Nashauri magari yote ya Serikali na Taasisi za Umma yapakwe rangi za nembo zao kupunguza ukiritimba

Nashauri magari yote ya Serikali na Taasisi za Umma yapakwe rangi za nembo zao kupunguza ukiritimba

Magari ya Seikali na Mashirika au wakala yanapaswa kuwekwa nembo ubavuni mlangoni ili yafahamike. Dawa ni hiyo tu.
 
Wazo zuri sana

Maana wengine wanazitumia kubebea
Madem zao tu

Ova
 
Wazo zuri sana

Maana wengine wanazitumia kubebea
Madem zao tu

Ova
Kuna connection imevuja gari LA serikali vijana wanafanyia ngono! Yapakwe rangi za nembo zao harafu tinted yasiwekwe serikali yetu ni ya uwazi kwann kujificha ndo maana hata yanatumika kwa magendo
 
Ukiondoa magari ya IKULU na yale ya Viongozi wa kitaifa;

Naishauri ofisi ya waziri mkuu ikiongozwa na Mh Majaliwa Kassimu kwa kushirikiana na Tamisemi chini ya Bashungwa!

Waelekeze magari yote ya serikali yapakwe rangi ya nembo ya taasisi husika kama ilivyo kwa taasisi chache kama (Polisi,Tanesco, NHC, NSSF n.k)

Na hili lisiishie tu kupaka magari ya SITE na kuacha mashangingi au magari mengine ya mameneja na wakurugenzi pasipo kuwa na rangi za nembo zao!

Maelekezo ya ukamataji magari yasiyo kuwa na nembo wapewe trafiki ili waanze msako wa kukagua kadi za gari feki na dereva atakayekamatwa ahukumiwe kesi ya hujuma.

Hili litasaidia uwajibikaji ili wanainchi waone nani mharibifu wa Mali ya umma, nani anakimbia mbio za hatari barabarani, nani kaenda kulewa muda wa kazi, nani yuko gesti mida ya kazi, nani kabebea mbuzi wake kwenye shangingi la serikali! N.k

Watu wa masijala wahakikishe kila chombo cha moto cha serikali kiwe na rangi za nembo husika ili kuongeza uwajibikaji na kupunguza ukilitimba.

Hili litasaidia mambo kama haya!
1. Madereva wa serikali siku hizi wamebuni mbinu ya kuwa na namba za usajili feki (fake plate number) ambazo hubandika siku za weekend na kutumia gari jambo linalochangia uchakavu wa haraka na kuighalimu serikali kufanya matengenezo

2. Madereva wanapokuwa na hayo magari yasiyo na nembo (waliyoweka feki namba binafsi) ni rahisi sana kuuza au kubadilisha vipuli orijino kwenye gereji bubu na kuitia hasara serikali

3. Matumizi ya mafuta yako juu kwasababu magari yasiyo na nembo yanashawishi mizunguko isiyokuwa ya lazima

4. Magari yasiyo na nembo hayaoneshi uwajibikaji kwa wananchi (hili lipo kisaikolojia zaidi)

Nasema hivi kwasababu nimeshuhudia mashangingi kadhaa ya serikali STL au DFPA lakini wakifika mtaani wanabandika namba binafsi mfano DZA!

Kwahiyo mtu kama huyu akiuza kipuli gereji yoyote hakuna atakaye mshitukia!

Updates
Wazo zuri lakini vipi Kama mhusika was wizara atakuwa nikilitimba?
 
Kuna connection imevuja gari LA serikali vijana wanafanyia ngono! Yapakwe rangi za nembo zao harafu tinted yasiwekwe serikali yetu ni ya uwazi kwann kujificha ndo maana hata yanatumika kwa magendo
Duh!Ntupie pm chief

Ova
 
Hivi dhumuni la kuacha gari on wa kiongozi yupo mkutanoni hua ni nini? Nisaidiwe
 
Hivi dhumuni la kuacha gari on wa kiongozi yupo mkutanoni hua ni nini? Nisaidiwe
Wanasema akitoka akute haijapoa ubaridi! Mi zaman nilizani magari ya serikali hayatumii mafuta ya kawaida kama wengine
 
Magari ya Seikali na Mashirika au wakala yanapaswa kuwekwa nembo ubavuni mlangoni ili yafahamike. Dawa ni hiyo tu.
Mashirika ya dini yalianza hili zamani kidogo, na utaratibu uliwekwa na serikali. Sasa ni wakati wa wao kufuata utaratibu walioweka kwa mashirika/taasisi za kidini.
 
Mashirika ya dini yalianza hili zamani kidogo, na utaratibu uliwekwa na serikali. Sasa ni wakati wa wao kufuata utaratibu walioweka kwa mashirika/taasisi za kidini.
Sijui kinachowashinda nn hawa viongozi wetu
 
Inasemekana kuna naibu waziri kaanguka na gari la serikali alikuwa na mchepuko akikimbizwa!.
Nasisitiza magari ya serikali yapakwe rangi ya nembo
 
Habari zilizotufikia mme wa yule mwanamke aliyekuwa anamfukuzia kiongozi kakamatwa kwa uchunguzi wa ajali
 
Habari zilizotufikia mme wa yule mwanamke aliyekuwa anamfukuzia kiongozi kakamatwa kwa uchunguzi wa ajali
Kwani alikuwa dereva wa huyo kiongozi au yeye alikuwa anamfukuza kibaka mla vya wenzie !!??
 
Back
Top Bottom