurugenzi pasipo kuwa na rangi za nembo zao!

Maelekezo ya ukamataji magari yasiyo kuwa na nembo wapewe trafiki ili waanze msako wa kukagua kadi za gari feki na dereva atakayekamatwa ahukumiwe kesi ya hujuma.

Hili litasaidia uwajibikaji ili wanainchi waone nani mharibifu wa Mali ya umma, nani anakimbia mbio za hatari barabarani, nani kaenda kulewa muda wa kazi, nani yuko gesti mida ya kazi, nani kabebea mbuzi wake kwenye shangingi la serikali! N.k

Watu wa masijala wahakikishe kila chombo cha moto cha serikali kiwe na rangi za nembo husika ili kuongeza uwajibikaji na kupunguza ukilitimba.

Hili litasaidia mambo kama haya!
1. Madereva wa serikali siku hizi wamebuni mbinu ya kuwa na namba za usajili feki (fake plate number) ambazo hubandika siku za weekend na kutumia gari jambo linalochangia uchakavu wa haraka na kuighalimu serikali kufanya matengenezo

2. Madereva wanapokuwa na hayo magari yasiyo na nembo (waliyoweka feki namba binafsi) ni rahisi sana kuuza au kubadilisha vipuli orijino kwenye gereji bubu na kuitia hasara serikali

3. Matumizi ya mafuta yako juu kwasababu magari yasiyo na nembo yanashawishi mizunguko isiyokuwa ya lazima

4. Magari yasiyo na nembo hayaoneshi uwajibikaji kwa wananchi (hili lipo kisaikolojia zaidi)

Nasema hivi kwasababu nimeshuhudia mashangingi kadhaa ya serikali STL au DFPA lakini wakifika mtaani wanabandika namba binafsi mfano DZA!

Kwahiyo mtu kama huyu akiuza kipuli gereji yoyote hakuna atakaye mshitukia!
Wewe jamaa umepinda, wahusika watakuwa wanachungulia na kuguna au kuchukia juu ya huu uzi wako.

Uliyoyasema ni kweli tupu katika bandiko lako hili.

Atakayekupinga itabidi akapimwe akili yake vizuri.

Gharama kubwa sana inatumika, mfano mafuta, matumizi ya magari, matengenezo n.k.

Juzi bungeni Spika alishauri gari za Serikali zizimwe wanaposhuka viongozi wawapo mikutanoni, madereva watoke ndani ya magari.

Kweli, plate namba fake ni jipu. Unakuta usiku wa manane gari zipo maeneo ya baa au mitaani.

Serikali ikitekeleza ushauri wako, kutakuwa na matumizi sahihi ya magari na kuleta tija kwa Watanzania.
 
Umenichekesha sana. Zama Mkete alimkimbia Ruge kwa mtego wa aina hiii. Yule dogo pia alikua na V8 katupia kiunoni na Kabastola ka Boss wake Zama akazama mzima mzima kuja kustuka watoto wa3 kaishia kumweka jamaa Billboards ili tujue amempenda kuuuumbe ana maumivu ya karne
[emoji38][emoji38], unasemaje? Hebu ongeza sauti tena tukusikie bwasheee
 
Wazo zuri ila hatuna wa kumvisha paka kengere, maana wote wenye uwezo huo ndo wanatumia hayo mashangingi
 
Wazo zuri ila hatuna wa kumvisha paka kengere, maana wote wenye uwezo huo ndo wanatumia hayo mashangingi
Wanapenda waonekane mashangingi ni yao wanapobebea mishangingi, yakipakwa rangi hata foleni itapungua, wanaotanua tutawajua vizuri kwa rangi zao
 
Roho mbaya iko wapi, waswahili banaa ndo maana hatuendelei.
Yaani maendeleo kwenye hizi nchi zetu za Afrika ni shida mnooo, imagine mwananchi hataki kuwa accountable kwa mali za umma,lakini kesho akienda zahanati na kukosa huduma analalamika wakati anaona kabisa dereva au bosi wake wanatumia magari vibaya. Mtu akiiba fedha ya umma anaonekana mwamba. Unawakuta kwenye Bus dereva anaendesha vibaya, hataki kusimama njiani watu wachimbe dawa na hapo ni safari ndefu... Lakini trafiki akuwasimasha na kuuliza je dereva anaendesha vizuri Bus? Bus zima utawasikia ndiyooo.. [emoji23] [emoji23] Yaani ni unafiki tuu
 
Yani maCCM yameharibu sana NCHI hii

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
 
una uchungu eeh kwa vile hipat wwewe? bahat ya wenzo silalie mlango wamzi!! utangatwa na umbwa

Sent from my TECNO CF7 using JamiiForums mobile app

Hapana julai ,sina uchungu na wao ,nazungumzia matumizi mabovu ambayo hayana tija , haiwezekeni uende na convoy ya vieite 20 kwenda kukagua shule ambayo haina choo au maji.

Haiwezekani msafara wa vieite 30 kwenda kwenye mkutano dodoma while tungetumia technlogy tukafanya online meeting na hizo fedha tutakazoziokoa ziende kama ruzuku kupunguza bei ya mafuta.

Wanalipwa mishahara inayowatosheleza mambo ya kufosi safari ,warsha ,makongamono ni WIZI mtupu.
 
Duh
 
Back
Top Bottom